Tamu na chungu ya safari yangu ya Agosti 24, 2023 Kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

Tamu na chungu ya safari yangu ya Agosti 24, 2023 Kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

Story yangu inafanana na ya huyu Mleta Mada lakini matokeo tofauti. Ilikuwa mwaka 2006 nimeingia Mwanza toka Dar kwa ndege ili nirudi nayo siku hiyo hiyo. Ndege ya ofisi hiyo, mara paap simu imepigwa ndege ikapewa safari kwenda kwanza Entebe.

Mambo yakavurugika. Nikasema ngoja nichuke basi nigeuze zangu maana wanaenda kuchukuliwa Entebe tayari ndege itakuwa imejaa.

Enzi hizo mabasi yanayowika ni Mohamed Trans na Mombasa Raha. Ila barabara ni vumbi kuanzia Misungwi mpaka Dodoma. Nilipofika stand za Mohamed full kiyoyozi kama stand za Scandnavia, nikakuta tiketi zimejaa. Kuelekea Mombasa Raha nako kumejaa. Nikaona siwezi kuahirisha safari lazima nirudi Dar kesho yake nimeshachelewa.

Sasa hapo ndipo nilipofanya kosa kama la Mleta Mada, maana nikaenda Stand na kuuliza basi lenye nafasi, nikambiwa kata tiketi ya Najma. Basi silijui na hata hapo stendi halikuwepo. Mimi nikaamua kukata hivyohivyo.

Kesho yake asubuhi, nimewahi stendi enzi hizo ipo pale Nata. Kila nikitafuta basi silioni. Kumbe kichwani mwangu taswira ya basi kama Mohamed Trans na Mombasa Raha ilikuwa haijatoka. Hivyo sisomi majina na mabasi ambayo nayaona ni ngarangara.

Baada ya kuzunguka sana, nikmpigia aliyeniuzia tiketi naye akaja kunionesha basi ambalo nilikuwa nalipita nikijua linaenda vijiji vya jirani. Tukabishana sana kuhusu basi lile kama litafika Dar, Kwa kujiamini sana yule jamaa akaniambia hili gari sio kufika tu, bali linafika la kwanza kabla ya Mohamed Trans na Mombasa Raha.

Kwa unyonge nikaingia kwenye ngarangara, huwezi amini ndani halina hata taa, halafu viti vyake vina lile bomba kwa juu bila kushonewa cushion. Sasa kilichonitia moyo ni engine inaunguruma vizuri. Kilichonifurahisha safari ilipoanza, ile lami toka Mwanza mpaka Misungwi ilikuwa ni full tracking force, nikasema hapa basi lipo.

To cut the story short, Dar tuliingia saa mbili asubuhi wakati basi zingine ziliingia saa nne asubuhi. IT WAS A BLESSING IN DISGUISE.
 
Wakuu, inaendelea.

Kwanza poleni kwa kuiachia njiani. Nilifanya hivyo kwa sababu kuu moja. Mwendelezo wake unahusisha gari niliyopanda hivyo wakati naandika uzi huu nilikuwa ndani nimepanda, na code ilikuwa rahisi kwa dereva na konda waliotupakia pamoja na abiria wengine maana tulipanda wawili tu. Hivyo ningegundulika (hasa kama kungekuwa na mtu anatumia JF muda ule).

Kumradhi sana!

Tuendelee sasa.

Tuliwaacha wale askari 3 na abiria wengine pale porini wakisubiria usafiri, nakumbuka nikiagana na mwanamke mwenye mtoto mdogo niliyekuwa namsaidia kumbeba mara kadhaa akipigwa baridi pale chini.

Gari nililopanda sasa lilikuwa linaitwa Johanvia (Musoma-Dar es Salaam). Silipigii chapuo, lakini moja ya magari mazuri unayoweza kupanda kwa safari za ukanda huo ni hili.

Dada mwenye maji ya kunde (Kondakta) alitukaribisha ndani, akauliza kama tungeweza kulipia Tsh. 10000/= kila mmoja tukamjibu haina neno. Akaruhusu tuingie, gari ikala mafuta.

Safari ilikuwa nzuri sana, tukafika Msamvu, Morogoro. Baadhi ya abiria wakashuka tukaendelea na safari.

Sokomoko la pili linaanza baada ya kuondoka msamvu. Kulikuwa na foleni ambayo kwa miaka ya karibuni kwenye safari zangu zijawahi kuiona. Ilikuwa inafika Chalinze. Magari yalikuwa yamejaa barabarani, hii ikiwa mida ya saa 7.

Tunafikaje sasa Dar es Salaam mapema tukiwa tumechoka sana, kumbuka gari hii inapaswa pia kubeba abiria mapema asubuhi kurudi Musoma.

Alitokea bodaboda mmoja akapiga honi mara kadhaa akimuomba dereva ashuke wazungumze, ndipo akasema atatusaidia kufika Dar es Salaam kwa kutupitisha kwenye mashamba ya katani (Sijui mkonge). Safari ikaanza tena tukipita kwenye mashamba hayo huku bodaboda akiongoza njia kwa pikipiki yake iliyowashwa taa.

Cha kushangaza, foleni ya magari ilikuwa hiishi, hadi sasa sijajua palikuwa na shida gani lakini baadhi ya watu walikuwa wanasema kuna ujenzi wa barabara maeneo hayo.

Tuliendelea kuchanja mbuga tukiwa kwenye shamba la katani (Mkonge) huku foleni ya magari yaliyokwama njia kuu tukiwa tunaiona kwa mbali.

Bila bodaboda huyu ambae baadae alituleta barabarani karibu na sheli moja (sikumbuki jina na sehemu) tungefika Dar es salaam saa 1 asubuhi. Pamoja na kwamba tulitumia njia isiyo sahihi na ilikuwa na risk kubwa ila namshukuru yeye binafsi na Mungu kwa kuwezesha tukaingia tena njia kuu mwendo kidogo karibu na maeneo ya Chalinze.

Baadae aliomba apatiwe Tsh. 10000/= kama sehemu ya wema aliotufanyia, dereva hakuwa na hiana akampatia. Tukaingia njia kuu, safari ikaanza ambapo tulikutana tena na foleni kubwa lakini haikudumu sana, tukaanza kuitafuta Dar es Salaam.

Basi, mambo yasiwe Mengi. Tumefika stand ya Magufuli saa 11 kasorobo alfajiri, nikaenda kwangu kupumzika.

Pamoja na changamoto zote hizi sijalaumu, kwani katika imani yangu ninaamini hii ni sehemu ya changamoto za kawaida za maisha ya binadamu. Nipo imara.

USHAURI NA MAPENDEKEZO
  1. Nilifanya kosa la kukata tiketi pasipo kuangalia ubora wa gari. Hata hii number plate nimeifahamu baada ya kupatwa na majanga. Ni muhimu kufuatilia kwanza details za gari kabla haujalipia nauli yako. Hapo nilibugi.
  2. Serikali ifuatilie magari haya, mengi yamechoka hayawezi kuhimili safari ndefu. Itasaidia kuepusha ajali zisizo za lazima
  3. Utaratibu wa wapiga debe uboreshwe kwenye vituo vya kukatia tiketi. Wengi sio waaminifu wanaongea uongo sana
  4. Serikali itafute namna ya kuzuia magari yasijaze abiria hadi mlangoni, hii ni hatari. Pia abiria tuwe makini, tukatae kupanda kwenye gari (ya umbali mrefu) ikiwa imejaa kiasi hiki.
  5. Kama nilivyosema, kuna mchezo wa kufaulisha watu waliozidi kwenye vituo vya polisi na mizani ili kukwepa faini. Serikali fuatilieni, mabasi yanafanya sana hii michezo.
  6. Matukio ya abiria kutelekezwa na wamiliki wa magari yanapopata changamoto yamekuwa mengi. Kwa nyakati fulani, abiria tuliotelekezwa pale jana usiku wengi walisema wamewahi kupatwa na majanga ya aina hii bila kupewa msaada wowote.
  7. Safari za basi la Dream Line (la jana) zisimamishwe kabla halijaleta madhara makubwa.
  8. Kifo kipo kila wakati. Kwa tunaoamini katika Mungu tusisahau kusali. Sali kabla haujasaliwa.
  9. Ukiwa safarini jitahidi uwe na akiba maana majanga hayatabiriki. Ninao uhakika baadhi ya wanawake wamefanyiwa mambo yasiyo mazuri baada ya kuharibika kwa gari lile polini wakiwa hawana chochote. Viashiria vya matendo haya vilianza kuonekana kabla sijaondoka, wengi walikuwa wanalia kuomba msaada wa kifedha huku baadhi ya vijana pembeni wakijadili namna ya kutumia hiyo fursa kujipatia utelezi.
NB: Tulipofika Kibaha kuna wanawake wawili walikuwa wanashuka lakini hawakuwa na tiketi zao. Walianza kudaiana na konda awape kwa sababu wasipofika nazo nyumbani waume zao hawataamini kuwa wametoka safari[emoji23][emoji23]

“Unataka niachike, mume wangu hataamini. Unafikiri nyumbani nitasemaje, ushahidi wa safari uko wapi? Wengine sisi waume zetu ni wakali mno”

Mimi sio Muumini wa ile kampeni maarufu ya kukataa ndoa, ila naona vijana wana hoja. Anyway, walifanyiwa mpango wa kupewa tiketi zao, wakafurahi sana.

Kama upo humu unayedai tiketi, nakufahamisha kuwa una mke mzuri sana na alikuwa katulia kwenye basi peke yake. Punguza wasiwasi, alisafiri kweli.
View attachment 2728066
Utopolo mtupu
 
Story yangu inafanana na ya huyu Mleta Mada lakini matokeo tofauti. Ilikuwa mwaka 2006 nimeingia Mwanza toka Dar kwa ndege ili nirudi nayo siku hiyo hiyo. Ndege ya ofisi hiyo, mara paap simu imepigwa ndege ikapewa safari kwenda kwanza Entebe. Mambo yakavurugika. Nikasema ngoja nichuke basi nigeuze zangu maana wanaenda kuchukuliwa Entebe tayari ndege itakuwa imejaa.
Enzi hizo mabasi yanayowika ni Mohamed Trans na Mombasa Raha. Ila barabara ni vumbi kuanzia Misungwi mpaka Dodoma. Nilipofika stand za Mohamed full kiyoyozi kama stand za Scandnavia, nikakuta tiketi zimejaa. Kuelekea Mombasa Raha nako kumejaa. Nikaona siwezi kuahirisha safari lazima nirudi Dar kesho yake nimeshachelewa.
Sasa hapo ndipo nilipofanya kosa kama la Mleta Mada, maana nikaenda Stand na kuuliza basi lenye nafasi, nikambiwa kata tiketi ya Najma. Basi silijui na hata hapo stendi halikuwepo. Mimi nikaamua kukata hivyohivyo.
Kesho yake asubuhi, nimewahi stendi enzi hizo ipo pale Nata. Kila nikitafuta basi silioni. Kumbe kichwani mwangu taswira ya basi kama Mohamed Trans na Mombasa Raha ilikuwa haijatoka. Hivyo sisomi majina na mabasi ambayo nayaona ni ngarangara.
Baada ya kuzunguka sana, nikmpigia aliyeniuzia tiketi naye akaja kunionesha basi ambalo nilikuwa nalipita nikijua linaenda vijiji vya jirani. Tukabishana sana kuhusu basi lile kama litafika Dar, Kwa kujiamini sana yule jamaa akaniambia hili gari sio kufika tu, bali linafika la kwanza kabla ya Mohamed Trans na Mombasa Raha.
Kwa unyonge nikaingia kwenye ngarangara, huwezi amini ndani halina hata taa, halafu viti vyake vina lile bomba kwa juu bila kushonewa cushion. Sasa kilichonitia moyo ni engine inaunguruma vizuri. Kilichonifurahisha safari ilipoanza, ile lami toka Mwanza mpaka Misungwi ilikuwa ni full tracking force, nikasema hapa basi lipo.
To cut the story short, Dar tuliingia saa mbili asubuhi wakati basi zingine ziliingia saa nne asubuhi. IT WAS A BLESSING IN DISGUISE.
Kuna baadhi ya matajiri walikua miamba wa kusuka injini.
Ukilitazama basi limechoka hatari ila mwendo wake sasa usipime. Miaka ya 2012 ilikuepo ngoma inaitwa coast line aisee ile gari ilikua inatembea
 
Halafu utaskia kuna watu hobbies zao ni kusafiri. Mie nasafiri kwa mambo maalum, sina budi ndio nisafiri
 
Wakuu, inaendelea.

Kwanza poleni kwa kuiachia njiani. Nilifanya hivyo kwa sababu kuu moja. Mwendelezo wake unahusisha gari niliyopanda hivyo wakati naandika uzi huu nilikuwa ndani nimepanda, na code ilikuwa rahisi kwa dereva na konda waliotupakia pamoja na abiria wengine maana tulipanda wawili tu. Hivyo ningegundulika (hasa kama kungekuwa na mtu anatumia JF muda ule).

Kumradhi sana!

Tuendelee sasa.

Tuliwaacha wale askari 3 na abiria wengine pale porini wakisubiria usafiri, nakumbuka nikiagana na mwanamke mwenye mtoto mdogo niliyekuwa namsaidia kumbeba mara kadhaa akipigwa baridi pale chini.

Gari nililopanda sasa lilikuwa linaitwa Johanvia (Musoma-Dar es Salaam). Silipigii chapuo, lakini moja ya magari mazuri unayoweza kupanda kwa safari za ukanda huo ni hili.

Dada mwenye maji ya kunde (Kondakta) alitukaribisha ndani, akauliza kama tungeweza kulipia Tsh. 10000/= kila mmoja tukamjibu haina neno. Akaruhusu tuingie, gari ikala mafuta.

Safari ilikuwa nzuri sana, tukafika Msamvu, Morogoro. Baadhi ya abiria wakashuka tukaendelea na safari.

Sokomoko la pili linaanza baada ya kuondoka msamvu. Kulikuwa na foleni ambayo kwa miaka ya karibuni kwenye safari zangu zijawahi kuiona. Ilikuwa inafika Chalinze. Magari yalikuwa yamejaa barabarani, hii ikiwa mida ya saa 7.

Tunafikaje sasa Dar es Salaam mapema tukiwa tumechoka sana, kumbuka gari hii inapaswa pia kubeba abiria mapema asubuhi kurudi Musoma.

Alitokea bodaboda mmoja akapiga honi mara kadhaa akimuomba dereva ashuke wazungumze, ndipo akasema atatusaidia kufika Dar es Salaam kwa kutupitisha kwenye mashamba ya katani (Sijui mkonge). Safari ikaanza tena tukipita kwenye mashamba hayo huku bodaboda akiongoza njia kwa pikipiki yake iliyowashwa taa.

Cha kushangaza, foleni ya magari ilikuwa hiishi, hadi sasa sijajua palikuwa na shida gani lakini baadhi ya watu walikuwa wanasema kuna ujenzi wa barabara maeneo hayo.

Tuliendelea kuchanja mbuga tukiwa kwenye shamba la katani (Mkonge) huku foleni ya magari yaliyokwama njia kuu tukiwa tunaiona kwa mbali.

Bila bodaboda huyu ambae baadae alituleta barabarani karibu na sheli moja (sikumbuki jina na sehemu) tungefika Dar es salaam saa 1 asubuhi. Pamoja na kwamba tulitumia njia isiyo sahihi na ilikuwa na risk kubwa ila namshukuru yeye binafsi na Mungu kwa kuwezesha tukaingia tena njia kuu mwendo kidogo karibu na maeneo ya Chalinze.

Baadae aliomba apatiwe Tsh. 10000/= kama sehemu ya wema aliotufanyia, dereva hakuwa na hiana akampatia. Tukaingia njia kuu, safari ikaanza ambapo tulikutana tena na foleni kubwa lakini haikudumu sana, tukaanza kuitafuta Dar es Salaam.

Basi, mambo yasiwe Mengi. Tumefika stand ya Magufuli saa 11 kasorobo alfajiri, nikaenda kwangu kupumzika.

Pamoja na changamoto zote hizi sijalaumu, kwani katika imani yangu ninaamini hii ni sehemu ya changamoto za kawaida za maisha ya binadamu. Nipo imara.

USHAURI NA MAPENDEKEZO
  1. Nilifanya kosa la kukata tiketi pasipo kuangalia ubora wa gari. Hata hii number plate nimeifahamu baada ya kupatwa na majanga. Ni muhimu kufuatilia kwanza details za gari kabla haujalipia nauli yako. Hapo nilibugi.
  2. Serikali ifuatilie magari haya, mengi yamechoka hayawezi kuhimili safari ndefu. Itasaidia kuepusha ajali zisizo za lazima
  3. Utaratibu wa wapiga debe uboreshwe kwenye vituo vya kukatia tiketi. Wengi sio waaminifu wanaongea uongo sana
  4. Serikali itafute namna ya kuzuia magari yasijaze abiria hadi mlangoni, hii ni hatari. Pia abiria tuwe makini, tukatae kupanda kwenye gari (ya umbali mrefu) ikiwa imejaa kiasi hiki.
  5. Kama nilivyosema, kuna mchezo wa kufaulisha watu waliozidi kwenye vituo vya polisi na mizani ili kukwepa faini. Serikali fuatilieni, mabasi yanafanya sana hii michezo.
  6. Matukio ya abiria kutelekezwa na wamiliki wa magari yanapopata changamoto yamekuwa mengi. Kwa nyakati fulani, abiria tuliotelekezwa pale jana usiku wengi walisema wamewahi kupatwa na majanga ya aina hii bila kupewa msaada wowote.
  7. Safari za basi la Dream Line (la jana) zisimamishwe kabla halijaleta madhara makubwa.
  8. Kifo kipo kila wakati. Kwa tunaoamini katika Mungu tusisahau kusali. Sali kabla haujasaliwa.
  9. Ukiwa safarini jitahidi uwe na akiba maana majanga hayatabiriki. Ninao uhakika baadhi ya wanawake wamefanyiwa mambo yasiyo mazuri baada ya kuharibika kwa gari lile polini wakiwa hawana chochote. Viashiria vya matendo haya vilianza kuonekana kabla sijaondoka, wengi walikuwa wanalia kuomba msaada wa kifedha huku baadhi ya vijana pembeni wakijadili namna ya kutumia hiyo fursa kujipatia utelezi.
NB: Tulipofika Kibaha kuna wanawake wawili walikuwa wanashuka lakini hawakuwa na tiketi zao. Walianza kudaiana na konda awape kwa sababu wasipofika nazo nyumbani waume zao hawataamini kuwa wametoka safari😂😂

“Unataka niachike, mume wangu hataamini. Unafikiri nyumbani nitasemaje, ushahidi wa safari uko wapi? Wengine sisi waume zetu ni wakali mno”

Mimi sio Muumini wa ile kampeni maarufu ya kukataa ndoa, ila naona vijana wana hoja. Anyway, walifanyiwa mpango wa kupewa tiketi zao, wakafurahi sana.

Kama upo humu unayedai tiketi, nakufahamisha kuwa una mke mzuri sana na alikuwa katulia kwenye basi peke yake. Punguza wasiwasi, alisafiri kweli.
View attachment 2728066

Huku ndo huwa kunatokea yale mambo ya masihara
 
Nililopanda mimi linaitwa Dream Line kwenye ticket waliandika tunafika dar 21:00 usiku lakini dah picha linaanza nafika stendi picha ya basi kwenye ticket na basi lenyewe nililokutana nalo vitu viwili tofauti yani wanavyopakia huko barabarani hamna tofauti na daladala za mabibo-K/koo
Shida kupakia au kufika 21:00?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Ayu 14:1

Ndio utangulizi ninaoona unafaa kwa uzi huu, ninaoanza kuuandika mida hii saa 7:25 usiku nikiwa eneo ambalo kwa maelezo ya vibao vya barabarani vonasoma Mdaula (Msolwa), Morogoro.

Safari yangu imeanza baada ya kukamilisha mazishi ya mtu wangu wa karibu sana niliyempenda, huko Kahama, Shinyanga, ndio maana ya mstari wa biblia nilioamua kuchagua kuutumia mwanzoni mwa uzi huu. Pumzika kwa amani.

Agosti 23, 2023 nikiwa kahama, niliamua kukata tiketi kwenye basi la Dream Line T 140 AZZ, Kahama-Dar es Salaam. Mnamo Agosti 24, 2023, saa 12:00 asubuhi, safari ya kulitafuta jiji la Mkuu wa Mkoa mwenye Maneno mengi, mropokaji na mcheshi ilianza.

Nikiri kwamba sikuwa nalitambua basi hili vizuri pamoja na kuwa miongoni mwa mtu/abiria wa mwanzoni kukata tiketi ya basi hili kwa safari ya siku husika. Hili ni kosa kubwa la kwanza la kiufundi nililofanya.

Baada ya kukaa kwenye gari, nilishangaa kuona likiwa limechoka sana, viti vimezeeka na muonekano wa ndani ukiwa duni.

Naikumbuka sauti ya abiria mmoja asubuhi hii akimuuliza konda, “Basi hili linafika Dar es Salaam?” Na konda akijibu “Ndio, linaenda Dar es salaam”. Bwana huyu anaanza kugombana na konda akisisitiza “Nauliza kama linafika Dar es Salaam, sio kama linaenda Dar es salaam maana kwa jinsi lilivyochoka naona kabisa halifiki. Nirudishie nauli yangu”

Anyway, tuachane nao. Walizozana kidogo hatimaye jamaa alighairi kupanda. Sijui alipata usafiri gani mwingine.

Safari ya kuondoka stand ya kahama ikaanza. Ajabu ya pili baada ya kufika eneo linaloitwa Kagongwa, abiria aliyepaswa kupandia hapo alikuta limeshapita kama dakika 10 hivi. Alipiga simu kwa konda akilalamika kwanini hakusimama ili apande, ndipo akaambiwa haiwezekani tena, atafute usafiri mwingine.

Utashangaa, kwa mwendo wa basi lile uliokuwa kama wa maharusi, abiria aliyeachwa na gari kwa dakika 10 alitutangulia kufika eneo la mbele linaoitwa Isaka akiwa na boda, akapandia hapo. Nilipoona jambo hili limetokea nikasema tayari kichwa changu kimeshawekewa maji, nijiandae kunyolewa. Nilimkumbuka pia Mandonga kuwa tayari nilikuwa nimedandia mtumbwi wa vimbwengo.

Safari iliendelea, mende wakiwa wanaonekana kwenye gari, hakuna system za kuchaji, hakuna huduma rafiki, gari likisimama kila kituo kama daladala.

Nikiri kwamba, baada ya kukaribia Singida, harufu kali ilianza kusikika upande wa kulia wa nyuma ya basi hili. Mzozano ulianza huku watu waliokaa upande huo wakituhumiana kuchafua hali ya hewa (Kujamba). Harufu hii iliendelea kwa muda, ikija na kuondoka.

Tulifika Singida mida ya saa 9 mchana, tukaanza kuitafuta Dodoma. Basi hili lilikuwa linakera sana, kwa baadhi ya vituo, mathalani Gairo lilisimama kwa zaidi ya dakika 45 likisubiria abiria. Pamoja na kwamba ni gari ya masafa marefu, abiria walikuwa wamejaa kiasi cha wengine kukaa kwenye mstari wa katikati usio na viti. Nakumbuka kuona abiria hawa wakipandishwa daladala na bodaboda kwenye baadhi ya vituo vya polisi na mizani ili watusibirie kwa mbele wakikwepa kugundulika. Kifupi, lilijaza hadi mlangoni.

Sekeseke lingine lilikuja baada ya kuanza kuingia Dodoma kwenye mojawapo ya Madaraja ya SGR (Nikiri kutokujua jina halisi la sehemu hii) ambapo basi hili likiwa juu ya daraja hilo lenye barabara ya vumbi lilinusurika kuporomoka baada ya kutaka kulazimisha ku overtake huku lori likiwa kwa mbele.

Mtakatifu Padre Pio anatuambia tusali na tuondoe hofu siku zote. Ndicho nilichokuwa nafanya kwenye safari hii yenye mikikimikiki mingi isiyo ya kawaida.

Dodoma kwenda Dar es Salaam haikuwa rahisi pia. Tukiwa tumevuka Gairo, tupo porini (eneo ambalo silijui kwa jina), harufu iliyokuwa inasikika mchana iliibuka tena kwa mara nyingine. Hapa ilidumu kwa muda mrefu. Nikiwa na uchovu mkubwa na usingizi, nilisikia mlio mkubwa kama wa bomu, Paaaaah.

Basi lilianza kuyumba, nilimuona dereva akihamaki na kuanza kunyonga usukani kuelekea mtaroni. Baadae ilikuja kufahamika kuwa harufu ile ilikuwa ni tairi za gari ile zilizokuwa zinaungua taratibu bila sisi kufahamu.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na ubovu wa basi hili, nikiri dereva wao ambae baadae nilikuja kumtambua kwa jina la Dullah (kama sijakosea) kuwa ni mtu makini, pamoja na Mungu, utulivu wake pia ulisaidia kunusuru vifo vya makumi ya watu tuliokuwa kwenye basi hili.

Watu walikuwa wameshaanza kuruka madirishani, kelele za kuomba Mungu na kukemea mapepo zilitoka. Nilianza kulikumbuka kaburi lililommeza mpendwa wangu siku chache nyuma ambaye ndie nilikuwa natoka kumzika kuwa lilikuwa linakwenda pia kunimeza.

Nikakumbuka siku ya Ijumaa kuu wakati nikiwa Seminarini wakati wa Kuimba injili, wakati Yesu anaisalimu roho yake. Nikamuomba Mungu aikumbuke ibada yangu kwake na jinsi nilivyomtumainia kwenye maisha yangu, nikamkabidi roho yangu ili mapenzi yake yatimizwe.

Baada ya muda kidogo nikiwa bado kwenye siti yangu (huku watu wakikanyagana mlangoni) nilianza kuona gari likiyumba kushoto na kulia likiingia mtaroni, hapo ndipo kelele za watu ziliongezeka. Hatimae dereva alifanikiwa kulisimamisha mtaroni, hakuna aliyeamini kama alifanikiwa kutoka salama.

Walau kwa ufahamu wangu sijawahi kupatwa na jaribu kubwa kiasi hiki lililoiweka rehani roho yangu na kunifanya niamini pasipo shaka kuwa kifo ni kitu kinachoweza kutokea muda wowote, popote. Tukio hili lilitokea mida ya 1 usiku.

Jambo la kushangaza, wahudumu wa basi hili walitokomea kusikojulikana, wakamuachia gari muuza juisi na biskuti. Baada ya kufuatilia, mchuuzi huyo alituambia walikuwa wamefuata spea za gari Dumila, na kwamba masikio ya breki ya nyuma ndio yalikuwa yameharibika na mataili ya nyuma yakiwa yamepasuka.

Saa 2 hawajarudi, saa 3 hawajarudi, saa 4 hawajarudi. Abiria tulibaki kama Yatima. Kila tukiuliza wanasema wapo Dumila wanashughulikia, jambo ambalo baadae iligundulika kuwa sio kweli, bali walikuwa wanaendelea na mambo yao binafsi kusikojulikana.

Mungu ni mwema, mida ya saa 4:30 walifika Askari wakiwa kwenye doria ambao lazima niseme wazi walitupa faraja sana kutokana na eneo tulilokuwepo. Walijaribu kumpigia simu dereva kwa namba inayoishia 60 (kama sijasahau) bila mafanikio. Ilikuwa haipatikani japokuwa mwanzoni ilikuwa inaita.

Mabasi, boda na daladala zilizokuwa zinapita zilikuwa hazitaki kusimama kutokana na nature ya eneo husika ambalo baada ya muda mfupi baadhi ya wapita njia walikuja kubainisha kuwa ni eneo baya ambalo siku chache nyuma lilikuwa limekunywa damu ya wanakijiji watatu.

Tunafanyaje sasa?

Mwandishi wa zaidi ya vitabu 160, msomi mwenye Doctorate 8, mzungumzaji wa lugha 10 na mtu anayefamika kama Mwanateolojia mkubwa zaidi wa Karne ya 20, Papa Benedicto XVI aliwahi kusema “We are not the product of blind chance or absurdity; instead our life originates as part of a loving plan of God.”. Maisha yetu ni fumbo, tunaishi kwa kadri ya matakwa na mapenzi ya Mungu.

Baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu, hatimae nuru ilionekana baada ya kusimama kwa basi moja ambalo mimi na jamaa mwingine mmoja tuliamua kupanda ili kuendelea na safari yetu.

Hapa ndio chimbuko la mkasa wa pili uliochangia kwa kiasi kikubwa mimi kuandika uzi huu unaanza.

Inaendelea….

Sehemu ya 2 (Mwisho)
Uktuma sehem ya 2 ,nitaarifu
 
Agosti 23, 2023 nikiwa kahama, niliamua kukata tiketi kwenye basi la Dream Line T 140 AZZ, Kahama-Dar

Hii chuma kama sikosei huwa inapak magomeni Idrisa inaweza kaa hata miezi mi3 ipo ipo tu imepaki, kila kitu ktk bus hilo ni cha kuunga unga. Ni bora ukatoka na bajaj kahama to dar kuliko hiyo Screpa! Kwanza inakopaki tu wanauza chuma chakavu na haya makopo wanayookota mtaani!
 
Unazingua mkuu, kwamba bora bajaji😂😂😂
 
Kuna basi inaitwa osaka na mj safaris zinatoka dar kwenda musoma bwana bwana hz zimechoka hiyo mj tulitoka dar saa 1 tukafika musoma saa 5 ya kesho yake. Gari ilipasuka tairi mara mbili pale simiyu ni usku wa manane na gari inatoa harufu ya dawa za kuulia mende kunguni na viroboto. Inshort haifai kwa safari ndefu kama zile maana haina ubora kabsa
 
Very interesting story..! Nimeburudika kuisoma..btw pole mkuu kwa changamoto ulizokutana nazo.
 
Buss namba T sijui nini AZZ nawewe ukakata ticket kabisa. Hilo lilipaswa liwe limesha yeyushwa Chuma chakavu
Hili gari nimeshapanda mara mbili Kahama-Dom mbona linamwaga moto fresh tu
 
Back
Top Bottom