Tamthilia ya Zahanati Kijijini

Hizi nyingine nyingi watu mda woote wapo na makeup.. Hadi muda wa kulala[emoji23][emoji23] adi unashangaa ni kwelii jamanii?

Ndo maana kuna mdau alisema kuwa japokuwa ni sanaa lakn wanaigiza kuigiza maisha[emoji23][emoji23]
Mimi nikiona mamakeup sijui magari makali
Ofisini muda wote
Kwa kweli huwa sifatilii.

Hatia na zahanati vimenirudisha kuangalia bongo movie.


Bi Ubwa
Unaona kabisa habebwi na kitu kingine chochote zaidi ya kipaji chake tu.
 
Ila anajua mnoo
 

Upo kama mim movie za vijijin,vita wanajeshi wengi sipendii
 

Kuna yule dada wa kwenye fungu langu anaitwa chelsea hajui kuigiza hata kidogoi
 
Kiukweli director wa hii series yupo vzr mnoo
 
Ila anajua mnoo
Yule mama kazi zake zote ni nzuri sana.

Hata ile iliyoisha ya hatia, alicheza kama mama Mboga.. alivaa character ya kipole.. unaangalia hadi unatokwa na machozi.


So far zahanati ya kijiji my best characters ni Huyu mama na Bi Ubwa, then wengine wanafatia.


Nilipenda alivyocheza muda ule kimbembe mfupa umemkaba[emoji23]
Huyu mama kipaji kipo kwenye damu[emoji119],, angekuwa na kielimu elimu kiasi angeweza kuandaa kazi zake mwenyewe.
Mungu amsaidie afikie hiyo hatua.
 
Bado Yule babu kibonge( MZEE MILANZI) na Yule bibi muuza duka la dawa
 
Mimi mwenyewe mchezo ya vijijini sipendagi
Na ilivyoanza nilikuwa naona mbaya sana Kwa kweli, haikunivutia.
Ila kadiri ilivyoendelea mbele ikachanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…