Wakuu, inaendelea.
Kwanza poleni kwa kuiachia njiani. Nilifanya hivyo kwa sababu kuu moja. Mwendelezo wake unahusisha gari niliyopanda hivyo wakati naandika uzi huu nilikuwa ndani nimepanda, na code ilikuwa rahisi kwa dereva na konda waliotupakia pamoja na abiria wengine maana tulipanda wawili tu. Hivyo ningegundulika (hasa kama kungekuwa na mtu anatumia JF muda ule).
Kumradhi sana!
Tuendelee sasa.
Tuliwaacha wale askari 3 na abiria wengine pale porini wakisubiria usafiri, nakumbuka nikiagana na mwanamke mwenye mtoto mdogo niliyekuwa namsaidia kumbeba mara kadhaa akipigwa baridi pale chini.
Gari nililopanda sasa lilikuwa linaitwa Johanvia (Musoma-Dar es Salaam). Silipigii chapuo, lakini moja ya magari mazuri unayoweza kupanda kwa safari za ukanda huo ni hili.
Dada mwenye maji ya kunde (Kondakta) alitukaribisha ndani, akauliza kama tungeweza kulipia Tsh. 10000/= kila mmoja tukamjibu haina neno. Akaruhusu tuingie, gari ikala mafuta.
Safari ilikuwa nzuri sana, tukafika Msamvu, Morogoro. Baadhi ya abiria wakashuka tukaendelea na safari.
Sokomoko la pili linaanza baada ya kuondoka msamvu. Kulikuwa na foleni ambayo kwa miaka ya karibuni kwenye safari zangu zijawahi kuiona. Ilikuwa inafika Chalinze. Magari yalikuwa yamejaa barabarani, hii ikiwa mida ya saa 7.
Tunafikaje sasa Dar es Salaam mapema tukiwa tumechoka sana, kumbuka gari hii inapaswa pia kubeba abiria mapema asubuhi kurudi Musoma.
Alitokea bodaboda mmoja akapiga honi mara kadhaa akimuomba dereva ashuke wazungumze, ndipo akasema atatusaidia kufika Dar es Salaam kwa kutupitisha kwenye mashamba ya katani (Sijui mkonge). Safari ikaanza tena tukipita kwenye mashamba hayo huku bodaboda akiongoza njia kwa pikipiki yake iliyowashwa taa.
Cha kushangaza, foleni ya magari ilikuwa hiishi, hadi sasa sijajua palikuwa na shida gani lakini baadhi ya watu walikuwa wanasema kuna ujenzi wa barabara maeneo hayo.
Tuliendelea kuchanja mbuga tukiwa kwenye shamba la katani (Mkonge) huku foleni ya magari yaliyokwama njia kuu tukiwa tunaiona kwa mbali.
Bila bodaboda huyu ambae baadae alituleta barabarani karibu na sheli moja (sikumbuki jina na sehemu) tungefika Dar es salaam saa 1 asubuhi. Pamoja na kwamba tulitumia njia isiyo sahihi na ilikuwa na risk kubwa ila namshukuru yeye binafsi na Mungu kwa kuwezesha tukaingia tena njia kuu mwendo kidogo karibu na maeneo ya Chalinze.
Baadae aliomba apatiwe Tsh. 10000/= kama sehemu ya wema aliotufanyia, dereva hakuwa na hiana akampatia. Tukaingia njia kuu, safari ikaanza ambapo tulikutana tena na foleni kubwa lakini haikudumu sana, tukaanza kuitafuta Dar es Salaam.
Basi, mambo yasiwe Mengi. Tumefika stand ya Magufuli saa 11 kasorobo alfajiri, nikaenda kwangu kupumzika.
Pamoja na changamoto zote hizi sijalaumu, kwani katika imani yangu ninaamini hii ni sehemu ya changamoto za kawaida za maisha ya binadamu. Nipo imara.
USHAURI NA MAPENDEKEZO
- Nilifanya kosa la kukata tiketi pasipo kuangalia ubora wa gari. Hata hii number plate nimeifahamu baada ya kupatwa na majanga. Ni muhimu kufuatilia kwanza details za gari kabla haujalipia nauli yako. Hapo nilibugi.
- Serikali ifuatilie magari haya, mengi yamechoka hayawezi kuhimili safari ndefu. Itasaidia kuepusha ajali zisizo za lazima
- Utaratibu wa wapiga debe uboreshwe kwenye vituo vya kukatia tiketi. Wengi sio waaminifu wanaongea uongo sana
- Serikali itafute namna ya kuzuia magari yasijaze abiria hadi mlangoni, hii ni hatari. Pia abiria tuwe makini, tukatae kupanda kwenye gari (ya umbali mrefu) ikiwa imejaa kiasi hiki.
- Kama nilivyosema, kuna mchezo wa kufaulisha watu waliozidi kwenye vituo vya polisi na mizani ili kukwepa faini. Serikali fuatilieni, mabasi yanafanya sana hii michezo.
- Matukio ya abiria kutelekezwa na wamiliki wa magari yanapopata changamoto yamekuwa mengi. Kwa nyakati fulani, abiria tuliotelekezwa pale jana usiku wengi walisema wamewahi kupatwa na majanga ya aina hii bila kupewa msaada wowote.
- Safari za basi la Dream Line (la jana) zisimamishwe kabla halijaleta madhara makubwa.
- Kifo kipo kila wakati. Kwa tunaoamini katika Mungu tusisahau kusali. Sali kabla haujasaliwa.
- Ukiwa safarini jitahidi uwe na akiba maana majanga hayatabiriki. Ninao uhakika baadhi ya wanawake wamefanyiwa mambo yasiyo mazuri baada ya kuharibika kwa gari lile polini wakiwa hawana chochote. Viashiria vya matendo haya vilianza kuonekana kabla sijaondoka, wengi walikuwa wanalia kuomba msaada wa kifedha huku baadhi ya vijana pembeni wakijadili namna ya kutumia hiyo fursa kujipatia utelezi.
NB: Tulipofika Kibaha kuna wanawake wawili walikuwa wanashuka lakini hawakuwa na tiketi zao. Walianza kudaiana na konda awape kwa sababu wasipofika nazo nyumbani waume zao hawataamini kuwa wametoka safari😂😂
“Unataka niachike, mume wangu hataamini. Unafikiri nyumbani nitasemaje, ushahidi wa safari uko wapi? Wengine sisi waume zetu ni wakali mno”
Mimi sio Muumini wa ile kampeni maarufu ya kukataa ndoa, ila naona vijana wana hoja. Anyway, walifanyiwa mpango wa kupewa tiketi zao, wakafurahi sana.
Kama upo humu unayedai tiketi, nakufahamisha kuwa una mke mzuri sana na alikuwa katulia kwenye basi peke yake. Punguza wasiwasi, alisafiri kweli.
View attachment 2728066