Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki

Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki

Jimbo kuu la Dar es salaam Lina Parokia zaidi ya 75. Hiyo Ni Parokia Moja tu.
Ni kama 117 hivi achilia mbali parokia teule! Tunawasubiri hao Msimbazi tarehe 23Novemba,2019 tuone wao watakuwa na madhara gani katika kulitegemeza kanisa
 
Hapo walei wametafuta mwanya wa kupiga sadaka na miradi ya kanisa Padre anaonekana kathibiti kila kona sasa wanaamua kumpiga majungu. Nani aliwaambia kuwa kuna demokrasia katika kanisa? kuna usemi wa kilatini usemao ROMA LUCUTA CAUSA FINITO maana yake ni kwamba kiongozi wa juu katika kanisa akitamka hakuna kupingwa, linguine kanisa ni tajiri wa waumini haliangaingi kufanya promo ta maupako, kutoa mapepo wala kubeba waamini kwa magari, kama kanisa limewashinda? kuna makanisa mengi hapo mjini akina gwajima , mzee wa upako, kakobe ,mwamposa wote wanataka waumini na kule mtapata hiyo democresia ya kuwapangia mapato na matumizi
Katoliki kila kitu kinauzwa ndoa inauzwa lazima utoe pesa,mazishi Yanauzwa lazima utoe pesa nk makanisa mengine hizo huduma haziuzwi
 
Acha dhambi zenu zifichuliwe hadharani!

Ati kitubio!
 
Mama Amon, sidhani kama kulikuwa na haja ya kuweka hapa hili swala cz mmeshalifikisha pahala husika.

Mmlichokifanya ni kumuaibisha kiongozi wenu wa kiroho.
Ametaka kuaibishwa!

Zama za kufuga wanafiki zinaanza kwisha sasa!
Awe safi au atoke!
Madhabahu zinachafuliwa sana .. ..
 
Mara ya kwanza, Padre Nicholas Bahati Kundy alizuiwa kusoma misa tarehe 19 Mei 2019. Waumini walitumia mbinu hii kufikisha ujumbe wao kwake. Polisi waliitwa, wakaingilia kati, hali ikatulia, na hatimaye akapata fursa ya kusoma misa, lakini kwa kuchelewa.


Mambo ya kusali chini ya bunduki yalianzia kwa waprotestant na sasa yanapanda kwenda Vatcan, hii ni aibu kwetu wakristo, tujiulize je tumeshindwa kuutumia ulinzi wa Kristo ambao ni mkubwa Zaidi mpaka tukatumie polisi? Je tukishindwa kulindwa na polisi si tutaanza kulindwa na waganga wa kienyeji?
 
Mkuu Nalendwa,

Kwa Mtazamo wangu; waamini inaonekana wana kiburi. Kanisa lina njia za kutatua migogoro kama hii:

• Walipaswa kuwa watii kwa kiongozi na Mchungaji Mkuu wa Jimbo. Kama wamepangiwa appointment na ikashindikana, haiwapi tiketi ya kutafuta umaarufu.

• Hakukuwa na sababu ya press release kwa mambo ya ndani na ambayo yanafuatiliwa. Athari yake kwa Mama Kanisa ni kubwa kuliko faida.

• Hata kama mtu amekosea, kuna namna ya kuwasilisha hoja hizo kwa unyenyekevu, busara na Ukristu wa hali ya juu. Hakuna mkamilifu, ninakuhakikishia, hata wao sio wakamilifu.

• Waamini hawana subira na wana mihemuko mithili ya vijana wanaobalehe. Hawalijui vizuri Kanisa letu.

• Wanapaswa kujua kuwa mwenye maamuzi ya mwisho juu ya Jimbo ni Askofu ambaye hawezi kuingiliwa na Askofu mwingine yeyote, hata Askofu wa Roma (Baba Mtakatifu), hivyo, wanapaswa kumheshimu Kiongozi wa Kanisa Mahalia.

• Zaidi ya yote; Kanisa Katoliki siku zote huwa halina haraka, na haliendeshwi kwa kufuata hisia za waamini.

Huwa linachukua muda kujihakikishia ukweli kabla ya kufanya uamuzi. Kwanini wanashindwa kuwa wavumilivu?

Kanisa Katoliki sio chama cha siasa.

Kuna mashirika yapo very straight kwa Mapadri wao. Padri anakiuka taratibu wanamuondoa. Waamini wapo siku zote hapo Kawe haiwezekani wawe na tatizo na Padri huyu tu wa sasa.

Parokia niliyopo sasa tulikuwa na tatizo la Paroko kuenda kinyume na taratibu, tuliwasilisha malalamiko kwa shirika lake likachunguza fasta akaondolewa, sasa hivi wameleta Mzungu mambo yanaenda Safi kabisa. Hatuna simile na Padri anayeturudisha nyuma.

Huyu Padri anaonekana anawakwaza waamini kwa tabia zake kutoa maungamo ya mtu, kudokoa sadaka n.k mpaka waumini wamefikia hatua ya kumuanika basi washavumilia sana.
 
Mimi nimependa avatar ya @Mama Amon

Huyu hapa?

1573822306103.png
1573822306103.png
 
Kwa kashfa hizo huyo Padre Atakuwa ashachepuka na waamuni wa kike hapo??

Ova
Ulikuwa unaitafuta hii point ya kuchepuka umeikosa!! Pole, na usilazimishe tuhuma!

Ushauri Kwa waumini: Hameni parokia abaki peke yake ale Vumbi!
 
Back
Top Bottom