TANESCO: Arusha sasa ni rasmi mgao wa umeme?

TANESCO: Arusha sasa ni rasmi mgao wa umeme?

Muwa mtamu

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2020
Posts
847
Reaction score
1,599
Tanesco Arusha, je sasa ni rasmi mgao wa umeme?
Mbona hamjatangaza?

Ndugu wanaJF, ni takriban wiki 3 sasa Tanesco Arusha wanakata umeme kila siku kuanzia saa 3 asubuhi na unarudi jioni sana.

Maeneo mengi yanaathirika na kadhia hii hasa Meru na Arumeru kwa ujumla.

Na maeneo kadhaa ndani ya jiji la Arusha.

Jambo la kushangaza ni kuwa Tanesco mkoa wa Arusha hawajatangaza rasmi ili wananchi wachukue tahadhari au kupangilia kazi zao.

Kwa wajasiriamali wanaotegemea umeme kama salon za kike na kiume, stationery, wenye baa, welders nk wameathirika sana kwa kushindwa kufanya kazi zao ipasavyo.

Je, kwanini wasitangaze tu huu mgawo ili raia wajipange?

Tatizo nini hasa?
 
Back
Top Bottom