Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Kaka analysis nzuri sana.
Unawajua wazee wa data wetu hapa JF. Unadhani wana uwezo(capacity), haiba (caliber) ama mamlaka ya kimaadili (moral authority) kuachwa kuwa waamuzi wa mawazo ya wananchi na hata kutaka kutuamulia hatma ya nchi yetu?
omarilyas
Yes!
Huyo mwenye bold hapo juu ni mhandisi na amekuwa wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1984, anajua details kibao kuhusu wizara na Tanesco, na kwa sasa ni kamishna msaidizi wa nishati jadidifu (Renewable energy) pale wizarani.
Yahitaji ujasiri usio wa kawaida kuwatetea watu kama akina Rashidi - swali ninalobaki nikijiuliza ni huu ujasiri unajengeka katika misingi ipi. Kuna wakati huyu Rashidi alitishia kujiuzulu akitoa sababu za kuingiliwa na wanasiasa katika maamuzi. Lakini inavyoelekea hivi sasa, pamoja na mkataba wake kwisha, ni wazi bado anautaka uCEO wa TANESCO na kuna watu wanaendelea kumpigia debe - eti one of the best CEOs Tanzania ever had ! Jamani, halafu wanaomsifia Rashidi si ajabu ukawakuta ni wale wale wanaomsifia JK kama the best President Tanzania ever had ! Nachoka na Watanzania !
Kwa jinsi ninavyofahamu, Dr. Rashid angekuwa one of the best CEO kama ambavyo mnasema basi tungeona performance yake pale Tanesco. Uwezo wa mtu unapimwa na performance yake! Kama mnataka kumtetea kwa kusema eti anaingiliwa na bodi ya wakurugenzi, waziri husika, katibu mkuu na baadhi ya wakurugenzi wizara ya nishati na madini basi angejiuzuru mapema na huo ndio weledi duniani kote!!
Professionalism means meticulous adherence to undeviating courtesy, honesty, and responsibility in one's dealings, plus a level of excellence that goes over and above the commercial considerations and legal requirements. Professionalism is not about your job title or self-proclaimed worth. It is not about self-perception at all. Professionalism is about personal ethics, quality work and a quality attitude.
Na kama kuna mazingira ya watu kukushurutisha ufanye jambo ambalo ni kinyume na wewe unavyoamini, you resign!!
Hata kama Rais atakuomba urudi unampa masharti ya kurudi, akishindwa kukutekelezea you quit!!!
He is just another failure, period!!!!
Nimesema hoja ya Radar na hoja tofauti na sijaona hoja hii imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale TANESCO. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.
Zitto ampigia debe
Dk. Rashidi Tanesco
*Adai ni mtendaji makini, asiyeyumbishwa na wanasiasa
*Apuuza tuhuma zake za rada, ang'ang'ana tena na Dowans
MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
WAKATI kuk...........siasa kwa nini watu wengine wakitumia njia hiyo kumhukumu Dk. Idris unaona wanakosea?
SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009
embu muulize zitto alivyomshambulia Karamagi alikuwa amuhukumiwa na mahakama ganiTunapogeuza ufisadi ni mijadala ndio tunapoenda mrama. Mpaka sasa ni tuhuma na mahakama ikimtia hatiani hutaniona ninajenga hoja hizi. Lakini kama kuna ufisadi, au tuhuma za ufisadi akafanya TANESCO toka amekuwa CEO pale ziwekwe hapa na sio kutumia visingizio vya SFO kumhukumu mtu katika court za vijiweni.QUOTE][/COLOR]
Hivi Mh Zitto kwenye ile list yenu of shame mliyoitoa pale Mwembe Yanga wale watu walikuwa wameshahukumiwa na mahakama gani? Kama ni mahakama za kisiasa kawa nini watu wengine wakitumia njia hiyo kumhukumu Dr Idris unaona wanakosea? Halafu katika ripoti ya EPA ya auditors ambayo iko JF wakaguzi wanasema kwamba waliona barua ya Ruth Mollel kwa Gavana wa Benki ya mwaka 1997 (wakati huo akiwa Idris) ikitaka kujua status ya EPA ambayo haikujibiwa. Kitu kingine ni CIS ambayo pia inafanana na EPA ambayo ilitokea Dr Idris akiwa gavana na hiyo utakuwa unafahamu maana zaidi kuliko mimi maana nadhani kuna kamati iliundwa kuchunguza. Pia Idris alivyoondoka BoT alikwenda Akiba ambako hakukaa akaenda Vodacom ambako alishushwa cheo kutoka CEO mpaka Marketing Manager, wewe unatuambia kuwa the guy is the best CEO.
Inawezekana unatumia vigezo vingine na sisi, lakini kipimo cha utendaji siyo faidia tu ndugu Zitto, na inabidi uwe makini sana kwani faida inaweza kutengenezwa kwa kupunguza matumizi ambayo pengine yangekuwa muhimu katika utoaji huduma. Hivyo basi kipimo kingine zaidi ya vipimo vya fedha ungeangalia kama kiwango cha huduma na ubora wa huduma.
Ukiangalia utaoji huduma ya umeme hali imekuwa ile na bila ubora kuongezeka. Na kibaya tunapata mgao hata msimu wa mvua tofauti na zamani ambapo tulipata wakati wa kiangazi tu. Muheshimiwa Zitto unaweza kuwa unamwona jamaa ni mzuri na hata ukiongea naye unamwelewa lakini ni kwamba ukiangalia utoaji huduma jamaa hajaweza kufanya kile kitu ambacho ungetaka watu tuamini utetezi wako.
Eti Mwandishi wetu Dar!! Unajificha ficha unaogopa nini kuweka jina lako kama una uhakika na unachoandika?
Zitto ampigia debe
Dk. Rashidi Tanesco
*Adai ni mtendaji makini, asiyeyumbishwa na wanasiasa
*Apuuza tuhuma zake za rada, ang'ang'ana tena na Dowans
MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
WAKATI kukiwa na hisia ya kuwepo mtandao unaofanya jitihada za kuhakikisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), Dk. Idris Rashidi, anateuliwa tena kushika nafasi hiyo nyeti, Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, ameibuka hadharani kumpigia debe Rashidi katika mazingira yanayoongeza utata kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa mbunge huyo katika siku za karibuni.
Katika hali isiyotarajiwa, Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, amedai kuwa Dk. Rashidi ni mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika ya umma waliopo Tanzania, licha ya tuhuma zinazomwandama na utendaji wake ambao umewakera Watanzania wengi.
Zitto, ambaye alipachikwa jina la "Mr Dowans" na baadhi ya watu mapema mwaka huu baada ya kuchukua mtazamo wa aina yake wa kutetea mpango tata wa Dk. Rashidi wa kutaka kununua mitambo yenye kutu ya Dowans kwa bei kubwa kuliko hata waliyoitumia Richmond kuinunua awali, sasa amejitokeza na kudai kuwa kiongozi huyo ni lulu.
Kauli hiyo ya Zitto aliyoitoa kupitia mtandao wa mijadala wa Jamii, imekuja ikiwa ni baada ya gazeti hili kubainisha kuwa jina la Idris limepenyezwa Ikulu ili ateuliwe kuendelea na wadhifa huo, hali ambayo imesababisha mgawanyiko katika Bodi ya Tanesco ambako baadhi ya wajumbe wameukana uamuzi huo kuwa si wao.
................................................
SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009
wanaogopa visivyoogopesha, wanawadanganya waajili wao kua wanafanya uchunguzi wakina kumbe tunashinda nao humu jamviniina maana KULIKONI hawana jina la MWAANDISHI ? wanaogopa nini?
oili inamaaan hawa kulikoni hawawezi kuandika JAMIIFORUMS.COM
its about tgime wan JF mkahit back on these people