Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

Edward

Filamu ya misukosuko ukiitazama hata kama imeigizwa kipindi kile bado inauzito na ubora wa kiwango cha juu.

Wanaweza kuirudia tena ile filamu kipindi hiki teknolojia ikiwa imekua.
Kama kuna maboresho wanaweza kuongeza ongeza au kupunguza baadhi ya ishu.

Hao wakiigiza hakunaga kulamba midomo au kutikisa tikisa makalio kama Wapuuzi.
Mkuu nilishangaa sana kumsikia Jimmy Mponda akisema kuwa vipande vya mapigano baina yake na Seba ilikuwa ni ukweli kabsa sio green screen. Walikuwa wakizichapa haswa na ndivyo tulivyokuwa tukiona kwenye luninga! sasa kipindi hiki mara fulani anamuomba ngono fulani! mara fulani anataka kutoa mimba! yaani ujinga juu ujinga chini
 
Ukitaka.kujua ujinga wao we muulize lengo kuu la yeye kufanya tamthilia zenye maudhuo haya ni nini!? Nakuhakikishia hajui kwenye hadhira yake anataka kufanikisha nini.

Kabla haujamuhukumu, waylize serikali na Viongozi wake wanapopitisha sera yoyote kama wameisoma na wameielewa na wanadhani italeta badiliko Gani ndani ya Mtanzania mmoja mmoja?! Hakutakuwa na jibu

Halafu nenda umuulize mwalimu anapofundisha Darasa... Anadhani anachofundisha alaenga kiwe na athari ipi chanya katika maisha ya mwanafunzi moja mmoja.. ukiachilia mbali yeye kufaulu mitihani?! Hawezi kuwa na jibu.

Toka nenda kamuulize mzazi..anapomfunza mtoto mafunzo aliyoyachagua..anatarajia yalete impact ipi kwa mtoto hapo baadae..katika mia labda wawili tu ndio watakupa maelezo ya kuridhisha.

Kwa kifupi maisha ya Watanzania wengi kwa ngazi zote ni maisha ya kubeti maisha ya kimachinga. Unapapasa papasa ukibahatika Alhamduliah. Ukikosa basi Insh'allah. Hakuna Nia ya dhati ya kupanga na kujitahidi kufuata njia.

Athari za mfumo huo unaziona kwenye elimu mtoto anapelekwa alikofaulu..wakati mmingine ni fluke tuu. Na inturn imetufanya hatujui tunataka kufanya nini mpaka tufeli..maana Hata ukitaka mwisho utakwenda ulipopangiwa tuu.

Tunajenga hovyo hovyo maana hatuna mpango thabiti. Tukibahatisha hapo hapo tunajenga .. mwendelezo wa kubeti. Ukiwatazama bodaboda barabarani na ujinga yao unaweza kudhani ni wao tuu ila mfumo wao na tabia zao barabarani ndizo tabia za Watanzania asilimia 98. Tunakwenda una upepo na upenyo.. ikitolea umefinywa.. umekufa na mengine kama hayo basi ni bahati mbaya.

Haya ya umbeya ujinga nk.. ni reflection ya kinachoendelea mitaani.. ila mtunzi hatujui lengo lake la kutuonesha ni nini.. tujifunze tuwe wambea ,wanafiki, wezi na mashoga? Au ayapinga haya?! Kwa kifupi sioni wanachotaka ku-achieve.. na Hadith isiyokuwa na lengo ni kelele tuu.

Hili ni la BASATA.. lakini ngoja Je BASATA wana kichujio cha maudhui?! Wanakitoa.wapi kama taifa halina dira ya Maadili?!

Mungu Aendelee kukulinda Mtoa Mada.
MAUA YAKO MKUU 🌹🌸
 
MAUA YAKO MKUU [emoji257][emoji254]
Asante sana Ndugu yangu. Uwe na Ijumaa njema.

Lakini usiache kupinga Ujinga kwa Nguvu zote kila ukisikia au kuuona pahali popote.

Tukiwakalia kimya wajinga watadhani wako sahihi.
 
Kuna Jamba moja sijalielewa, huku kwenye film hii nmeona kama watu wenye kipato ndani ya tamthilia wanazitafta kwa kuua watu na kafara, je mnataka kutuaminisha Kila kupata pesa lazma uloge au utoe kafara, Tamthilia nzur kimuonekano lkn ukiichunguza sana hutaiangalia.
 
Asante sana Ndugu yangu. Uwe na Ijumaa njema.

Lakini usiache kupinga Ujinga kwa Nguvu zote kila ukisikia au kuuona pahali popote.

Tukiwakalia kimya wajinga watadhani wako sahihi.
Kitaalamu upo sahihi Mkuu!
A luta continua
 
Mdogo wangu hapa nakuunga mkono kiukweli hata ukisema hiyo movie inatoa funzo gani siwezi kukwambia,movie nzima ni watu kupendana hovyohovyo,nashangaa wanavoikuza kumbe hamna kitu
Kuna lijamaa eti mpali na huba eti huba ni kali

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Jamba moja sijalielewa, huku kwenye film hii nmeona kama watu wenye kipato ndani ya tamthilia wanazitafta kwa kuua watu na kafara, je mnataka kutuaminisha Kila kupata pesa lazma uloge au utoe kafara, Tamthilia nzur kimuonekano lkn ukiichunguza sana hutaiangalia.
Mkuu!
Sio kweli wote wanapata fedha au Mali kupitia uchawi au ulonzi (Hapa nadhani Mshana Jr ) anaweza kunisaidia.
Ila nikupe zoezi kidogo katazame tamthilia ya Lupin, inayomhusu Assane Diop kutoka Senegal, ndani humo utaona utamu wa uandishi wa visa na mikasa wa huyu mwamba akisumbua Jiji la Paris . Shida kubwa ni kuwa waandishi wa visa na mikasa hawaumizi vichwa kwenye kutafuta mada zenye uzito kwa jamii. Nijeria wnaingiza filamu na tamthilia za Kichawi ila sio wote Mkuu.
 
Mamangu hataki kuonana king'amuzi Cha DSTV sababu hakuzoea filamu za kiswahili kama hizo. Ndio maana filamu za Azam za kituruki zitabaki kua family friendly daima.
 
Mamangu hataki kuonana king'amuzi Cha DSTV sababu hakuzoea filamu za kiswahili kama hizo. Ndio maana filamu za Azam za kituruki zitabaki kua family friendly daima.
Marehemu Bibi mpaka anafariki alipenda sana kutazama tamthilia za Kinejira kutoka kituo cha Iroko TV. Ila hizi za kina Hemed PhD alikuwa akikataa katu katu!
 
Huba ni filamu ya ma socialite na ma model kushow off, hakuna filamu pale. Filamu zipo kenya angalia magic east sisi ni wababaishajii
 
TAMTHILIA YA HUBA HAIENDANI NA JINA LAKE. KINACHOENDELEA NI UPOTOSHAJI NA UHUNI TUU.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanafilamu wengi walikuwa wakilalamika hakuna wawekezaji katika tasnia ya filamu ndio maana kazi zinazotoka ni mbofumbofu. Miaka ya hivi karibuni kumetokea mabadiliko kidogo yenye matumaini katika tasnia hii baada ya dunia kuhama kutoka analojia kwenda dijitali. Uwepo wa Dstv na makampuni mengine umekuwa kichocheo cha ukuaji wa tasnia ya uigizaji hapa nchi.

Wawekezaji haitakuwa kisingizio tena. Watanzania walitarajia kuona kazi nzuri zenye kupendeza, zenye kusisimua, utunzi wenye ubunifu wa kipekee, tamthilia zenye mipangilio ya visa, matukio na maneno ya kisanaa yenye kuleta akili mpya ndani ya jamii.
Lakini Taikon ninasikitika kuwa bado kuna ombwe kubwa katika Filamu zetu.

Ukiangalia uigizaji wa wasanii wetu hauna tofauti na ule uliokuwa unafanyika sekondari. Yaani ni kama watoto wadogo hivi ambao wanaigiza Kibabababa na kimamamama.

Ninaamini Waigizaji hawana makosa kwa sababu muigizaji anaigiza kulingana na mtunzi na muongozaji atavyotaka filamu ichezwe. Tatizo kubwa la Tasnia ya filamu hapa nchini ipo kwa Watunzi na waongozaji wa filamu.
Uwezo wa Watunzi upo chini sana. Mtunzi ndiye chanzo cha Filamu. Yeye ndiye anayeandaa kisa, matukio, wahusika, mandhari nzuri.k.
Muongozaji wa filamu ambaye pia anaweza kuwa mtunzi yeye kazi yake ni kuwa katika ulimwengu halisi na kuchagua wahusika na mandhari halisi inayoendana na simulizi ya mtunzi hata kama ni ya kubuni. Muongozaji wa filamu lazima amuelewe mtunzi alikuwa anapicha gani kichwani mwake katika stori yake. Ndio maana inashauriwa kama mtunzi yupo ni bora muongozaji wa filamu amshirikishe ili filamu itoke kama ilivyokusudiwa.

Tuachane na mambo hayo. Turudi kwenye mada.

1. Filamu za Bongo zinatatizo la misconceptions.
Nafikiri hii inatokana na watanzania wengi pia kuwa na tatizo hili.
Wabongo wengi tunatatizo la misconceptions katika baadhi ya ishu. Mfano wabongo wengi wanashindwa kutofautisha kati ya heshima na Woga.
Sio ajabu ukamsikia mtu akisema ukiwa na pesa unaheshimika wakati heshima inatokana na matendo yenye heshima, maadili mema. Badala ya kusema ukiwa na pesa unaogopeka.

Upendo Vs Tamaa.
Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha kati ya upendo na tamaa. Na hiki ndicho kinachojitokeza kwenye filamu ya huna.
Huba kwa lugha nyingine huitwa upendo "mapenzi ya dhati" ambapo pakiwa na huba automatically hakuwezi kuwa usaliti.

Lakini ukitazama kwenye tamthilia ya huba kuna hiyo misconception ya kuchanganya huba na tamaa.
Mtunzi anafikiria kila mapenzi ni HUBA. Wakati mapenzi yasiyo ya dhati huitwa tamaa. Na mapenzi ya kweli ndio huitwa HUBA.

Ukifuatilia kinachoendelea kwenye tamthilia hiyo utagundua kinachoendelea ni umalaya, uhuni na tamaa mbaya. Na wala hakuna kitu kinachoitwa Huba kama jina la tamthilia lilivyo.

Umalaya, uchafu, na uasherati uliovuka mipaka ndicho kinachoendelea humo ambapo ni kinyume cha Huba. Kuchukuliana Mabwana, kuchukuliana Wake.
Mara Mama anatoka na Kijana wake wakiume.
Mara Baba "JB" anatoka na Mke wa Mkwe wake "Tima" yaani uchafu uchafu tuu. Filamu inanuka uchafu tuu. Hakuna huba hata sehemu moja.

2. Kuwajibika kisheria hakuna.
Mtu kafanya uhalifu kwa mfano kaua au kateka. Mtunzi hajaandaa kisa cha namna ya kushughulikia wahalifu katika simulizi yake.
Jambo hilo limejitokeza pia katika tamthilia ya wimbi. Tukio la utekaji limetokea, hiyo ni jinai ni lazima mtunzi angeandaa wahusika wengine wa kisheria kama polisi wakifuatilia tukio hilo.
Haya huku kwenye tamthilia ya Huba, Mke wa JB aliuawa, lakini ufuatiliaji wake hauridhishi ni kama kesi imetekelezwa hewani.

Angalau Pazia walijitahidi kwenye kipengele hiki.
Mnashindwa na Wakenya kama kwenye Semina, Kovu, n.k.
Mtunzi lazima ukishatunga kisa cha uhalifu lazima jicho lako na kalamu yako iwe kali mno kuhakikisha unaandaa tukio jingine mbele kumuadhibu mhalifu na kuleta madhara makubwa yatokanayo na huo uhalifu ili jamii ijifunze kuwa uhalifu sio mzuri. Watu waogope.

Lakini ninyi mnafundisha Watu umalaya, kudanga, kufanya uasherati. Yaani mawazo kama watoto wanaobalehe Balehe hivi muda wote kuwaza mapenzi tena katika namna nyepesi kabisa.

Ati huyu kamtongozo huyu kisha Kalala naye, kisha kumfuata tena Dadaake Kalala naye, mara Kalala na mama yake.
Mara mkwe na mkwe wanalalana tena. Mpaka unajiuliza hivi haya mambo yanafanywa na watu wenye akili timamu kweli.
Tena bila aibu yapo live nchi nzima Watu waone kuwa Watanzania ni wajinga kwa kiwango hiki.

Badilikeni bhana!

3. Ubunifu katika Visa hakuna.
Ubunifu wa migogoro hakuna hata unajiuliza hivi tamthilia maana yake nini. Yaani unakuta kipande kizima kinaenda Watu wanajizungusha zungusha tuu.

Alafu kuna ile kasumba mbaya ya kudhani kupiga piga kelele na kutupiana maneno makali ati ndio migogoro. Embu acheni hizo.

Kwa mfano kwenye filamu ya Huba mgogoro ambao ungevutia zaidi ni ule wa kuchunguza nani aliyemuua mke wa JB?
Mhusika mmoja anafuatilia kuhakikisha muuaji anapatikana mhusika mwingine anakazana kuficha.
Upande mwingine mgogoro mwingine wa kuchunguza mali za JB zinatokana na nini na sio iishie tuu kwenye mambo ya kishirikina, kusadikika ambayo hayana uhalisia.

Haya athari za baba na mama kuachana lazima mgogoro mwingine ungezuka kwa kuonyesha jinsi watoto wanavyopata tabu, na lazima watoto wapewe kipande wacheze.

Kwa vile jina la tamthilia ni HUBA, lazima kuna wahusika wawili ambao wangekuwa wanapendana sana kiasi kwamba nguvu ya mapenzi ingeonekana.
Wengine wanajaribu kuyasukasuka hayo mahusiano na kuyateteresha lakini wahusika hao ( love birds) wanapitia hizo changamoto lakini wanashinda majaribu.
Hivyo ndivyo mambo yanavyoenda.

Sasa ushasema Huba alafu muda huohuo unaonyesha nguvu ya Pesa kwamba pesa inaweza kuvunja Huba. Hii haipo hivyo. Labda kama huba yenye maana ya kudanga hapo sawa.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Yaani umegusa sehemu muhimu sana kwenye mapungufu ya filamu zetu, sehemu ambayo wengi hatupendi kuiongelea. Unajua social media na entertainment industry e.g.music etc zinatakiwa pia zi-shape thinking na direction ya fikra za watazamaji ambao ni wananchi mbali ya kuburudisha Ukiangalia kwenye upande wa phychology , hizi platform zikitumiwa vibaya zinaweza kushape social-culture ya jamii negatively na zikitumiwa vizuri zinaweza kupromote good culture na behaviour za community at large ambao ndio watazamaji na ni wengi ajabu.

Ebu tumulike tochi kwenye maneno/ujumbe wa miziki pendwa ya kibongo (bongo fleva), twende tuangalie video zao;hakuna tofauti na porno iliyohalishwa, kwenye upande wa tamthiliya umekwisha elezea vizuri hapo juu. Uko sahihi uzoefu ni muhimu kwa waandishi na madirector wa tamthiliya zetu lakini elimu husika,utaalamu husika ni muhimu zaidikuwawezesha kwenda beyond entertaining audience na kujikita kutoa mafunzo, ufahamu, elimu kwa walengwa watazamaji.
 
Hii kazi yao haina mvuto hata misamiati ya sanaa (literary jargon) hakuna, maneno mengi ni kama ya form one B wa kule kwetu Marendego.
Mkuu Mtibeli Taikon hivi main Character ni nani kwenye hiyo huba?
Ha ha ha ha Kwa akili za mtunzi utakuta Tima na Yule jamaa msomali
 
Huba ni filamu ya ma socialite na ma model kushow off, hakuna filamu pale. Filamu zipo kenya angalia magic east sisi ni wababaishajii
Sasa ni heri waseme kuwa HUBA ni Reality Show tu kama vile Young, Famous & African halafu waweke na PG au Rated X kabsa maana tunafundisha watoto wetu upumbavu.
 
"Ukifuatilia kinachoendelea kwenye tamthilia hiyo utagundua kinachoendelea ni umalaya, uhuni na tamaa mbaya. Na wala hakuna kitu kinachoitwa Huba kama jina la tamthilia lilivyo.

Umalaya, uchafu, na uasherati uliovuka mipaka ndicho kinachoendelea humo ambapo ni kinyume cha Huba. Kuchukuliana Mabwana, kuchukuliana Wake.
Mara Mama anatoka na Kijana wake wakiume.
Mara Baba "JB" anatoka na Mke wa Mkwe wake "Tima" yaani uchafu uchafu tuu. Filamu inanuka uchafu tuu. Hakuna huba hata sehemu moja"

Hapa umemaliza Mkuu.
 
Ukitaka.kujua ujinga wao we muulize lengo kuu la yeye kufanya tamthilia zenye maudhuo haya ni nini!? Nakuhakikishia hajui kwenye hadhira yake anataka kufanikisha nini.

Kabla haujamuhukumu, waylize serikali na Viongozi wake wanapopitisha sera yoyote kama wameisoma na wameielewa na wanadhani italeta badiliko Gani ndani ya Mtanzania mmoja mmoja?! Hakutakuwa na jibu

Halafu nenda umuulize mwalimu anapofundisha Darasa... Anadhani anachofundisha alaenga kiwe na athari ipi chanya katika maisha ya mwanafunzi moja mmoja.. ukiachilia mbali yeye kufaulu mitihani?! Hawezi kuwa na jibu.

Toka nenda kamuulize mzazi..anapomfunza mtoto mafunzo aliyoyachagua..anatarajia yalete impact ipi kwa mtoto hapo baadae..katika mia labda wawili tu ndio watakupa maelezo ya kuridhisha.

Kwa kifupi maisha ya Watanzania wengi kwa ngazi zote ni maisha ya kubeti maisha ya kimachinga. Unapapasa papasa ukibahatika Alhamduliah. Ukikosa basi Insh'allah. Hakuna Nia ya dhati ya kupanga na kujitahidi kufuata njia.

Athari za mfumo huo unaziona kwenye elimu mtoto anapelekwa alikofaulu..wakati mmingine ni fluke tuu. Na inturn imetufanya hatujui tunataka kufanya nini mpaka tufeli..maana Hata ukitaka mwisho utakwenda ulipopangiwa tuu.

Tunajenga hovyo hovyo maana hatuna mpango thabiti. Tukibahatisha hapo hapo tunajenga .. mwendelezo wa kubeti. Ukiwatazama bodaboda barabarani na ujinga yao unaweza kudhani ni wao tuu ila mfumo wao na tabia zao barabarani ndizo tabia za Watanzania asilimia 98. Tunakwenda una upepo na upenyo.. ikitolea umefinywa.. umekufa na mengine kama hayo basi ni bahati mbaya.

Haya ya umbeya ujinga nk.. ni reflection ya kinachoendelea mitaani.. ila mtunzi hatujui lengo lake la kutuonesha ni nini.. tujifunze tuwe wambea ,wanafiki, wezi na mashoga? Au ayapinga haya?! Kwa kifupi sioni wanachotaka ku-achieve.. na Hadith isiyokuwa na lengo ni kelele tuu.

Hili ni la BASATA.. lakini ngoja Je BASATA wana kichujio cha maudhui?! Wanakitoa.wapi kama taifa halina dira ya Maadili?!

Mungu Aendelee kukulinda Mtoa Mada.
Cmnt zako nmezikubali

Ukweli mtupu unayosema

Ova
 
Asante sana Ndugu yangu. Uwe na Ijumaa njema.

Lakini usiache kupinga Ujinga kwa Nguvu zote kila ukisikia au kuuona pahali popote.

Tukiwakalia kimya wajinga watadhani wako sahihi.
Agiza kinywaji aise ntakuja kukulipia

Ova
 
Huba ni filamu ya ma socialite na ma model kushow off, hakuna filamu pale. Filamu zipo kenya angalia magic east sisi ni wababaishajii
Wadangaji tu wote hao

Wauza papa tu na wanaume mariooo

Ova
 
"Ukifuatilia kinachoendelea kwenye tamthilia hiyo utagundua kinachoendelea ni umalaya, uhuni na tamaa mbaya. Na wala hakuna kitu kinachoitwa Huba kama jina la tamthilia lilivyo.

Umalaya, uchafu, na uasherati uliovuka mipaka ndicho kinachoendelea humo ambapo ni kinyume cha Huba. Kuchukuliana Mabwana, kuchukuliana Wake.
Mara Mama anatoka na Kijana wake wakiume.
Mara Baba "JB" anatoka na Mke wa Mkwe wake "Tima" yaani uchafu uchafu tuu. Filamu inanuka uchafu tuu. Hakuna huba hata sehemu moja"

Hapa umemaliza Mkuu.
HIVI MTU NA AKILI TIMAMU KWELI,UNAWEZA KUANGALIA HAYO
MATAMTHILIA

ova
 
Back
Top Bottom