Tamko la wazee Chadema: Mbowe ndiye kiongozi pekee barani Afrika asiyelipwa posho wala malipo yoyote na chama chake, anajitolea!

Tamko la wazee Chadema: Mbowe ndiye kiongozi pekee barani Afrika asiyelipwa posho wala malipo yoyote na chama chake, anajitolea!

johnthebaptist,
Wazee wa jimboni kwake wanamkataa na wanajua ni mpigaji. Hao wazee wa Chadema wanatwanga maji kwenye kinu. Nenda jimboni kwake Wazee na vijana hawamtaki kabisa. Mpiga madili na alitaka JPM aweke lockdown ili tuteseke.
 
Mtu mweusi hawezi fanya kazi bure haitokaa itokee duniani na ahela/peponi

Yupo kwa ajili ya maslahi tusidanganyane wazee, kwani bila yy chama hakiendi?
 
Amesha wapiga kahawa wazee wa watu na alkasusu Ila mbowe ajiandae kua Kama lipumba Mana chama kinaenda kua mzigo kwake
Baraza la wazee wa Chadema limetoa tamko lake la kumtetea Mwenyekiti wa chama hicho dhidi ya njama ovu zinazotekelezwa na wabunge waliohamia CCM wakimtumia Mwita Waitara aliyewahi kuwa mlinzi wa Mbowe.

Katika tamko lake baraza la wazee limetaja sifa kuu 3 za Mbowe:

Mosi Mbowe ni mwenyekiti pekee wa chama cha siasa barani Afrika ambaye hapokei posho wala malipo yoyote kutoka kwenye chama chake anaitumikia Chadema kwa kujitolea.

Pili, Mbowe ndiye Mwenyekiti pekee wa chama cha siasa nchini anayeaminiwa na chama pamoja na wanachama ambao wameamchagua mara zote na amedumu katika uongozi kwa takribani miaka 25.

Tatu, Mbowe ndiye kiongozi pekee nchini aliyeingia katika uongozi akiwa tajiri na serikali kumfanyia figisu hadi anafilisika bila kuogopa wala kukata tamaa tofauti na wenyeviti wa CCM mzee Mwinyi, mzee Mkapa na mzee Kikwete ambao waliingia wakiwa maskini na kuondoka wakiwa matajiri.

Mwisho wazee hao wamemtaka Mwita Waitara kama ni mzalendo na siyo mnafiki anayejipendekeza, aanze kuhoji ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM.

Source: Ayo TV


Maendeleo hayana vyama
 
Mbowe arudishe bilion nane. Aache kuwatumia wazee kuhalalisha ufisadi wake
Jibu hoja kwa hoja, hapo inaonesha namna ambavyo vijana hatufikirii vema.
Mimi nawauliza, je nini malengo ya tajir kufanya kazi bure na Kama anafilisiwa lakin bado hakati tamaa basi Kuna mawili; anafaidika ama kaamua kuwa mzalendo
 
Back
Top Bottom