TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Mkuu thanks,

Ila ulichoelezea ni mechanism ya generation ya power pekee kwa solar.

Sasa tunachohitaji hapa ni breakdown ya gharama kwa unit moja inayotokana na Solar na ile inayotokana na umeme wa maji/oil/gas ili basi sisi vilaza wa maswala hayo ya umeme tuseme kweli mradi wa solar ni gharama kuliko wa maji ama vinginevyo.
 
Hawezi.
Huyu nadhani bado ni mwanafunzi mahala fulani.

Hata kama bado ni mwanafunzi, inashangaza yeye kutojua kwamba kuna kampuni tayari zinazalisha umeme wa solar na kuuingiza kwenye 'grid' na kusambazwa kwa watumiaji!
 
Kwa nini gesi haijawa mwarobaini wa mahitaji ya umeme kama tulivyoaminishwa
 
Ndugu yangu solar cells ni semiconductors material they shall be costly kuliko Electrical machines
 
Najigamba kwa sababu nafahamu vyema zaidi ninachozungumza..

Tafuta watu kumi wanaotumia solar energy uwaulize kuhusu gharma yake
 
Najigamba kwa sababu nafahamu vyema zaidi ninachozungumza..

Tafuta watu kumi wanaotumia solar energy uwaulize kuhusu gharma yake
Kutokana na unayoandika hapa, sioni huo "ufahamu vyema" unaojinadi nao.

Kwa mfano hilo unaloandika hapa la "tafuta watu kumi wanaotumia solar energy", kwani hujui kwamba matumizi ya "photovoltaic panels" kwa matumizi ya nyumbani ni tofauti na kuzalisha umeme wa kuingiza kwenye gridi?

Huko nyuma ulishatoa mfano wa China, na kuna mataifa mbalimbali yanayozalisha umeme kwa ajili ya usambazaji, unadhani hawa hawajui gharama hizo?

Nikakuomba utupe mchanganuo wa gharama kati ya "thermal na solar", lakini ukapiga chenga! Sasa unataka tuseme ujuaji wako upo sehemu gani?
 
Stupid abstract! Nuklia, duniani kote, bhla! bhla!
Umeingia mtego huo huo kwamba hakuna hata ulichoeleza zaidi ya kutukana. Unaamini huyu mtu hajui chochote? Wewe unajua nini? Tueleze ili tujue unajua chochote. Unawezaje kutumia neno duniani kote bila ushahidi. Rwanda, Burundi Congo, umewatembelea? Katika njia mbalimbali unazotaja solar imo? Nchi gani inayotumaini solar iwe ni njia muhimu, mbadala ya umeme? Shiiit!
 
Wewe ni mpuuzi mmoja tu aliyelewa bangi. Sina muda na wapuuzi kama wewe. Go f*c* yourself.

The last part of your diatribe merits a sensible response.

Unauliza, ni "nchi gani inayotumia solar iwe ni njia muhimu, mbadala ya umeme"? Ondoa ulevi wako, halafu unionyeshe katika maandishi niliyoweka humu nilipoandika maneno kama hayo uliyotumia wewe au yenye maana inayofanana na maana ya maneno yako. Ni wapi nilipoandika solar iwe mbadala? "Muhimu", ndio; kwa sababu inaweza kuchukua nafasi ya 'thermal'.
Na kama sehemu ya "energy source mix", 'of course. Sijaandika popote kuonyesha kwamba itakuwa 'mbadala'. Kwa hiyo achana na ulevi wa bangi unapochangia humu ndani.
Nimekujibu kiungwana kwa sababu ni mara ya kwanza kukutana na mpumbavu kama wewe. Hutapata 'privilege' kama hiyo tena hoodlum!
 
Niliamua kuacha kujadili hii mada baad ya kuona shida ya watu kuelewa vitu vidogo...

Mfano inawezekana kutoa Nishati kutoka kwenye maji (kwa kutenganisha Hydrogen na Oksijeni) mtu wa kawaida ukimwambia maji ni Rahisi anaweza kuona hii Njia ni cheap kuliko kununua mafuta, kumbe process ya kuipata hiyo Hydrogen na kuifanya kuwa nishati ni ghali kuliko hata kununua mafuta...

Kuna wazee wetu waliwahi kuwekeza fedha kadhaa kwenye umeme wa solar kwa matumizi ya Nyumbani baada ya mwaka wakajuta
 
Hakuna safe and clean Energy kuliko Nuclear fusion. changamoto ni kutengeneza Reactors zake...so ukitaka cheap and reliable energy ni Maji, mafuta na gesi
Mkuu, kuna kitu hakiko sawa katika uamini wako. Unapoweka "mafuta" katika orodha hiyo, inastia shaka una maanisha kitu gani. Umeme wa mafuta ni wa aghali sana kuliko njia nyingine yoyote kwa sasa. Huwezi kamwe kuiweka njia hiyo katika orodha ya 'cheap'.

Na hili la "nuclear fusion", nadhani una maana ya "nuclear fission". Nimeona ukirudiarudia kosa hilo.
 

Kuna aina mbili za kugenerate Energy from Nuclear process
1. Nuclear fission
2. Nuclear Fusion

Nuclear fusion​

Yenyewe unaunganisha two atomic nuclei, mfano ni namna nyota zinazalisha energy yake

Nuclear Fission
Unavunja radioactive material kama Uranium
 
Kuna wazee wetu waliwahi kuwekeza fedha kadhaa kwenye umeme wa solar kwa matumizi ya Nyumbani baada ya mwaka wakajuta
Huu "umeme wa nyumbani" mkuu wangu 'Intelligent Electronics', ndio unaochanganya unayoyaweka hapa. Huu ni umeme unaotokana na hivi vi-'solar' panels watu wanavyoweka kwenye mapaa ya nyumba zao na kuchaji simu na kuwashia balbu.
Kuna umeme wa solar unaozalishwa maksudi kwa kuingizwa kwenye gridi, kuunganishwa na ule unaozalishwa na njia nyingine mbalimbali za kuzalisha umeme. Bila shaka huu ndio uliokuwa unauandika juu yake ulipokuwa ukiwataja waChina kuwa nchi ya pili duniani. Kuna tofauti kubwa kati ya solar hizi mbili.

Hapa ndipo unapotakiwa kuweka focus ya mawazo yako katika kutofautisha njia hizo. Bila shaka, Tanesco hawana nia kabisa ya kutumia 'Photovoltaic panels' katika kuzalisha umeme wao wa gridi. Uganda wanazalisha umeme wa gridi kwa solar, hata Kenya wanao kiasi kidogo, mbali kabisa na huo wa 'solar panels' zinazotumika majumbani mwa watu binafsi. Umeme wa mafuta kamwe hauwezi kuwa nafuu zaidi ya umeme wa solar, per unit.
 
Hii ni sawa, lakini sijui reactor yoyote kwa hivi sasa inayotumia "nuclear fussion" Kama ipo, basi sina taarifa nayo. Ni nchi gani inatumia hii njia?
 
Kuna wazee wetu waliwahi kuwekeza fedha kadhaa kwenye umeme wa solar kwa matumizi ya Nyumbani baada ya mwaka
Kuhusu suala la wazee wetu hao, tunahitaji kujua nini kilitokea toka:
1. ununuzi wa vifaa hivyo ( kuna vifaa fake, mfano unakuta battries robo tatu ya cells zake vipande vya 'sabuni' ama solar panels nusu nzima ya cells ni karatasi silizomwagiwa wino wa 'givii'),

2.usimikaji wa mtambo huo wa solar ( kunawafungaji hawafuati masharti ya ufungaji, mfano juzi kuna mwenzetu hapa alikuwa na tatizo la ufungaji tukaelezena), na

3.uendeshaji/matumizi ya mtambo ( kama una weka load ya 6000 Wh/day wakati uwezo wa mtambo ni kubeba 3500 Wh/day lazima mtambo ufe tu na hasa kama Charge controller ama inverter ya mtambo hawezi kudetect over discharge sawsawa). Yaani, kuna mtindo wa watumiaji wanaambiwa kuwa mtambo, mfano unaweza kuchaji simu 50 kwa siku...yeye kwasababu wataje ni wengi anafunga chargers 150! Mwisho wa siku ni kuharibu betteries za simu za watu na mtambomwake mwenyewe!

Namba moja na mbili hapo juu, ili kuepuka matatizo hayo, watafute Tanzania Renewable Energy Association (TAREA) watakupatia dealers wa vifaa sahihi/ orijino vya solar orijino. Pia TAREA watakupatia technicians waliobobea kwenye kufunga mitambo ya solar Tanzania nzima. TAREA wana website ambayo ina page yenye directory ya dealers, engineers, technicians wanaohusika na masuala ya solar na teknolojia nyingine za nishati jadidifu

====
Kwa maelezo hayo hapo juu, ni kuhujumu kampeini sahihi na halali za kuhimiza matumizi ya nishati itokanayo na jua kwa kuleta habari za mapungufu ya mitambo ya kuzalisha nishati itokanayo na jua bila ushahidi usiotiliwa shaka!
 
h2020-wp1820-cc-activities_en.pdf

EU Green Deal opportunity.

Business opportunities for Energy companies / Energy Engineers

Wasiliana kupitia Inbox yangu, Commercial Adviser, Turboden/ EC Energy.
 
Wewe ni ka-mtu kazembe tu! Hakuna mradi wa solar unaosifika kuwa cheap energy source, haupo!! Miradi mingi ya solar inakosa sifa hizo na wale wanaoifagilia wanataja sana mambo ya carbon saving, which is totally stupidity for a country like Tanzania kuamini faida ya mradi iwe ni carbon saving wakati tunaelewa leeway tuliyonayo kwenye mambo ya carbon.

Kuna sehemu unasifia Uganda na Kenya, nicampoop! Ukitaka kujua akili haikutendei mema, Linganisha gharama za Bujagali hdro power na solar farm ya kabulasoke au Soroti solar project. Nahisi unajiandikia kwa kusikia tu.
Eti hata Tanesco na wewe mwenyewe unakuja na mifano ya Uganda na Kenya na bhlabhla! eti ni cheap energy. Fallacy! Kuna wakati naamini munaenda shule kukariri vitabu tu! Afrika ikiendelea kuwa na watu wa aina yako serikalini tutafanyiwa majaribio hadi kiama.
 
Achana na hao watu ukisikia mtu anasema solar ni cheap kuliko Hydropower achana nae mara moja... either haelewi kabisa anachosema au anahadithiwa zile story jua ni bure basi ukitumia solar utapata nafuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…