TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Lakini operating cost ni ndogo zaidi ya theluthi mbili ya hiyo Tanesco! Na hapa unasahau mambo ya kuwa umeme utakatika ghafla muda wowote.
KUna watu kama wewe mukereheka na kukatika kwa umeme wa Tanesco na kuanza kuwaza solar lakini mukiulizwa umeme unapokuwepo munafanyia nini, jawabu ni kuangalia supersport! Ni uzembe kulilia umeme kwa mambo yasiyo ya maendeleo.
 
Mkuu, Solar PV arries si zinazalisha DC? Hizo converters tutaziweka huko mwishoni, maana hatuna haja ya kubadili AC ambayo hatuzalishi kwenye solar pv modules!! Kumbuka mada iliyopo mezani ni Solar Energy.
Sawa Turudi Kwenye Cost of production and maintaining per unit cost
 
Kuna jamaa anaitwa TUJITEGEMEE namsisitizia Solar Energy is cost per unit price
 
Kweli wewe zero,kwa akili yako hujui kuwa solar inaweza kuendesha kiwanda kikubwa?
Jiongeze kwanza kuelewa solar power ni nini kwa ulimwengu wa leo, kabla hujatapika.
 
jawabu ni kuangalia supersport! Ni uzembe kulilia umeme kwa mambo yasiyo ya maendeleo.
Tujiepushe na kauli za jumla jumla kwa sababu kauli hizo haziwatendei haki wasiohusika.
 
Solar ni umeme mzuri
Viwanda vyote vya eloni musk giga factories vinaendeshwa KWA solar
Amefunga station mbalimbali za umeme wa solar KWA ajili ya kuchajia nagari ya tesla
Elon anasema umeme wa solar ndio future
 
Kweli wewe zero,kwa akili yako hujui kuwa solar inaweza kuendesha kiwanda kikubwa?
Jiongeze kwanza kuelewa solar power ni nini kwa ulimwengu wa leo, kabla hujatapika.
Hata mafuta ya ndege yanaweza endesha kiwanda kikubwa. Tunachotaka ni gharama ndogo za uendeshaji. Hakuna kenge yeyote anayefanya biashara atatumia solar energy badala ya HEP.
Hao kina Elon Musk na Tesla yake wanatengeneza magari ya umeme ili ya mafuta yasichafue mazingira. Ila wakati huo umeme wa kuchaji magari yao hawajui unatoka wapi. Na wala viwanda vya magari yao havitumii umeme wa jua.
 
Sawa Turudi Kwenye Cost of production and maintaining per unit cost
Mara nyingi wale wafuatiliaji wa masuala ya gharama za kuwekeza kwenye biashara ya umeme upenda kutumia factors kama levelized cost of energy, specific capital cost, na nyinginezo. Factors hizi, uondoa upendeleo katika maamuzi ya kujua ni mradi gani wa umeme utakuwa na faidia.

Sasa tukiamua kutumia mojawapo tu ya parameters ( cost of production and maintaining) zitumikazo kukokotoa factors nilizoeleza awali tutakuwa hatufanyi maamuzi sahihi katika kuhukumu uhalali wa Tanesco kujiingiza moja kwa moja kuwezesha upatikanaji wa umeme kwa nguvu ya jua ( solar energy).

Mkuu, asante kwa changamoto zako, nikutakie siku kuu njema na heri ya mwaka mpya na mimi najitakia siku kuku njema na heri ya mwaka mpya. Amina.
 
Kweli wewe zero,kwa akili yako hujui kuwa solar inaweza kuendesha kiwanda kikubwa?
Jiongeze kwanza kuelewa solar power ni nini kwa ulimwengu wa leo, kabla hujatapika.
Unao mfano wa hicho kiwanda au uliona kwenye film?
 
Unao mfano wa hicho kiwanda au uliona kwenye film?
Panua ubongo,Huko Morocco wanazalisha umeme wa solar in mass production.
Wanaendesha viwanda vikubwa kwa umeme huo.Sio tu hapo kuna maeneo mengi kama China ,India wanafanya hivyo.Ndio maana nilikwambia jiongeze mkuu.
Siku za usoni sitashangaa kuona Solar ndio tegemeo kuu la uzalishaji umeme hasa kuzingatia kutunza mazingira.
 
Mjadili huu unavyoendelea nimesoma michango ya wana JF. Nilichokihisi, kuna wana TANESCO kibao ndani wanatetea hata wasiyoyajua. Hawa watakuwa mainjinia waliosoma umeme, wana digrii hawajui lolote nje ya umeme.

Ulichokisema kuhusu mazingira, nilishakiona hapa. Nimekitafuta na kukuta kwenye msg #144 kuna mtu alimfundisha mchangiaji wa TANESCO anayejiita TheDreamer Thebeliever aliyejaribu kuonesha kwamba anajua sana mambo ya mazingira. Naona hakurudi kwenye mjadala.
 
TUanjadili mambo ya usoni au mradi wa sasa wa TANESCO? Kwani hujui usoni hatutahitaji jua kuzalisha umeme?
 
Wewe your outdated,tekinologia ya solar imeishapiga hodi katika mataifa mengi, na zimefanyika breakthrough ya solar panel hata battery.
Hata ujenzi wa nyumba kwenye watu makini wanaezeka kwa solar panels.
Kama hiyo haitoshi wenye nyumba wanazalisha umeme wa ziada kuliko matumizi yake na kuuzia makampuni makubwa ya ugavi wa umeme.
Lakini solar tekinologia imehujumia na makampuni yanayozalisha mafuta.
 
TUanjadili mambo ya usoni au mradi wa sasa wa TANESCO? Kwani hujui usoni hatutahitaji jua kuzalisha umeme?
Ahaa jua ndio baba wa umeme, Mwenyezi Mungu katupa jua tulitumie kwa maarifa.
Wewe endelea kuabudu outdated tekinology.
 

Nipo tayari Mkuu.

1. Watts 60
2. Taa moja chumbani ,nyingine sebuleni ,moja kibarazani ,nyingine kwa nyuma ya nyumba nje...Taa za watts 5
3.Chumba ni 3.5m kwa 4m na kimo ni 4m.
4.Mkoa - Manyara - MINJINGU.
5.Orientation - sina uhakika wa angle lakini imefuata slope ya bati.
6.Nimeweka upande wa jua limapochomozea.
7.Solar hizi unauziwa mfumo mzima kwa laki na 45.
 
Mkuu, Solar PV arries si zinazalisha DC? Hizo converters tutaziweka huko mwishoni, maana hatuna haja ya kubadili AC ambayo hatuzalishi kwenye solar pv modules!! Kumbuka mada iliyopo mezani ni Solar Energy.
Issue iliyokuja mezani ni kusafirisha DC over long term sio Economical,

Kusafirisha DC over very long distance in theory ni bora kuliko(but mostly not economical) AC kwa sababu ya Reactance loss ya AC (But this one has solutions...

Normally DC will be constant kwenye waya therefore inaweza kuwa na Madhara, ndio hapo inabidi utumie hizo configuration za Converter which are very expensive
 
Mkuu, Solar PV arries si zinazalisha DC? Hizo converters tutaziweka huko mwishoni, maana hatuna haja ya kubadili AC ambayo hatuzalishi kwenye solar pv modules!! Kumbuka mada iliyopo mezani ni Solar Energy.
For very LARGE DISTANCE and VERY HIGH VOLTAGES, DC is preferred over AC. Actually there is a break even point for transmission line distance (600–700 kms) beyond which DC transmission is cheaper than AC mainly because only 2 lines are required (or 1 if you take ground for return path) and absence of skin and proximity effects.

But DC becomes costly for sub 600 km distance due to the presence of expensive converting stations. AC is preferred in such scenarios due to the flexibility in voltage transformation allowed by cheaper and efficient transformers which helps in better and more economic transmission of voltages over this range.

So niambie Solar plant gani yenye very large voltage ambayo unataka kuisafirisha kutoka Songea hadi Kagera au Dar hadi Arusha...
For that investment mtu atatakiwa kununua unit ya umeme kiasi gani
 
Asante kwa kujibu maswali kama livyouliza.

Mkuu, kwa haraka kabisa ninaona kosa kwenye namba 5 na 6. Na makosa haya yamefanywa sehemu nyingi tena sehemu nyingine unakuta ni mradi mkubwa kabisa lakini namba sita na namba tano zako zimewapiga chenga. Makosa haya uchangia pakubwa kwa sababu yanaathiri uzalishaji wa umeme kutoka kwenye panel.

Ipo hivi, panel uweza kuzalisha umeme kwa kiwango cha juu sana endapo muale wa jua utaipiga panel kwa pembe mraba yaani katika nyuzi tisini. Kwa kuwa jua ubadilika orientation kwa siku ( asubuhi jioni) au majira ya mwaka ( March Ikweta, Juni Tropiki ya Kansa September Ikweta na December Tropiki ya Kaprikoni), ili kufanisha zoezi la kuhakikisha muale wa jua unagonga panel katika nyuzi tisini yahitajika tracking system ya kugeuza panel kulifuata jua. Hii uongeza gharama kwa system ndogo ya umeme jua.

Hata hivyo, wataalamu walishafanya ukokotozi wa kupata muale wa jua kwa kiasi kikubwa kwa siku na mwaka bila tracking system. Kwa upande wako ambaye upo Arusha. Arusha Latitude yake nadhani ni mbili au tatu na ipo kusini mwa Ikweta. Kwa hiyo unatakiwa utege panel yako katika nyuzi 10 kujumlisha nyuzi za latitude ya Arusha. Tukichukulia Arusha Latitude yake ni tatu, basi panel itegwe nyuzi 13 kutoka uso wa aridhi ulio sawa ( horizontal surface). Na itegwe hiyo panel kwa ukuangalia upande wa Kaskazini kwa sababu Arusha ipo upande wa kusini mwa Ikweta hivyo muda mwingi jua litakuwa upande wa kaskazini mwa Arusha. Cha msingi pia, usilaze panel yako juu ya bati. Inyanyue kwa kuiwekea stendi ambayo ni zaidi ya sentimeter ishirini kutoka uso wa bati. Joto likizidi upunguza uzalishaji wa umeme kutoka kwenye panel. Kwa viwango maalumu vya utengenezaji wa panel, Joto la nyuzi joto 25 ndilo hutumika kupimia hiyo kiwango kikubwa cha umeme ( maximum power) kizalishwacho na panel. Joto likiongezeka in away power upungua.

Kwa uchache hayo tu ni baadhi ya matatizo yanayoweza kuwa yamefanya system yako kutofanya vizuri kadiri ulivyotarajia. Kwa masuala mengine tuwasubiri nguli wa utaalamu wa mambo ya umeme huu wa jua watuelimishe.

Nikutakie siku kuu zote njema. Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…