Tamu na chungu ya safari yangu ya Agosti 24, 2023 Kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

Tamu na chungu ya safari yangu ya Agosti 24, 2023 Kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

Shukuru kufika angalau saa 11 alfajiri kuna wengi walilala palepale mpaka asubuhi.
 
Mbeya-Tanga 2018/2019 nilipanda chuma inaitwa Mbeya City. Tulisafiri siku mbili[emoji23] gari imejaza magunia kwenye corridor. Gear inatafutwa mara mbilimbili[emoji1430] kuna makampuni ya mabasi yanafanya majaribio kwenye roho za watu
 
champion abiria wanapanda hadi na mbuzi, kuku na wanakaa nao kwenye siti, katikati ya safari mbuzi anakuhemea unazimia kwa harufu ya mdomo. Kuna mabasi sipandi bora nisisafiri ikiwepo hiyo champion.

Mabasi mengi uswahili mwingi nilipanda basi ya esther luxury ya mheshimiwa wa fedha from dom to dar linalotoka singida, utaratibu wao nao ni wahovyo wanaokota abiria barabarani na basi lishajaa hali iliyopelekea mizozano kati ya wahudumu na abiria. Bado makampuni mengi yana cha kujifunza kwa SHABIBY na KLM, wapo vizuri mno na wanakwenda na mda.
Siku niliyolipanda Champion, nilishukia Chalinze. Yaani basi halina breki🙄
 
Bora nipande coster hizi private jion kuliko kupanda basi lisilieleweka,mara ya mwisho nimesafiri na Costa kutoka khm to Dar ,nimetoka 10 jion nimefika dar sa 3 asubuhi
 
Niliwahi kupanda bus Moja la kuitwa champion from dar- dodoma aise yaani utazani mnasafirisha msiba wa shoga, gari lipo kimya halina mzik, tv wala huduma yoyote na vioo vya Gari vipo wazi havifungi,. Usiombee ukae dirishani unaweza kudhani unaendeshwa bodaboda.. ila sikulalamika coz haya magari ni bei rahis San ndio maana huduma mbovu na mara nyingi Huwa yanaondoka mchana kuzoa abiria walio sahaulika.
NB. Ukiona bus Lina mafundi zaidi ya watatu usipande achana nalo.
Kwamba basi kama😂😂😂
 
Mkuu unachoongea ni kweli kabisa kwakuwa Mimi ilinitokea kwa mwaka Jana hapohapo kahama. Nilikata tickets kwa jina la bus jingine asubuhi naambiwa Hilo bus limeharibika kwa hiyo nimefaulishwa nipande dreamline.... Aseee kahama uhuni Mwingi Sana.
 
safari ya kulitafuta jiji la Mkuu wa Mkoa mwenye Maneno mengi, mropokaji na mcheshi ilianza.
Huyu sio mwingine bali ni Challamila sio Rehema Challamila Ray C ila ni Challamila hivyo hivyo yule mkuu wa Mkoa anaepambana na wadangaji jijini Dasalama
 
Hiyo Kampuni ya Dream line ni ya kipumbavu mno!

Ulicho eleza nami kilinikuta siku moja na hilo Bus la Dream liner!

Nikiwa nimefika hapo KAHAMA nikitokea Masumbwe nikakosa tiketi ya Frester na Satco akaja Kijana mmoja akamishawishi Kukata Bus la Dream Liner kwenda Dar!

Kesho yake asbh nilijuta nilipofika Bus Stand!
Bus lilipaswa kuondoka saa 12 asbh lakini tuliondoka karibia saa 3!

Traffic Police kumbe walishalijua Hilo Bus, ilipofika muda wa kuondoka Traffic Police akaja kwa ajili ya ukaguzi akasema matairi ya Hilo gari ni mabovu na gari ipelekwe kituo cha police!

Kwakweli siku hiyo tulisota na wafanyakazi wa Hilo gari hawajali, Kauli zao mbovu na gari ni chafu kupindukia!

Kwa ufupi Dream Liner siyo Kampuni ya Usafirishaji ya maana hata kidogo!
 
champion alichelewa kufanya transfomation ni kama nokia, wakati serikali inahamia dodoma alipaswa aboreshe huduma zake na kutafuta mabasi yenye hali nzuri angepiga hela sana tatizo lake anapenda magonga nyundo, basi zimechoka zimechakaa. Machame inv alishtuka na mafanikio yanaonekana.
Wana ki-gereji chao bubu maeneo ya area c mbele ya town campus ya chuo cha hombolo, fika pale ujionee yanavyopigwa nyundo na mafundi mchundo, halafu cha ajabu wale mabwana kuanzia madereva, wahudumu wa mabasi,wakata tiketi mpaka hawa mafundi wote ni kabila moja WARANGI ukifika pale ni mwendo wa kutafuna mirungi na kuongea kilugha chao
 
Wana ki-gereji chao bubu maeneo ya area c mbele ya town campus ya chuo cha hombolo, fika pale ujionee yanavyopigwa nyundo na mafundi mchundo, halafu cha ajabu wale mabwana kuanzia madereva, wahudumu wa mabasi,wakata tiketi mpaka hawa mafundi wote ni kabila moja WARANGI ukifika pale ni mwendo wa kutafuna mirungi na kuongea kilugha chao
Na huo ukabila pia umechangia pakubwa kuwa hivyo walivyo.
 
Huko kahama kuna majina mazuri ya magari ila mgari yenyewe yamechoka hadi hayastahili kuitwa majina hayo
 
Back
Top Bottom