TANAPA yatangaza kifo cha Faru Rajabu (mtoto wa Faru John) katika Hifadhi ya Serengeti

TANAPA yatangaza kifo cha Faru Rajabu (mtoto wa Faru John) katika Hifadhi ya Serengeti

Kuna muda Dunia haiko fair kabisa

Yaani ulimwengu mzima unajua faru Rajabu amekufa

Wakati siku Kuna binadamu chungu mzima wanakufa na hawajulikani

Kweli acha watu wagombane kuusaka umaarufu
 
Shirikia la Hifadhi la Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kifo cha Faru Rajabu aliyekuwa na umri wa miaka 43, leo Jumatatu Machi 21, 2022 akiwa katika Hifadhi ya Serengeti sababu ikitajwa kuwa ni uzee.

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa Faru John ambaye alifariki mwaka 2015 akiwa na miaka 47.

Faru Rajabu ambaye alizaliwa mwaka 1979 eneo la Ngorongoro, mwaka 1993 alihamishiwa katika Hifadhi za Taifa ya Serengeti, ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.

TANAPA imeeleza kuwa wastani wa maisha ya faru Weusi ambao wapo katika kundi la Wanyama walio katika hatari ya kutoweka hukadiriwa kuwa na kati ya miaka 35 hadi 40.

View attachment 2159078




Akaungane na John aliyekufa mwaka jana.
 
Hawa Kina John, Rajabu n.k. au kama huyu Rajabu pia ana mtoto tukiwatumia vizuri huendwa tukakuza sana utalii wa ndani...

Mfano huyu John huenda alikuwa famous kuliko hata Olduvai Gorge kwa mtanzania wa kawaida
 
Asante kwa taarifa,tutawataarifu na wengine ili nao waweze kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za mazishi,ikiwa ni pamoja na kutuma michango kwa kupitia namba yangu amabayo nitaitoa baadaye...
Picha ya marehemu.
 
Ila Hii Nchi Ngumu, Wizara inatoa taarifa officially Mnyama Kufariki.
.
Faru wana uspesho Gani Mpaka akifariki Taarifa Itolewe wakati Huo Simba+swala wakifariki Taarifa Hazitolewi [emoji3][emoji3]
Screenshot_20220321-132401.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom