Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kwa wanasayansi, wanasema" don't re-invent the wheel".
Ndicho tunachoona kwa baadhi ya miradi ya serikali kwa sasa inayojengwa kwa FORCE ACCOUNT.
Serikali mkoani Tanga inalia na watendaji wake.
Waliagizwa huko Muheza kujenga shule ya sekondari, darasa moja kwa milioni 20, wao kwa ubishi na weledi wao kiutendaji wakaongeza (inasemekana ) 12 za kwao kwa kila darasa na darasa moja kuwa milioni 32!
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ndg Mgumba.
Kwa staili ya Force Account tunashindwa kuelewa msingi wa kila darasa kuwa milioni 20, sijui kama kuna BOQ hapo(hesabu za gharama halisi).
Na mkaguzi wa kazi, mpitisha malipo ya fundi Maiko sijui ni akina nani hapo?
Lakini watendaji wanne wameisha sajiliwa na TAKUKURU kwa uchunguzi.
Force Account inawamaliza watendaji serikalini re-inventing the wheel!