TANESCO board split on MD Rashidi's fate

 


- Mkulu Mag3, heshima mbele sana mkuu kwa kusimamia principle bila kuangalia nani anahusika, ambao ndio hasa msimamo wangu, sina ya kurudia maana umesayema yote tena kiroho mbaya, yaani kumkoma nyani style, ninaomba kukuombea kwa Mungu wangu wa Mbinguni akubariki zaidi,

- Tuendelee kusimamia ukweli bila kujali unamuhusu nani huko upande wa pili wa gilasi. Tupo pamoja sana mkuu mpaka kieleweke!

Respect.


FMEs!
 

Ni mambo ya intellectual jujitsu tu, nothing less nothing more, kama nimeenda overboard niwie radhi sometimes I tend to go overboard in the midst of mediocrity.

Principles mut prevail

Inawezekana kabisa Zitto kachemsha, inawezekana kabisa Zitto wa online ndiye mbunge.

At the very least, lazima ukubali waandishi wameboronga na wangeweza kuiandika habari hii vizuri zaidi.

Binafsi, hata kama sipendi kauli za Zitto, articles kama hizi naona zinaweka loopholes katika kum nail Zitto, wana squander opportunities. Mi najua (kwa mujibu wa uzoefu wa hapa na kwenyepress) Zitto si mtu wa kukataa position yake, jamaa anaonekana kuwa na conviction na audacity fulani, sasa kwa nini waandishi wale ng'ombe mzima na kushindwa kula mkia tu kwa kumpigia simu Zitto na kupata an airtight story?

Badala ya kufanya hivyo, wameacha room for debate on the authenticity of their story.

Ndiyo maana I cannot stand these little imbecile sea urchins passing themselves for reporters.
 
 
The simple facts of the matter ni kwamba waandishi wameandika habari kutokana na an undeniably unreliable source.

Sasa kama na wewe unataka kuwa katika mkumbo huo huo shauri yako. Basically husaidii kukuza level ya scritiny, ila unadidimiza standards.

Leo tunamquote Zitto hapa kesho itakuwa you know who.

Ni principles, precedents na policies, hatutaki politricks na propaganda.
 

Ulikuwepo humu wakati Zitto alipoleta muswada wake wa ethics hapa?

Unajua popularity aliyokuwa nayo Zitto wakati huo, kabla ya kuwa the so called "Mr. Dowans"? Practically the entire JF ilikuwa inamsupport.

Unajua nani ali dare kuuchambua huo mjadala point by point na kum criticize Zitto katika enzi ambayo hakuwa na mpinzani hapa JF? Unajua kwamba yours truly huyo huyo ndiye huyu anayedaiwa kutetea Zitto leo.

Tatizo ni kwamba ukiwa mwizi unaona kila mtu mwizi, ukiwa biased on partisan grounds, hata ukiji convince vipi kwamba uko neutral, unaona kila mtu yuko biased on partisan grounds.

Kwa tarifa tu, nilianza kumlima Zitto wakati Zitto alikuwa halimiki humu. Bef yangu ni hii standard ya uandishi wa habari, kama huwezi kuamini uandishi utaamini vipi kilichoandikwa?

Kwa hiyo usije hapa kusema kwamba watu wanamtetea Zitto, kabla hata hatujaenda nyuma sana huko kwenye muswada wa ethics ambapo probably hukukumbuki kwa sababu hukuwa member hapa, juzi tu Zitto kandika something about Salim nikamlima, kamuandika Kikwete in good light nikamlima kwamba hajawa firm kukataa ufisadi, brother Mukandara akaja kuniunga mkono, sasa utasemaje kwamba mtu anaye demonstrate objectivity kama hivi, kumcriticize Zitto inapostahili, na kucriticize uandishi mbaya (ambao kwenu Machiavellians mnaona ni kumtetea Zitto pale inapostrahili)

Acheni hii simplistic approach, kutaka labelling na simple answers to complex questions. Inabidi tuya address haya matatizo deply mpaka kwenye root zake, sio kuangalia mambo juu juu tu.Ama sivyo tutakuwa tunabadilisha majina na issues tu, lakini kila siku tutakuwa tunaogelea kwenye mitatizo ile ile huku tukiwapa sababu kina Nyani Ngabu kusema "Miafrika Ndivyo Ilivyo" over and over and over.
 


- Sawa sawa mkuu, umesikika sana.

Respect.


FMEs!
 

Bluray, I am honestly surprised with your level of contemporary news analysis.
 
Bluray, I am honestly surprised with your level of contemporary news analysis.


What surprises you?

You cannot have "news analysis" if you don't have news, this is what I am saying all along.

Get some news first, then we can analyse, otherwise ni propaganda, innuendos, he said he said.

You really think there is any analysis here?
 
Wakuu zangu,
Hizi habari zilizoandikwa hapa, huyo Zitto alizungumza lini na wapi?..
 
aliyeandika yupo humu humu ndio maana pamoja na kuwa anaongoza kwa posts hapa JF kwenye hili kakaa kimya akitumia majina mengine.inajulikana kuna watu wameajiriwa na Mengi kupambana na Zitto Kabwe.

wajuaji wala hatukushtuka kuona habari hii na kusingizia source ni JF wakati mwandishi ni mwanachama Mwandamizi hapa JF.kuna wakati alipomualika Zitto Huko Marekani.

Zitto nilikutahadharisha uwe makini na watu.
 
Wakuu zangu,
Hizi habari zilizoandikwa hapa, huyo Zitto alizungumza lini na wapi?..
Alikuwa akichangia humu JF kwenye thread ya 'Tanesco Board Split on MD Rashidi's Fate' iliyotokana na news story kwenye This Day/Kulikoni iliyohusu mchakato wa kumpata Boss mpya Tanesco. Zitto alimtetea Dr. Rashid as one of the best CEO's Tanzania has ever had. Thisgay/Kulikoni wakashuka nayo kama lead story kesho yake, Zitto akakasirika na kuamua kujinyamazia kwa kutochangia tena kwenye mijadala hapa JF.
 

Mkandara unaona mambo hayo mkuu wangu?

Unanielewa sasa?
 
Wakuu zangu,
Hizi habari zilizoandikwa hapa, huyo Zitto alizungumza lini na wapi?..

Zitto:

Pre-emptive strategy...........!

Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals.
__________________
“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa - TUJISAHIHISHE, Nyerere 1962.”
 
Zitto:-

1. Siasa...........! tungeacha mashirika yakawa na bodi huru na kuziwekea malengo na kuzipima kutokana na malengo mashirika haya yangeenda vizuri sana.

2. Siasa zinaingia sana na huyu Rashidi ni mmoja wa CEOs anayewakatalia wanasiasa waziwazi.

3. Wanamchukia sana. Mfano kawaambia Wizara walipe pango la jengo la TANESCO, wizara eti hawataki..... CCM nao wameng'ang'ania Rest House ya TANESCO dodoma, amewatimua. Wamekasirika.

4. Basi ni matatizo tu..... Sasa kwenye kampeni wanataka waweke CEO goigoi awape pesa maana Rashidi hatakubali na wao wameshazoea..... __________________



“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa - TUJISAHIHISHE, Nyerere 1962.”
 
Zitto:-

Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.

Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.

Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.

Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.

Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs.


Niendelee? _
_________________
“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa - TUJISAHIHISHE, Nyerere 1962.”
 
Mkandara unaona mambo hayo mkuu wangu?

Unanielewa sasa?
a
Blue Ray nimekukubali sana kwenye journalisim ethics na standards, Tanzania bado hatuna any cyber legistlation hivyo habari yoyote ya kwenye mtandao including sms haiwezi kutumika kama ushahidi mahakamani kwenye mambo ya admisability of evidence na ndivyo ilivyo kwenye uandishi wa habari, habari ile haikupaswa kutumiwa bila double checking na cross checking na Zitto mwenyewe hili ni kosa la kisheria kabisa and can land the editor behind bars.

Pili ni kosa la kimaadili, hata kama ni kweli kabisa yes ni Zitto kayasema hayo, aliyasema kuchangia kwenye mjadala according to freedom of expression akiwa free. Gazeti lilitakiwa kuheshimu his 'right to privacy' kwa anachochangia humu na kuitreet mijadala ya humu as 'off the record' unapotaka kuigeuza 'on the record' lazima umjulishe mhusika kuwa unadhamira ya kuyatumia maelezo yake for public consuption, akibali ndio unaitumia gazetini, vinginevyo ni hearsay na inabaki kuwa majungu.

Hata waandishi, wanapata habari nyingi tuu from various sources na sio kila kitu wanaandika, wanawajibu wa kutunza 'comfidentiality of the source' kama walivyofanya Kulikoni, Zitto is always reachable, it was a matter of contacting him kunjulisha we have this and that ulichosema jamiiforums, angekubali then its really news.

Kwa maoni yangu, habari hiyo imeandikwa na mwandishi kigogo wa Thisday/Kulikoni ambaye anauwezo wa kihariri kuithibitisha jamiiforums as a reliable source bila kuhitaji double checking na cross checking. Naungana na Zitto, habari hiyo imetumika kwa nia mbaya, kuonyesha Zitto ameingilia mchakato wa kumpata MD wa Tanesco, Zitto is only made victim ili kumdisqualify Rashidi katika mchakato mzima ili hata kama ni kweli ilikuwa Rashidi arudishwe kwa merits zake, sasa itabidi ang'olewe kwa vile mchakato umeingiliwa kwa kupigiwa chapuo na Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ambayo Tenesco ni subject.
 
Mkuu FMES,
Journalisim ni proffesional kama professional nyingine zote, ina rules of the game na ethics zake, tunachobishania hapa sio kama Zitto alisema ama hakusema, there is no doubt ni Zitto huyo huyo 'the one and only' kuhusu Zitto hapa hakuna haja ya kuleta hadithi za Sigmund Freud kwenye Dr. Jekely na Mr. Hide.

Tunabishania contex aliyoizungumzia Zitto ni kwenye forum na kuwa quoted bila idhini yake, hii sio maadili kwa upande wa Thisday/Kulikoni. Ni kama Zitto amechangia off the record wewe unakimbilia kubandika on the record, ni uungwani kumwambia nio yako, hii inapoteza uaminifu as a result, JF imeloose confidence ya Zitto, tutakosa michango yake.
 


- Mkuu Pasco, maneno yako ni mazito sana, lakini mnasahau kwamba sisi JF tunachojali ni hoja muhimu kwa taifa, mambo ya sheria za uandishi hzituhusu hapa, kutumiwa kwa habari hii kwa nia mbaya kama alivyosema mwenyewe Zitto hakuna uhusiano wowote na context za maneno ambacho ndio hasa interest yetu hapa JF,

- Nijuavyo ni kwamba viongozi wetu kuanzia ngazi za ubunge kama wa Zitto, wanakuwa on duty 24/7 chochote wanachosema to the public kama hapa JF tulivyo ni fair deal kuwa quoted, sikatai kwamba huenda kuna ethics za uandishi zimekiukwa, sasa hayo tuwaachie mahakama ndio iamue kwamba maneno ya Zitto hapa JF ni off the record, lakini sio members wa JF hapo na sisi sasa tunaingilia uhuru wa mawazo wa Zitto, ndio maana tuna mahakama sisi tunaweza kuichambua hukumu iliyotolewa na mahakama, lakini sasa tunaanza hata kuwa mawakili wa Zitto bila ya yeye kutuomba, pleasee!

- Ya sheria za uandishi wa habari hazituhusu wakuu!

Respect.


FMEs!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…