TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Mleta mada hakuna anachokijua kuhusu maswala ya energy hata certificate ya energy sidhani kama anayo,ss ndio tume master kwny hiyo sector tumekaa class 4 yrs+masters degree ya hiyo kitu.

Unasema mleta mada anaongea kuhusu energy efficiency mm nakataa mleta mada anaongea bla bla sababu hata ni kimuuliza energy efficiency ya PV au concentrate solar inakuwa calculated VP hawezi jibu,!!!nikimuuliza zile yaw na pitch angle zina setiwa VP kupata optimal electricity production hawezi jibu!!ss ww na mleta mada hakuna mnachokijua kuhusu energy efficiency.Ikiwa hamjui factors zinazo affect hiyo energy efficiency.

Hzo no taaruma za watu,kuingilia taaruma za watu ni kuwa unprofessional.Juzi kocha wa Liverpool kaambiwa azungumze chochote kuhusu Corona kakataa kasema yy sio taaruma yake.Waacheni watu wenye taarum zetu ndio tujadiliane na Tanesco hayo mambo.
 
Kama ni hela zake hakuna shida, hila kama TANESCO wanaweka hela hapo ndio tatizo.
 
Hayo sasa atakuja jibu mwenyewe anajua kwa kiwango gani, but he comes across knowledgeable on matters of strategic planning.

Nisije mwekea maneno ambayo hakusema ‘energy efficiency’ hilo neno mimeliweka mimi. Policy wise watu wanapotumia neno energy supply efficient it refers to demand and supply requirement. Sio mambo ya mgao mgao au kukatika katika wakati kuna mahitaji.

Na nilivyomuelewa mimi yeye alikuwa anaangalia sustainable and reliable sources za muda mrefu na kwa angle hiyo he made lot of sense.

Anyway mchana mwema.
 
Kama ni hela zake hakuna shida, hila kama TANESCO wanaweka hela hapo ndio tatizo.
Usijisahaulishe boss wangu tupo busy na Stiglers gorge boss ,mradi wenye uwekezaji mkubwa na wenye manufaa makubwa katika sector ya nishati .

Hawa wanakuja ni watu wanataka kuwekeza kwny nishati,TANESCO hawawezi kuwakatalia.

Nasikia yule msanii wa Senegal (AKON) naye anampango wa kuja kuwekeza kwny hayo maswala ya nishati mbadala huku Afrika.
 
Stiglers Gorge kwenye post za awali utaona niki support.

Na upande wa uwekezaji yeyote anaekuja na utaratibu wa hela zake, kuendesha na kuuza sio shida. Isiwe tena return ni jukumu la serikari sijui kuna government guarantees hapo ndio shida.
 
Huko kwenye taaruma zenu efficiency ndio maana hiyo lakini engineer akisema energy efficiency tunamanisha mfano kama unatumia KWh 10 kupikia utadesign VP system yako ili kupunguza hicho kiasi kwa kupikia utumie angalau kwh 2kwh.Hapa sasa kunaingia mambo chungumzima kama kupunguza noise,energy waste,green house gases,costs n.k.
 
Stiglers Gorge kwenye post za awali utaona niki support.

Na upande wa uwekezaji yeyote anaekuja na utaratibu wa hela zake, kuendesha na kuuza sio shida. Isiwe tena return ni jukumu la serikari sijui kuna government guarantees hapo ndio shida.
Kifupi mambo ni mengi mda ni mchache,serikali haiwezi toa hela kizembe zembe wakati yenyewe inashida na pesa.Tupo pamoja boss.
 
Uzi nimeupitia ngoja na mimi nitoe mchango wangu kwanza Tanzania tunatumia karibia asilimia 50 ya nishati kupitia renewable energy hapa nikimaanisha Hydro ppwer na ndio major contributors za Power kwenye Grid ikifatiwa na Thermal ila tu Kwa taarifa yako future ya dunia ni Renewable energy hii solar ni ya milele tofauti na vitu kama mafuta au Nuclear ambavo ni limited, Swala la tanesco kutaka ku opt na solar sijaliona ila mimi sioni tatizo lolote la wao kufanya ivo kwanza nchi inakuwa secured zaidi mkiwa na multiple sources of power hata kwako imagine una Tanesco, Generator na Solar je Power security yako ikoje apa incase mtu akishambulia chanzo kimojawapo cha Nishati?? Renewable enegy kama solar zina very high initial costs ila pia running costs zake ziko chini sana compare na hizo nuclear au thermal plants ambazo initial costs ni low ila running ni very costfull tuki calculate payback solar inalipa japo inatikiwa pasiwe na upigaji tu ikitokea upigajo wowote tu kama Wrong designing au kutonunua vifaa genuine basi solar mtaona taka taka acheni tuwe na multiple sources of energy for security of our country ila nguvu zaidi iwekwe hapo Rufiji hio project ikimalizika na ikafua MW 2100 basi tutegemee kuongoza kwa Ukanda wote wa afrika mashariki kwa energy kitu ambacho kitafanya tuwe na energy nyingi tu
 
Mkuu kumbuka mleta mada hajui kama hydroelectric power ni renewable energy!!! Nimemshangaa kweli mleta mada. Lakini nashukuru kama siyo mvivu wa kusoma atakuwa amepata jibu mujarabu kwenye uzi wake huu.
 
Tatizo litakalotokea kwa hawa IPP watakao jiingiza kichwa kichwa kwenye biashara hii ya solar hapa nchini ni kusimika mitambo ya solar bila kuwa na Reliable Solar radiation resource availability data.

Kumekuwepo na mazoea ya kutumia satellite data za NASA na vyanzo nyingine kwa ajili ya kufanya tathimini na usanifu wa mifumo ya nishati ya jua/ Solar PV systems. Satellite data zina utofauti mkubwa sana( kati ya 18-45%) na kiasi halisi cha solar radiation kinachoweza kukusanywa na Solar panels ardhini/on ground. Na utofauti huu unaweza kusababisha hasara kubwa sana.

India waliingia mkenge wa namna hii wakatumia satellite data kusanifu na kusimika mifumo mikubwa kabisa ya solar pv na CSP systems...kumbe data hizo ni tofauti na uhalisia. Walipata hasara sana...wakaamua kufanya thorough Solar radition resource Assessment ardhini karibu kwa kila makutano ya latitude na longitude kwenye nchi yao. wakatengeneza mfumo mzuri wa kuchakata takwimu walizokuwa wanakusanya kutoka kwenye weather stations zao( Al maarufu SRRA stations). Na hizi SRRA stations zilisimikwa vifaa vya kisasa vya kukusanya data za solar radiations( direct, diffuse type raditions), hapa usiniulize vituo vyetu vya hali ya hewa vina kusanya takwimu zake kwa staili ipi. Kwa India, SRRA zinakusanya takwimu kwa temporal resolution ya mpaka 10 seconds. Na takimwu hizi zikishachakatwa zinatumiwa na mabenki kwa ajili ya kufanya investment assessment ya miradi wanayotaka kuipa mikopo. Yaani SRRA zinatoa Bankable data.

Sasa nikijikita kwenye mada...ingawa mleta mada kavuruga mambo mengi kwenye uwasilishaji wake wa hoja( kwa kutoa kauli zisizo na uzito wa kiushahidi), lakini hoja yake inaweza kuwa na mashiko kwani Kwa Tanzania, Sidhani kama tuna bankable data za Solar radiation resources na hata Wind pia kwa nchi nzima na kwa mikoa lengwa hasa. Yàani hatujafanya ground data assessment za nishati jadidifu(solar na wind) kwa kutumia vifaa vya kisasa na ' reliable' (kwa kufanyiwa calibrations zinazotakiwa) kwa spatial resolution ya karibu mraba unaotengenezwa na latitude na longitude kwa mpishano wa degree moja na temporal resolution ya basi hata ya robo saa.

Takwimu hizi zikikusanywa kwa miaka matatu mfululizo, kwanjia niliyoeleza hapo juu, zinaweza kusaidia kufanya reliable assessment ya investment kwenye miradi husiaka ya solar na wind bila wasiwasi.

Kwa hiyo, binafsi nawashauri TANESCO wasitishe tenda hizi kwanza na wajikite katika kuwezesha kufanya on ground solar radition and wind resources assessment kwa angalau miaka mitatu kama nilivyofafanua hapo juu ndipo sasa wahitishe tenda hizi.

Yangu ni hayo, lakini wanaJF nawakumbusha tunapotaka kushauri ama kukosoa kitu iwe kwa serikali ama watu binafsi tuache kufanya hivyo kwa kejeli, dharau, lugha za kuudhi na kadhalika. Tujenge hoja kwa staha.

Asanteni.
 
Nadhani umezunguka sana kiasi umeshindwa kuelewa unakotoka na unakokwenda. Kama mtu binafsi anawekeza pesa yake kwa nini Tanesco ndo itangaze tender? Unaweza ukatangaza tender ya investment ya mtu binafsi? Utaratibu gani huo. Soma tena hiyo page usijejikut nawe unajigonga mwenyewe.

Hujaelewa jinsi gani Tanesco wanavyojiingiza. Wao wametangaza ujenzi wa farms na specifications za expected outputs na hatimaye hizo ni farm za Tanesco. sasa unaleta mambo ya kiingereza gani wakati hata procedure tu zingeweza kukustua. Hizo ni farm za Tanesco, simple!
 
Nikifuatilia mjadala huu tena, wewe una matatizo ya aina mbili. Kwanza mambo ya mazingira na siasa za climate change ambazo ndo zinapelekea kuwekeana ngumu mambo ya emission, huyajui kabisa! Ila unadokoa dokoa. Pili unaonekana kuitetea Tanesco kama sehemu ya maisha yako. Nahisi uko Tanesco na sasa baada ya kuona upepo huu, unapotosha kwa makusudi maana halisi inayojadiliwa hapa, na mifano mingi ya Trump na muelekeo wa US gvt. US government hata bila Trump msimamo wake unaeleweka kwenye mambo ya energy.

Tangu enzi za Bush huo ndo mgogoro uliowafanya kugoma kukubaliana na Kyoto protocol. Wakati wote wameona ni gharama kupunguza emission wakati nyuma yao waliiona China ikiwa kundi la wanaoruhusiwa ku -emit bila kikwazo ikifanya hivyo kwa nguvu na uchumi kukua haraka sana! US na wenzao wengi wakaja na mambo ya CDM na carbon trading badaye tena wamekuja na mambo ya clean coal.

Nimeingia mtandaoni na kujionea tangazo la Tender ya Tanesco, laonesha ni tangu 2018 wakijieleza na mradi huo ili kufikia lengo lao la 2050. Kwa nini unageuza kuonesha kwamba eti ni investor binafsi? Waliotangaza ni Tanesco kampuni itakayojenga ni binafsi lakini pesa ni ya Tanesco! Acha kuvuruga mambo baadaye ujivune kwamba nimewaweza. Hakuna Kiingereza cha ajabu hapo. Ni tangazo la tender, basi! achana na kuleta mambo ya kiingereza hapa, hii siyo literature.

Soma maelezo ya mradi hapa:
Tanzania launches 150 MW solar tender
 
Ukiaza kuuliza watu ulichosoma darasani wakati unaelewa hilo siyo suala la chuo. ni kushindwa kuelewa maana ya JF, Ni sawa na yule mbunge-waziri aliyekuwa akiulizwa maswali yeye anaanza kutaja digrii alizonazo. Jadili na watu siyo kuleta maswali ya mitihani. Suppose unafahamu yote hayo na uko Tanesco na sasa unapotosha kwa makusudi, ukiulizwa unaanza kusema efficiency ya PV. Mtu kama wewe ndo mmekuwa kikwazo cha maendeleo kwa kuamini bila wewe nchi haitaeleweka.

Binafsi sihitaji kujua theory uliyosoma maana najua hujawahi gundua chochote. Ninachofahamu, solar energy bado technolojia haijaweza kushawishi nchi za dunia hii kuweza kuiamini na kutelekeza vyanzo vilivyozoeleka. Ni gharama kuliko vyanzo vingine. Mmekuja na hadithi ya clean energy na renewable, kwani hydro ni nini? kwa nini watupeleke kweye energy ambayo siyo ya kuaminika kwa kutumia pesa kibao kwa sifa za kijinga?

Kuna jambo limeelezwa humu kwamba tuko nyuma ya ulaya na US kwa karne 2 je, ulaya na US nchi gani inatumia hata 20% ya energy yake toka solar na wind? Kwa nini Tanesco ijiaminishe eti 2050 wako mbali? Nami naamini ni uharibifu wa pesa za nchi.
 

Umekosea kwa kuanza kwa kuwakejeli wanakijiji ambao ndio uti wa mgongo wa nchi yetu. Pili kwa kuwadharau wataalamu wetu wa Tanesco kwa kudai kuwa ni vilaza na malimbukeni ambao hawajui maana ya solar energy. Ungeweza kujenga hoja zako bila kuwakebehi wenzako lakini inaelekea ndio mtindo wa kisasa. Sasa hebu tuongelee hili suala la renewable energy ambalo umelivalia njuga:
1. Renewable energy haitokani tu na upepo na jua. Geothermal, biomass, mawimbi (tides) ya bahari n.k. vyote vinaweza kutumika kuzalisha nishati.
2. Renewable energy inaweza kuzalishwa katika scale yeyote ambayo mtu anataka, Kwa upande mmoja, huyo mwanakijiji unayembeza akitaka nishati kwa ajili ya taa ya kusome mtoto wake, kuchaji simu yake na kuangalia luninga anaweza kufunga panels za kumpatia umeme wa kumwezesha kufanya hivyo bila kungoja mradi wa serikali wa kumuunganisha kwenye grid ya taifa.Na wengine ambao wana umeme wa gridi lakini wamechoshwa na huduma zisizotabirika za huo umeme ( ambao kiasi kikubwa unatokana na Hydro) wanaamua kufunga solar system ambayo itamuondolea adha ya kukatika umeme mara kwa mara na wakati mwingine bila taarifa bila kelele zinazotokana na generators. Kwa scale ya miji au nchi, bado the jury is out. Tesla wamefanikiwa Hawaii lakini sio sana Puerto Rico. Kwa upande mwingine wachina wana zaidi ya Giga Watts 174 za Solar capacity. Lengo lao ni ifikapo 2050 watakuwa na Giga watts 1,300.
3. Hakuna mtu anaesema kuwa traditional sources zote za umeme zifungwe mara moja na tuhamie wote kwenye renewables. Lengo kubwa ni kudiversify na kuacha utegemezi wa traditional sources kama makaa ya mawe ambayo sio tu uungazaji wake unachafua mazingira lakini hata uchimbaji wake ni hatari na sehemu nyingi duniani unashindwa kushindana na vyanzo kama gesi asilia. Pamoja na mbwembwe zake Trump ameshindwa kufufua machimbo mengi ya Appalachian kwa sababu hayalipi. Hao wajerumani unaowabeza mwaka 2012 21.9 % ya umeme wao ulitokana na renewables, mwaka 2017 38%. Wakati huo huo matumizi ya makaa ya mawe yameshuka kwa 16%. Kwa mara ya kwanza, mwaka 2019 renewable sources zimetoa umeme zaidi ya wa nuklia na makaa ya mawe kwa pamoja. Merkel aliahidi kuwa Nuclear plants zote zitafungwa ifikapo Disemba 2022 na tayari mwaka 2016 walikuwa wameishafunga 9 kati ya 17.

4. Kuna dhana kuwa umeme wa hydro ni wa bei nafuu kuliko mwingine. Hii si kweli, hasa uki factor in gharama ya athari kwa mazingira, unpredictable nature yake n.k. Hapa kwetu, mojawapo ya vikwazo vikubwa kwa industrialization ni bei ya umeme wetu ambao kwa kiasi kikubwa ni wa hydro.

Ingawa natofautiana na wewe katika dhana yako ya kupigia debe Hydro na makaa ya mawe kama mkombozi wetu, nakubaliana nawe kuwa kuwekeza katika mradi mkubwa wa solar sio sahihi. Miradi midogo ya kati iliyotawanywa nchi nzima itakuwa more effective kwa vile tuna bahati jua linawaka kila sehemu ya nchi yetu. Aidha, serikali ingewawezesha wananchi kufua umeme wa renewable majumbani mwao, mashuleni n.k. kwa kupunguza gharama za uwekezaji kwa masharti kuwa umeme wa ziada wataweza kuwauzia Tanesco. Kwa kufanya hivi tutapunguza gharama za transmission na distribution. Ujerumani na nchi nyingine za magharibi zimefanya hivi kwa mafanikio makubwa. Vile vile viwanda ambavyo vinaweza kutengeneza umeme kutokana na process zao ( Cogeneration ) zipewe motisha wa kufanya hivyo. Kwa wenzetu ( Brazil, Mauritius n.k.) viwanda vingi vya sukari vinatumia bagasse wanayozalisha kuzalisha nishati kwa ajili ya shughuli zao. Umeme wa ziada unaweza kuuzwa kwa Tanesco ambao watawauzia wananchi.

Tunachohitaji hapa kwetu ni kuwa na sera ya ku diversify uzalishaji wetu wa umeme na kuondokana na source ambazo zinaweza kutuletea matatizo hapo baadae. Tungeweza kuwekeza katika umeme wa gesi asilia wakati tunaendelea na miradi ya vyanzo vingine vya umeme. Badala ya kutaka taasisi kama Tanesco kuhodhi uzalishaji wote wa umeme, serikali inatakiwa iwawezeshe wote wenye uwezo wa kuzalisha umeme (hata mdogo kiasi gani) kufanya hivyo ili kuipunguzia Tanesco mzigo.

Elon Musk sio mjinga kuwekeza katika solar. Hata wachina na wajerumani nao sio wajinga kuwekeza humo maana ndiko sote tunakoelekea. Kudhani kuwa mito ambayo kila mara inashindwa kujaza Kihansi, mtera n.k. itakuwa inajaza Stiegler kila mwaka ni kujidanganya.

Amandla......
 
Majivuno mengine musiyalete JF wakati yana makosa kibao! Kwa hiyo una masters. Hiyo masters ndo ulijiunza low Co2 emission badala ya low-carbon emission? Ukajifunza na mambo wanayoyasema ulaya na sasa unayaleta Tanesco? Hao waliokueleza hayo ulaya wao wameweza kufikia kiasi hicho cha kuachana na hydro na kuelekea kwenye solar. Mbona wako nuklia?

Hiyo ndo elimu ya mwafrika, alichokariri ulaya sasa anakileta Tanesco. Tueleze wewe unaonaje? Ni sahihi kuachana na hydro kuelekea solar? sababu ni zipi. usisimulie hadithi za masters. Duniani ktk low-carbon energy source ya kwanza ni hydro na pili ni nuklia, kwa nini munarukia solar?

Boss mazingira ni tofauti. Sisi hatuna mito inayoganda kuwa barafu, maji yanenda mwaka mzima. Hatuna winter storm! Uchumi wetu bado ni pesa za kuokoteza na hatuna muda wa kujaribia.
 
mambo ya wengi, mimi sikuelewa hivyo. Ila ukitaka tafsiri utakavyo utaharibu mjadala wetu. Naishi kjijini hata mimi nafahamu watu wanavyodanganywa kununua solar ambazo zingine ubora uko chini kupindukia. Ndo maana wengi tunaona REA ni mkombozi wa energy vijijini na siyo solar. No!
 
Upo makini sana boss,napenda watu wanaopitia uzi kwanza na kuulewa.Watu km nyny hata ukiweka comment mnashusha mondo za kweli.
 
Mleta Uzi nilimuomba aweke reference ya alichokiandika hapo juu,km ulifuatilia huu Uzi vizuri ,akaweka hii link
TANESCO LAUNCHES 150 MW SOLAR TENDER IN TANZANIA
Nakushauri soma vizuri ,maana unaposema kwmb Tanesco wanataka kuachana na hydro ina maana haukusoma hii link kabla ya kuchangia mjadala .Soma kiingereza ukishindwa tumia translator.
 
Mkuu
Umenena vyema hasa Katika kipengele cha elimu. Sisi waafrika tuna Shida Kweli ya kujimwambafai Katika hamna.
Mchangiaji, ingetosha Sana kwake kuweka ufahamu wake kuliko kukariri Mara kwa Mara kuwa Mimi nimesoma, Nina masters, nimeipata... Nina MTu marekani anayeniambia ....
Hii Ndio Shida yetu. Tunasoma lakini hatuelimiki. Ndio maana utaona watanzania wanapigwa Kweli ktk sekta nyingi huku tukiwa na hao wanaojiita wasomi.
Ukiangalia hata hizo solar zinazofubgwa majumbani, watu wanapigwa kwelikweli lakini Kuna wasomj wa kiwango cha masters ambao wameshindwa hata kutengeneza charger controller na matokeo yake wachina wanafanya kula kitu.
No wasomi wangapi wameweza kuunda hata mini HEP ya kuhudumia hata familia 50? Zaidi Sana ni kujadili dhana za kufikirika na hasa kwa lengo LA kujinufaisha wao binafsi.
 

Patriot, hivi kweli mwanakijiji wa leo anahitaji mwanga kwa ajili ya kuwafukuza wanyama peke yake? Huyu mwanakijiji wa leo hasomi, hana watoto wanaoenda shule, hana simu ya mkononi n.k.! Mimi naona hiyo ni sawa na Trump ambae anaamini kuwa waafrika wote tunaishi kwenye vibanda vya nyasi.

Kuhusu ubora wa vifaa vya solar na ufungaji wake hilo ni ishara ya udhaifu wa regulators na sio teknolojia yenyewe. Hivi sasa solar imekuwa cottage industry na kila mtu anajiuzia na kufunga bila usimamizi wowote. Sio watu wote wanaouza na kufunga solar systems wana ujuzi unaotakiwa. Lakini mbona hata simu nyingi tunauziwa ambazo hazidumu lakini hatuwezi kuitaka serikali izuie uuzaji wa simu za mkononi kwa sababu hiyo. Tunachokifanya ni kuzitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa simu zote zinazoingia kwenye soko ni za kiwango kinachotakiwa. Inakiwa iwe hivyo hivyo kwa hii biashara ya solar. Mimi binafsi nimewahi kuweka system ya solar kijijini na haikunisumbua.

Kitu kingine ni kutaka kuepuka gharama kwa kutumia mali duni. Kwa mfano, watu wanatumia betri za lead acid badala ya za lithium ion ambazo ni bei nafuu zaidi lakini hazidumu sana. Aidha, kuamini kuwa betri na solar system zitadumu milele bila maintenance. Betri za solar kama betri zozote zinapungua nguvu kila unapotumia na life span zake ni kati ya miaka mitano hadi 15.

Bahati mbaya wengi wetu ni conservative na huwa hatutaki kutumia vitu vipya. Wengi wetu bila kujali uwezo wetu bado tunaamini chakula kilichopikwa kwenye mkaa ( sijui kwa nini hatusemi kuni) ni kitamu kuliko kilichopikwa kwenye jiko la gesi au umeme. Inabidi tubadilike.

Amandla........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…