Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki

Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki


Nina maandiko mawili kwenu katika magomvi yenu ya wenyewe kwa wenyewe;

1 Corinth 14: 33; 33 For God is not a God of disorder but of peace—as in all the congregations of the Lord’s people.

Mathew 7:21-23: 21“Not everyone who says to me, ‘Lord, Lord,’ will enter the kingdom of heaven, but only the one who does the will of my Father who is in heaven. 22 Many will say to me on that day, ‘Lord, Lord, did we not prophesy in your name and in your name drive out demons and in your name perform many miracles?’ 23 Then I will tell them plainly, ‘I never knew you. Away from me, you evildoers!’
 
Nilisoma juzi ila sikutoa maoni. Kanisa Katoliki tunabahati ya kuwa na viongozi wa ngazi kwa ngazi mpaka kumfikia Papa au Baba Mtakatifu.

Haya matatizo yangepelekwa kwa kiongozi wake ambae ni Askofu, akishindwa kuyatatua yangeenda kwa Kadinali.

Kuweka haya matatizo hapa ni kuanika nguo chafu nje kwenye kamba.
 
Nilisoma juzi ila sikutoa maoni. Kanisa Katoliki tunabahati ya kuwa na viongozi wa ngazi kwa ngazi mpaka kumfikia Papa au Baba Mtakatifu.

Haya matatizo yangepelekwa kwa kiongozi wake ambae ni Askofu, akishindwa kuyatatua yangeenda kwa Kadinali.

Kuweka haya matatizo hapa ni kuanika nguo chafu nje kwenye kamba.
Halafu uone walivyo na tabia ambayo sijaipenda, yaani kwenda siku moja tu kuambia Mzee Rwaichi hayupo tayari wamekata tamaa. Utadhani hawajui kuwa baba anaumwa
 
Yaani nyie ni kamati ya ufuatiliaji tu! na vipi Halmashauri yenu ya walei? mbona wao hawako nanyi kwenye hili? Fateni sera za kanisa katoliki mambo ni kwa hirakia tuu?
Kama hayo malalamiko Yenu mlisha yapeleka ngazi husika na hata Askofu wa jimbo mmekutana naye.... Sasa huku JF umeyaleta ya nini? Maana ukweli unabaki kuwa mwenye uamuzi wa mwisho juu ya Parokia na hata nani awe paroko ni Askofu wa jimbo
Baraza la Walei nadhani ni chombo cha kumsaidia paroko kufanikisha maendeleo ya Parokia kiimani na ki uchumi Ila si kumuongoza paroko au kumuongoza
Kanisa katoliki halina utamaduni wa waumini kumkatalia padre kuongoza Misa.. lina utaratibu wa kukabiliana na migogoro ya ndani
Kama kwenye Parokia hiyo mmefikia kufanya hayo mliyoyafanya.. basi kuna kila sababu ya sisi tuliosoma post yako hii kuamini kuwa baraza la Walei la Parokia hiyo lina tatizo kubwa na yawezekana kwa sehemu kubwa ndio wanaochangia mgogoro huo ( kama upo kweli) na mtoa post hii ni among the Ring learders.
 
Hapo walei wametafuta mwanya wa kupiga sadaka na miradi ya kanisa Padre anaonekana kathibiti kila kona sasa wanaamua kumpiga majungu. Nani aliwaambia kuwa kuna demokrasia katika kanisa? kuna usemi wa kilatini usemao ROMA LUCUTA CAUSA FINITO maana yake ni kwamba kiongozi wa juu katika kanisa akitamka hakuna kupingwa, linguine kanisa ni tajiri wa waumini haliangaingi kufanya promo ta maupako, kutoa mapepo wala kubeba waamini kwa magari, kama kanisa limewashinda? kuna makanisa mengi hapo mjini akina gwajima , mzee wa upako, kakobe ,mwamposa wote wanataka waumini na kule mtapata hiyo democresia ya kuwapangia mapato na matumizi
 
PAROKIA YA MT. MIKAELI KAWE, DAR ES SALAAM
Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki
Tarehe 04 Novemba 2019

View attachment 1254572
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Juda Thaddeus Ruwaichi, ambaye ndiye Askofu mwenye mamlaka na Paroko wa Parokia ya Kawe, Padre Nicholas Bahati Kundy

Ndugu wanahabari,

UTANGULIZI


Tangu mwaka 2011, Parokia ya Mtakatifu Mikaeli ya Kawe, jijini Dar es Salaam, imekumbwa na mgogoro unaohusisha paroko kwa upande mmoja na walei kwa upande mwingine. Waumini wengi tunapinga utaratibu unaotumiwa na Paroko Nicholas Bahati Kundy kuendesha. Yeye anaendesha parokia kana kwamba ni kampuni ya biashara inayotafuta faida kubwa na bila kujali ubora wa huduma za kiroho kwa waumini.

Tayari tabia hii imesababaisha hasira kubwa kwa waumini mpka kufikia hatua ya Padre Nicholas Bahati Kundy kuzuiwa kusoma misa mara mbili.

Mara ya kwanza, Padre Nicholas Bahati Kundy alizuiwa kusoma misa tarehe 19 Mei 2019. Waumini walitumia mbinu hii kufikisha ujumbe wao kwake. Polisi waliitwa, wakaingilia kati, hali ikatulia, na hatimaye akapata fursa ya kusoma misa, lakini kwa kuchelewa.

Mara ya pili, waumini wenye hasira walimzuia Padre Nicholas Bahati Kundy kusoma misa tarehe 06 Oktoba 2019. Siku hiyo, misa ya kwanzana misa ya pili ilisomwa na Padre mgeni aitwaye Kisoko, wakati misa ya tatu, ilifutwa. Padre Nicholas Bahati Kundy hakujitokeza kabisa kusoma misa yoyote kwa sababu ya hofu na misukosuko kutoka kwa waumini wanaopinga mwenendo wake.

Matukio haya yamekuwa yanaripotiwa katika vyombo vya habari mbalimbali, vikiwemo vyombo vya Kanisa Katoliki, katika namna ambayo haitoi picha halisi kuhusu chimbuko la mgogoro huu. Hivyo, tumeona ni muhimu na lazima kutoa ufafanuzi mfupi ili kuweka kumbukumbu sawa.

SABABU ZA MGOGORO


Kuna sababu nyingi zinazozalisha mgogoro kati ya waumini na Padre Nicholas Bahati Kundy. Kubwa ni kama ifuatavyo:

Mosi, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kufichua hadharani siri za sakramenti ya kitubio. Kwa mfano, aliwahi kufichua siri za kitubio za mzee Francis Katambi katika kikao cha Mashauriano parokiani, jambo lililozua mtafaruku mkubwa. Mpaka leo mzee Francis Katambi hawezi kwenda kufanya kitubio kwa Paroko. Tabia hii ni kinyume cha sheria za Kanisa Katoliki toleo la mwaka 1983.


Pili, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kufuta chaguzi za Jumuiya Ndogo Ndogo pale wanapochagiliwa waumini ambao yeye hawapendi. Aanapofanya uamuzi huu hatoi sababu kwa waumini. Hivyo, waumini humgomea. Migogoro ya hivi karibuni inatokana na sababu hii. Amefuta uchaguzi katika Jumuiya nne zikiwemo Jumuiya ya Mt. Stefano na Mt. Martin Deporres. Alipoagiza uchaguzi urudiwe waumini wakakataa kwa hoja kwamba wao wamekwishamaliza kufanya uchaguzi wa viongozi wanaowataka. Tabia hii ni kinyume cha ibara ya tisa (9) ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Tatu, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kuendesha shughuli za Parokia bila kushirikisha vyombo vya ushauri vilivyo chini ya Halmashauri ya Walei, kama vile Kamati Tendaji. Kwa mfano, alisaini mkataba na kusimamia ujenzi wa Ukumbi wa Mkitano wa Parokia bila kushirikisha kikao chochote cha Kamati Tendaji. Hata Katibu wa Halmashauri ya Walei, Mzee Makwabe, ambaye ni mtendaji mkuu wa Parokia, hakushirikishwa. Mwenendo huu ni kinyume cha matakwa ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Nne, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kutumia sadaka ya Parokia kinyume cha bajeti ya Parokia iliyopitishwa na Kamati ya Uchumi na Fedha ya Parokia. Kwa mfano, mara kadhaa, fedha inayopelekwa benki kila siku ya Jumanne inakuwa ni pungufu ya makusanyo yaliyopatikana siku ya Jumapili iliyotangulia. Akiulizwa na Kamati Tendaji, jawabu lake ni kwamba, “mimi ndiye bosi wa Parokia, naweza kusonga mbele bila kuwasikiliza walei, sio lazima niombe ushauri kwa walei, kwani mwisho wa siku mimi Paroko peke yangu ndiye nawajibika kwa Askofu wa Jimbo.” Tunaona kuwa, mwenendo huu ni kinyume cha matakwa ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Tano, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kutoa huduma ya sakramenti ya ndoa kwa kutoza gharama kubwa zaidi kuliko viwango vilivyopitishwa na Kamati Tendaji ya Parokia, yaani shilingi 136,000/= pekee. Kwa mfano, mtoto wa muumini mmoja aitwaye Mzee Masanja alitakiwa kulipa shilingi 370,000/= kama sharti la ndoa yake kufunguwa. Paroko Kundy aliposafiri, padre msaidizi aitwaye, Padre Sentaro, alifunga ndoa hiyo kwa gharama ya shilingi 50,000/= pekee. Kwa ufupi, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa anatoa huduma ya sakramenti ya ndoa kama huduma ya kibiashara.


Na sita, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kushindwa kutoa huduma ya misa ya mazishi kwa waumini wake pasipo sababu za msingi. Kwa mfano, muumini aitwaye Lucy Mduda alipofariki hakupata huduma ya misa ya mazishi. Mazishi yaliendeshwa na Mzee Mgila kwa kutumia uzoefu wake kama Katekista mstaafu.

Haya malalamiko yetu yamefafanuliwa kwa kina katika barua yetu kwenda kwenye Ofisi ya Askofu Mkuu Jimboni, iliyowasilishwa tarehe 07 JUni 2019. Tunaambatanisha barua hii kama “Kiambatanisho A.” Aidha, malalamiko haya yalifafanuliwa zaidi kwenye barua za ushahidi zilizoandaliwa kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Walei Jimbo, Padre Vitalis Kasembo. Tunaambatanisha barua hizi kama “Kiambatanisho B.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Tayari malalamiko haya yamefikishwa katika ngazi za juu za uongozi wa Jimbo. Kiongozi wa Dekania na Paroko wa Mwananyamala, Padre Penedict, alikuja na kutusikiliza. Baadaye, Mkurugenzi wa Baraza la Walei Jimbo, Padre Vitalis Kasembo alikuja pia. Hivi karibuni, tulikutana na Askofu Mkuu, Juda Thadeus Ruwaichi na kuongea naye.

Kadiri tunavyosubiri kukutana na viongozi wa Jimbo, ndivyo mahusiano kati ya waumini na Paroko yanavyozidi kudorora. Mfano, kila mara viongozi wa kwaya na Jumuiya Ndogo Ndogo wanaondolewa madarakani. Tunaona kwamba, uongozi wa Juu wa Kanisa unakuwa tayari kusikiliza lakini hauna haraka ya kutoa majibu kwa hoja zetu. Mara ya mwisho, tulikuwa na miadi ya kuonana tena na Askofu Ruwaichi juzi tarehe 01 Novemba 2019. Masisita walitwambia kwamba hayupo na hakuna siku mbadala aliyoitaja kwamba tunaweza kumwona. Ni kama tumetekelezwa.

WITO KWA UONGOZI WA JIMBO

Hivyo, tunapenda kutumia fursa hii kumfahamisha Askofu Juda Thadeus Ruwaichi kwamba, bado tunayo nia ya kuonana naye ili tuweze kupatiwa majibu ya hoja zetu. Hatupendi kuona fedha inateka dini ndani ya Kanisa Katoliki.

Taarifa hii imeshuhudiwa na:

SAMWEL MGILA
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji
Simu: 0652763968

DAVID KULWA
Katibu wa Kamati ya Ufuatiliaji
Simu: 0747508633

View attachment 1254569View attachment 1254570
Munahangaika na sadaka hakuna lolote
 
Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba kijana anayeandaliwa kuwa padre uanzia seminari ndogo akiwa darasa la tano, yaani darasa la sita na la saba ndio seminari ndogo kisha f1 hadi fvi na kuendelea huko....pamoja na kuchukuliwa akiwa mdogo bado vitu kama familia anamotoka huangaliwa kwa umakini sana. Malezi ya mapadre wa kule hayaishii hapo jamaa wanaangaliwa sana hdi kwenye parokia zao....nimeandika haya baada kuona kunautofauti sana kati ya Mapadre wa jimbo la Bukoba, na majimbo mengine.

Hapa nilipo kina Padre Nicholas Bahati Kundy ni wengi sana hadi waumini wengi tunaanguka kiimani!
 
Wakatoriki nao wamekuwa kama walokole. Migogoro kibao. mmetia aibu. lakini bado ni kanisa stable kama wakitatua migogoro hii mapema mapema.
Jimbo kuu la Dar es salaam Lina Parokia zaidi ya 75. Hiyo Ni Parokia Moja tu.
 
Kuungama kwa Padre Kuna maneno Kuna kijana mmoja alishawahi kwenda kuungama kwa Padre dhambi ya uzinzi kuwa alizini na msichana akamtaja jina huyo msichana .Kumbe yule msichana ni hawara yake na padri aliyekuwa akiungamisha.

Kilichofuata yule padri alitoka na yule msichana jioni kwenda kunywa pombe akamtandika makofi yule msichana na kumtukana kuwa ni Malaya anatembea hovyo akamtajia na mvulana anayetembea naye.Yule msichana akashtuka akasema unanionea ulnani kakwambia huo uongo? Padri akasema kaniambia kijana mwenyewe alipokuja kuungama
Kwenye kuungama hakuna kutaja jina la uliyeshiriki naye kutenda dhambi. Acha kupotosha.
 
Jimbo kuu la Dar es salaam Lina Parokia zaidi ya 75. Hiyo Ni Parokia Moja tu.
Sasa zipo parokia 120. Hiyo kamati tendaji ya parokia ya Kawe ndio wanaochochea huo mgogoro kati ya paroko na waumini. Wamebanwa kuchakachua sadaka na kuwapa marafiki zao tenda za ujenzi wa ukumbi. Njaa mbaya sanaaa.
 
Mkuu Nalendwa,

Kwa Mtazamo wangu; waamini inaonekana wana kiburi. Kanisa lina njia za kutatua migogoro kama hii:

• Walipaswa kuwa watii kwa kiongozi na Mchungaji Mkuu wa Jimbo. Kama wamepangiwa appointment na ikashindikana, haiwapi tiketi ya kutafuta umaarufu.

• Hakukuwa na sababu ya press release kwa mambo ya ndani na ambayo yanafuatiliwa. Athari yake kwa Mama Kanisa ni kubwa kuliko faida.

• Hata kama mtu amekosea, kuna namna ya kuwasilisha hoja hizo kwa unyenyekevu, busara na Ukristu wa hali ya juu. Hakuna mkamilifu, ninakuhakikishia, hata wao sio wakamilifu.

• Waamini hawana subira na wana mihemuko mithili ya vijana wanaobalehe. Hawalijui vizuri Kanisa letu.

• Wanapaswa kujua kuwa mwenye maamuzi ya mwisho juu ya Jimbo ni Askofu ambaye hawezi kuingiliwa na Askofu mwingine yeyote, hata Askofu wa Roma (Baba Mtakatifu), hivyo, wanapaswa kumheshimu Kiongozi wa Kanisa Mahalia.

• Zaidi ya yote; Kanisa Katoliki siku zote huwa halina haraka, na haliendeshwi kwa kufuata hisia za waamini.

Huwa linachukua muda kujihakikishia ukweli kabla ya kufanya uamuzi. Kwanini wanashindwa kuwa wavumilivu?

Kanisa Katoliki sio chama cha siasa.
 
Ingawa mimi si mkatoliki ila hii njia uliyoitumia kuweka hadharani hivi huu mgogoro siyo sahihi labda kama mngetumiana wakatoliki wenyewe, Jaribuni kutatua migogoro yenu wenyewe ndanindani kwa ndanindani pasi na kuonyesha watu wa nje ambao wengi badala ya kuwasaidia watawadhiaki na kuwakashfu na hivyo lengo kutofikiwa

Nina imani malalamiko yenu viongozi wenu wanayashughulikia kama mlishawaeleza kuweni na subira majibu au hatua wakati mwingine zinachukua muda kulingana na tatizo husika
Kuna nini cha kuficha sasa hapo, unatumia kifungu gani cha sheria juu ya hiyo hoja yako
 
Back
Top Bottom