Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Siku chache zilizopita niliandika uzi unaoitwa: “Watu wanasali, mabomu yanalia. Je, kuna uhuru wa kuabudu?”Ulikuwa ni mwitikio wa kile tulichoshuhudia tarehe 22 na 29 June 2025: waumini wa dhehebu flani wakitawanywa kwa mabomu wakati wakiwa kwenye ibada.
Sikuandika kwa lengo la kutetea mtu, dhehebu au msimamo wa kisiasa. Niliandika kwa kutumia nafasi yangu kama raia kuhoji kama kweli uhuru wa kuabudu upo, na kama upo, unalindwa vipi?
Jana tareh 1 July 2025, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo. Wameeleza msimamo wao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan ibara ya 19(2), ambayo inatambua haki ya kila mtu kuabudu, kuamini na kueneza dini yake. Wamerejea pia ibara ya 18 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu. Katika maelezo yao, TLS wameeleza kuwa walichoshuhudia si sawa na kwamba wanatoa wito wa kuheshimu haki hii ya msingi katika mazingira ya sheria na utulivu.
Issue ya msingi si kwamba TLS wamesema nini, bali sisi kama jamii tunapaswa kujiuliza: haki za msingi kama hizi zikianza kuonekana kama “hatari” au “kosa”, nini kinafuata?
Haki ya kuabudu haijaanza jana. Na wala si ya mtu au kundi maalum. Ni haki ya kila mmoja. Mara nyingi tunajisahau kwamba Katiba hailindi walio wengi tu, bali inalinda pia walio wachache na wakati mwingine hata wasiopendwa. Hiyo ndiyo maana ya sheria kuwa juu ya utashi.

Nimeona pia kuna hoja ambayo imekuwa ikirudiwa sana katika mijadala mbalimbali, hasa mitandaoni, kwamba kanisa la Askofu lilifutwa usajili na Msajili wa Vyama vya Kijamii, hivyo linafanya ibada chini ya kanisa hilo kuwa kinyume cha sheria.
Siwapingi wanaotoa hoja hiyo kwa sababu ni kweli taarifa hizo zimesambaa sana na kwa muda mrefu zimekuwa zikitajwa kama msingi wa hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya waumini wa kanisa hilo.
Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa suala hili halikuishia kwenye mijadala ya mitandaoni bali lilipelekwa Mahakamani, na Mahakama Kuu ilishatoa maamuzi kuhusu suala hilo.
Kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu, ilibainika kwamba kanisa lililotajwa kufungiwa na Msajili si Glory of Christ Tanzania Church linaloongozwa na ndugu Askofu, bali chombo kingine tofauti kwa jina la “Glory of Christ Church.” Pia, Mahakama hiyo ilieleza kuwa notice iliyodaiwa kuwa wa kufuta usajili huo haukuwa rasmi, haikusainiwa, na haujawahi kutumwa kwa kanisa husika.
Kwa msingi huo, Mahakama ilionyesha wazi kuwa hakukuwa na uamuzi wa kisheria uliolifuta au kulipiga marufuku kanisa la Askofu kama taasisi halali iliyosajiliwa kisheria.
SOMA:Kesi ya Kanisa la Ufufuo na Uzim
Hoja yangu itabaki pale pale kama maamuzi ya Mahakama yanayoonesha kuwa hakuna agizo halali la kufuta au kulizuia kanisa hilo, basi hakuna msingi wa kisheria unaoeleza kwa nini waumini wake wazuiwe kuabudu.
Kwahiyo hali halisi inaonesha wazi pengo kubwa kati ya kile sheria inasema na kile kinachotendeka, na hilo ndilo jambo la msingi tunalopaswa kuendelea kulitafakari.