TANAPA: Kwanini hakuna "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kama ambavyo kuna Mobile Courts?

nenda shinyanga mkuu utashuhudia huwa haipiti muda mrefu fisi zinaonekana na mwenye nayo anajitokeza, ma fisi mengi ni maoga sana yanakutafuna kama ukikimbia tu
Duh ya kweli hayo? Mbona naskia habari za watu kuliwa na fisi? hivi hawa hawa wa kwenye zoo ndio hawa hawa wa mbungani na wakufugwa kwa ukubwa/kimo?
Anafugwa kama mbwa?
 
nenda shinyanga mkuu utashuhudia huwa haipiti muda mrefu fisi zinaonekana na mwenye nayo anajitokeza, ma fisi mengi ni maoga sana yanakutafuna kama ukikimbia tu
Wasukuma watakuja kukushambulia mkuu hahahahaaaaa
 
Ni jambo mbalo haliwezekani na tukirudi kwenye haki za wanyama ndio Haiwezekani kabisa

unajiskiaje wewe ukichukuliwa uwekwe kwenye ndege ukatembezwe huko kwa kina amsterdam

wakuone wakujue kisha unarudishwa? umekaa kwako unaangalia TV team ya kina sirro inakuja inakubeba

inakupeleka kwenye ndege tayari kupelekwa India kuonyeshwa onyeshwa kwa wahindi,huku nyuma haiachi hata

senti 5 ya familia yako,haiachi hata senti kwa ajili ya ulinzi,nk unaionaje hiyo,imekaaje? basi ndio ufahamu wanyama nao

ni kama tulivyo wanadamu,wanapaswa kuheshimiwa sio kwasababu hawaongei ndio wabebwe bebwe tu,wazo zuri lkn HALIWEZEKANI.
 
Ni jambo mbalo haliwezekani na tukirudi kwenye haki za wanyama ndio Haiwezekani kabisa
Mkuu, mbona sasa huwa tuna wachinja kisha tunapika nyama zao na tunakula kama issue ni suala la haki?...
 
Tunachinja na kuwala lakini tunafanya kwa viumbe vilivyozeeka au dhoofu au kuumwa na wala si vyenye umri mdogo mkuu lakini tukirudi kwenye swala lako halitohitaji aina ya viumbe tunaowachinja na kuwala litahitaji wale wazima na wenye afya imara.
 
Hao hao wazima na wenye afya imara ndio ambao tunatakiwa kuwaweka katika hizo "Mobile Zoos"
 
Back
Top Bottom