TANAPA yatangaza kifo cha Faru Rajabu (mtoto wa Faru John) katika Hifadhi ya Serengeti

TANAPA yatangaza kifo cha Faru Rajabu (mtoto wa Faru John) katika Hifadhi ya Serengeti

Ila faru John nae alianza kugegeda mapema sana yaani akiwa na miaka kumi tu kishatia mimba ya Rajabu
 
Pesa za rambirambi afikishiwe Steve Nyerere popote alipo
 
Kwa sisi wenye mapenzi na wanyama
Tumesikitika sana

Ova
 
Shirikia la Hifadhi la Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kifo cha Faru Rajabu aliyekuwa na umri wa miaka 43, leo Jumatatu Machi 21, 2022 akiwa katika Hifadhi ya Serengeti sababu ikitajwa kuwa ni uzee.

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa Faru John ambaye alifariki mwaka 2015 akiwa na miaka 47.

Faru Rajabu ambaye alizaliwa mwaka 1979 eneo la Ngorongoro, mwaka 1993 alihamishiwa katika Hifadhi za Taifa ya Serengeti, ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.

TANAPA imeeleza kuwa wastani wa maisha ya faru Weusi ambao wapo katika kundi la Wanyama walio katika hatari ya kutoweka hukadiriwa kuwa na kati ya miaka 35 hadi 40.

View attachment 2159078




Huyo Faru Rajabu alisilimishwa nini? maana baba yake ambaye ni Faru John ni Mkristo.
 
Ila Hii Nchi Ngumu, Wizara inatoa taarifa officially Mnyama Kufariki.
.
Faru wana uspesho Gani Mpaka akifariki Taarifa Itolewe wakati Huo Simba+swala wakifariki Taarifa Hazitolewi [emoji3][emoji3]View attachment 2159176

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni aina ya faru, ambao ni tofauti na faru tuloyowazoea
Na idadi yao ilikuwa chache sana duniani

Ova
 
Kwa heshima azikwe na pembe zake mazishi yawe live kwenye tv
 
Haujamuelewa maana yake ni kwamba baba kapata mtoto akiwa na miaka mitatu ila kihesabu ni alikuwa na miaka minne ndio akampata huyo rajabu
Hapana , sio mitatu mkuu
2015 faru John alikufa umri ukiwa 47,
Meanwhile faru rajabu umri ukiwa 36
Kwa mwaka huo

Kama Niko sawa lakni.
 
Back
Top Bottom