TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Mradi wa umeme wa jua ukiacha gharama zake, ila zaidi Tanesco kuwa sehemu ya uwekezaji huu ni pigo zaidi.

Ingekuwa ni shirika tofauti la kuleta ushindani dhidi ya Tanesco ingeleta unafuu kwa watumiaji wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio
Cost-base ya solar nchi hii tunaijua kama umetumia chini ya milioni tano hayo ni mahitaji ya chumba na sebule. Hakuna haja ya kujidai kulinganisha energy mbalimbali kwa matumizi kama hayo.
Kama hujui sema ufundishwe ulekezwe ndugu!!!..unajua umeme watts 1000 ni panel ngapi za solar za Germany!!!..unajua watts 1000 unaweza kufanya vitu gani au wewe unaishi kwenu na umekariri!!!..
 
Nili
Kwa level ya familia sawa ila Tanesco wanafanya kwa level ya taifa
Hata huo umeme wako uliotumia kwa miaka 6 uliwahi kuangalia gharama ulizotumia kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nifanya gharama haijafika 5 millions nawasha fridge,Tv, taa zote masaa 24, computer na vitu vengine vingi!!!..
 
Wewe ndio
Kama hujui sema ufundishwe ulekezwe ndugu!!!..unajua umeme watts 1000 ni panel ngapi za solar za Germany!!!..unajua watts 1000 unaweza kufanya vitu gani au wewe unaishi kwenu na umekariri!!!..
Tatizo unajadili mambo yako ya nyumbani wakati sisi tunajadili Tanesco. Kila mtu analazimisha asimulie ya nyumbani kwake. Nawe unakuja na 1000 W! Ndo nini hicho? Tunajadili jambo la kitaifa kiuchumi, siyo fridge na pasi ya umeme ya nyumbani kwako.
 
Nimeona majadiliano haya yanavyoendelea. Kikubwa ni ignorance kwa watu wengi juu ya hicho kinachoitwa Solar energy na suala la mazingira. Nikianza na huyu; yeye anaamini kuzungumzia mipango ya tanesco ya 2050 ni kuwa selfish. Anaweka na kingereza ka kimarekani kidogo ili aonekane najitambua. Naye yuko kundi la elimu mbaya tu. Hizo unazoita house gas ni kitu gani?

Kimataifa third world hailazimishwi kutimiza matakwa ya emission kwa sababu za kiuchumi. Hatuna uchumi unaoweza kuyatimiza na tukijilazimisha kuyatimiza hatutafika kokote. Wanaolazimika ni walioendelea kwa sababu zinazoeleweka ingawa wao pia zinawapa taabu sana! sasa wewe unawashabikia Tanesco kujiingiza huko kwa sababu ambazo umesamehewa! huko ni kuturudisha nyuma bila sababu. Waambie wahangaike na hydro. Achana na bhla! bhla! Mambo ya mazingira siyo uelewa wako.

Ulaya na US imetuacha nyuma kwa karne mbili! Pamoja na hayo, hakuna nchi inayotumia umeme wa solar au wind hata kwa robo ya mahitaji yake. Kwa nini wewe ujikweze kwa kisingizio cha mazingira?
 
Nili
Nifanya gharama haijafika 5 millions nawasha fridge,Tv, taa zote masaa 24, computer na vitu vengine vingi!!!..
Ongezea na kuchaji simu. All in all, hiyo ni mipango yako. Tanesco ni mipango ya taifa, uchumi wa taifa na maendeleo ya taifa. Hawawezi kupanga kwa kuhesabu fridge, Tv na computer yako.
 
Mkuu unatoka shimo gani la giza , tena gizo totoro la ufahamu.
Ulichoandika ni sawasawa na mababu zetu waki argue kuwa taa za koroboi ni bora kuliko umeme miaka ya 1940s!

Elimu , elimu, elimu!!!!
 
Very true.......
"...........Wakati mwingine ni uungwana kukubali kuwa wewe ni mjinga na pengine mpumbavu inapotokea kitu unachofahamu kuhusu jambo fulani ni matokeo ya ujinga ulio nao...."

WHO can argue with that!!
 
Mashirika ya umma Tanzania ndio kwenye vichaka vya ufisadi wa hali ya juu kwa ivyo si ajabu hawa watu kuja ni miradi ya ovyo ovyo.

Gharama za kuwekeza kwenye renewable energy sio ndogo kabisa, return inachukua muda.

Asilimia kubwa ya makampuni yanayofanya ivyo nchi za ulaya yanapata government incentives au yanachangiwa na makampuni yanayozalisha CO2 and other toxic gases in large quantities kama vile oil refiniries, viwanda vya vyuma, uzalishaji wa makaratasi etc with polluting industries.

Ivyo kupitia environmental policies zao ndani ya EU kuna limit za kuchafua au ukitaka kuendelea na uzalishaji inabidi uwekeze kwenye greener energy kama part ya carbon trade off au ulipe fine ukizidisha allowed emissions na ndio hizo hela serikari inazotumia kuwekeza kwenye greener policies zao.

Hizo farm zenyewe hili ziwe meaningful kuzalisha umeme labda tuseme sawa na ‘kinyerezi I’ si ajabu ukakuta unahitaji more than 100 acres za ardhi sasa hiyo ardhi ya kuchezea utaitoa wapi in the long run.

Kwa Tanzania kuwekeza kwenye renewable energy sio shida kwa sasa kwa hali ya uchumi wa Tanzania na average pato la kila mtu. Hila kama tuna imani ipo siku asilimia kubwa ya nyumba za Tanzania zitakuwa na airconditions, jiko la umeme au gas, washing machine, friji, TV, pasi ya umeme etc kama nyumba za wazungu. Kutakuwa na network ya train ya umeme nchi nzima, viwanda vitakuwa vinaajiri labda 60% ya watanzania, etc with development and the rise of energy demand ni upuuzi kujiingiza kwenye renewable energy kwa sasa.

Chances are kwa sasa kuna kampuni huko EU inataka kufanya trade off wao waendelee kuchafua kwao under EU rules ukiwekeza third world kwenye renewable energy inahesabika kama sehemu ya Carbon Trade off, ni upuuzi kama huu na tamaa ya hongo ndio utakuwa nyuma ya pazia otherwise hakuna mzungu atakuja kuwekeza Tanzania kwenye renewable kibiashara the return takes too long, kama ni biashara angetaka gesi maana tunayo ya kutosha and has more quick return.
 
Nina uzoefu wa kutumia sola power Dar tangu 2005. Nilifunga ya kutosha kutumia taa za nje na za ndani, fridge, mafeni na tv. Mchana natumia pump ya maji (borehole ya mita 65) kumwagilia bustani. Mashine ya kufua na pressure pump pia. Na kufunga na kufungua gate.

Sijapata maintenance cost yoyote kwa miaka 15 hadi sasa, na hakuna dalili ya kupata maintenance costs. Kwa kawaida mchana natumia sola na usiku Tanesco, ila kukiwa na shida ya umeme wa Tanesco natumia sola usiku pia. Yaani sikatikiwi umeme.

I recovered my investment long ago.

Sola ni mwarobaini wa umeme, hasa sehemu ambazo haziko kwenye grid. Hata kwenye grid, ni vema kuwa na angalau backup ya solar. It's reliable, reasonanly priced and maintenance free. Kwenye Parokia yangu lazima nishauri tuweke sola kama backup, na sio generator la diesel, kelele na moshi.
 
Kweli mkuu! Hii haina utofauti na yazima moto.
Umeme wa sora nimpango wa kupiga tu! Km serikari inatoa pesa !
Labda kama ni wabure
 

Nikipofika kwenye eti hujui green houses gases nikajua naongea na chizi

Good riddance!
 
Mleta mada sio solar farm nadhani hyo pronunciation ulivosikia ukafikiri ni farm, hyo inataandikwa solar firm nadhani hili swala hulijui vizuri usipotoshe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Solar ni best kwa matumizi Tena kwetu Africa tunakopata jua la uhakika the only challenge ni kufunga mitambo kwa Mara ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee ni kweli asikundanye mtu, umeme utokanao na jua ni ghari sana mimi ni mtaalamu kwa sekta hiyo angalau kidogo kwa huu utokanao na upepo.
 
Nikipofika kwenye eti hujui green houses gases nikajua naongea na chizi

Good riddance!
Mmmmh! Angalia meseji yako ya mwanzo angalia tena hicho ulichoandika. kama dunia hii in mtu anayefahamu Green houses gases, fahamu huyo yuko kundi tofauti. Hiki ni nini? Nonsense! Bado unashiriki mjadala unaohitaji ufahamu!
Kuandika makosa ni kawaida lakini kurudia tena na tena, inaonesha siyo kosa bali hujui hata unachoandika. Sahihisha mwenyewe maana naona tayari umekariri makosa, na unayarudisha JF ukiamini ni sahihi.
 
Mleta mada sio solar farm nadhani hyo pronunciation ulivosikia ukafikiri ni farm, hyo inataandikwa solar firm nadhani hili swala hulijui vizuri usipotoshe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kitu hujui na unatumia mtandao, umeshindwa kuingia google au yahoo ukapata tofauti ya unachokijua na kilichoandikwa? Solar firm ni nini sasa? Siyo kila kitu uchangie, mengine waachie wenyewe.
Tuna solar farm na wind farm. Tafakari!
 
Usiandike kama uko sayari tofauti boss. Simply, niambie uliweka betri za aina gani ambazo zimekupa service kwa miaka 15? Taja jina la betri, tuanzie hapo. Kumbuka life span ya solar pannel haizidi miaka 20 pia.

NInacholumbushia hapa, tunazungumzia Tanesco. wanaolenga kukuza uchumi wa nchi. watupe umeme wa viwanda siyo pump na kuosha gari.
 
Hii ni sahihi! Hii ni Clean development Mechanism na Carbon trading. Kwa maana nyingine anayeweka pannel anategemea kupata pesa kutoka kwa yule anayechafua, kwa kuuza carbon equivalence. Sasa hapa JF sijui wapo wangapi wanaoweza kuelewa hilo. Angalia mifano wanayotoa ya kuwasha taa na pump za maji. Ni watu wanajadili maisha ya kwenye nyumba zao badala ya taifa.
 
Mkuu JF kama ni muelewa wa masuala fulani siku zote angalia line of reasoning za mtu if you want to get a meaningful debate.

Mtu mwenye uelewa wa maswala ya global energy policies lazima afahamu nini kilikubaliwa kwenye Kyoto Protocol, Paris agreement, nani anatekeleza na kwa namna zipi, kwanini kwa first world ni strict whereas in third world wamepewa leeway’s bado za kuwekeza kwenye fossil energy, jinsi Carbon Trade inavyofanya kazi duniani, reliable energy sources ni zipi na kwanini nchi kama US wamejitoa kwenye Paris Agreement etc with the global energy industry.

Mtu anaeongea sijui umeme wa upepo ni bora kushinda jua wakati vyote ni bure; sijui mambo ya Solar Firm, jua kujibizana nae ni kupoteza muda wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…