TANESCO board split on MD Rashidi's fate

TANESCO board split on MD Rashidi's fate

Zito kisha kapoteza mwelekeo siku nyingi ninyi hamjui tu. kisha nunuliwa, hana kauli yake tena. Msimamo wote umeyeyuka.

utumbo mwingine huo!

kwa hiyo na mimi nikisema RWECHU ni fisadi then watu wataniamini?

Mkuu ukiweka vithibitisho havitaisaidia JF tu, ila vitaongeza heshima yako wewe! maana mawazo yako hayana tofauti na ya mtaani , na kwa tabia hii CCM haitatoka madarakani mkuu, kwa nini umejiingiza kwenye kundi la wapumbavu! wewe sio mmoja wapo, story za vijiweni hazitusaidii

Just imagine wewe ndio Zito na mtu kaandika ulivyoandika wewe na pengine ni completely false.Ikiwa kweli ukatuhabarisha tutapona wengi!

Rwechu huyu sio wewe usiige wengine, wameshajichokea
 
Gazeti la Rostam Aziz (Mtanzania), leo limeandika habari inayofanana kimaudhui na hoja ya Zitto kuwa ukiwauliza wafanyakazi wa Tanesco watakwambia kuwa Rashidi ni one of the best CEOs of our parastatals. Ikumbukwe pia kuwa Zitto alitetea mpango dhalimu wa kununua mitambo iliyotumika ya Dowans. Pia Zitto huyu huyu alishabihiana tena kimawazo na Rostam pale alipo tamka kuwa Richmond ichunguzwe upya na jopo la majaji, which is unconstitutional kwani one pillar of the state (judiciary) haiwezi kufufua upya jambo lililo amuliwa na another pillar (legislature). Leo hii Zitto ameibuka tena na kumtetea hadharani Rashidi eti ni kiongozi bora zaidi.

Swali ninalo jiuliza, Je Rostam Aziz na Zitto ni wabia? Au it's just a coincidence tu kuwa wana mawazo ya kufanana kwenye maswala nyeti, eg Dowans, Richmond na hatma ya Rashidi?
 
Good analogy Tina, somebody said...BIRDS OF THE SAME FEATHERS FLY TOGETHER?... or are we dreaming!!!
 
Jamii forum inatakiwa kuwa na taratibu zake sio hizi za kukopy na kupaste ambazo zinatumika dunia nzima haswa zinazohusu mtu anapoamua kuchukuwa habari ya humu kwenda kutumia kwenye chombo chake na mambo yake mengine -- hata hivyo wanavyomnukuu zitto inawezekana wana uhakika wa asilimia 100 huyu ni zitto mwenyewe -- kwamba hata mimi kesho nikija na jina jipya nikajiita zuberi zitto nitakuwa ni yule yule mbunge -- tuwe makini sana na mambo haya
 
Zitto
Maoni yako mazuri lakini yanafaa darasani na majamvini kama humu tu. Uko kwetu Uswazi hayafai. Dr. Rashidi hawezi kuwa CEO bora unless analinganishwa na ma CEO wachovu. Hakuna nchi yenye ambako ili mtu apawe huduma ya umeme inabidi:-
-Abembeleze power company badala ya kampuni kumbembeleza ili afanye nayo biashara
-Mteja anunue nguzo ya umeme wakati atalipa bill ya umeme
-Mteja atoe rushwa ili apate huduma ya umeme
-Mteja apate hasara ya kuunguziwa vifaa vyake na umeme, akilalamika akatiwe umeme
-CEO atumie milioni 60 kuweka maua na mamazia nyumbani kwake wakati kuna mgawo wa umeme nchi nzima, n.k

Ubora wa CEO huyo uko wapi Zitto? You are not playing devil's advocate, you are blaspheming the public service.

Hapa umenena. Tuangalie ufanisi wa kiongozi kwa jinsi anavyotatua matatizo na sio kutuongezea matatizo.
 
Huyu jamaa kisha poteza mwelekeo, kishakula hela za watu hana tena uhuru wa kusema mambo yake. Misimamo yote kwisha.

Pole sana rwechu kumbe ulikuwa hujui kuwa kauli kama hizi zingeweza kukubaliwa hapa JF kama unge mkoment SS au serukamba ambao tunadhani wao tu ndio wanaweza kununuliwa! hujajua kuwa objectivity ni ishu jamvini tehe tehe tehe

We do not see things as they are: We see things as we are
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto
Kauli hii ya Zitto inanikumbusha msemo maarufu utuatao....

“Since a politician never believes what he says, he is quite surprised to be taken at his word.” Charles De Gaulle (1890 – 1970), a French general and statesman
 
Gazeti la Rostam Aziz (Mtanzania), leo limeandika habari inayofanana kimaudhui na hoja ya Zitto kuwa ukiwauliza wafanyakazi wa Tanesco watakwambia kuwa Rashidi ni one of the best CEOs of our parastatals. Je Rostam Aziz na Zitto ni wabia? Au it's just a coincidence tu kuwa wana mawazo ya kufanana kwenye maswala nyeti, eg Dowans, Richmond na hatma ya Rashidi?
Aisee ni wabia hawa, zipo dalili, namuheshimu Zito lakini mwenendo wake unatia mashaka sana.
 
Tumeshindwa kukutumia mh., pia hakuna anayejali unaathirika vipi kisaikolojia kwa haya maneno. Mimi nakubaliana na wewe after all tuna wabunge wengi sana kama 300 hawaonekani humu, tunayekuona tunakupiga mawe humu humu na watu wanalisha watoto wao kwa kuuza magazeti,watu wanasema bila vithibitisho.Hakuna anayejiweka nafsi yako aone unajisikia vipi.Yet tunalilia mabadiliko wakati wapiganaji tunawapiga kabali

Hii dhambi na tabia hii imerudisha nyuma wengi, siasa kwa vijana Tz ni ndoto, watu watabaki kuwa wenyeviti wa kipaimara na harusi za ijumaa na jumamosi kwisha!

Inaboa sana, wazo lako zuri litakusaidia mkuu! tunakujali mkuu!
Kamanda, umesema yote! Kuwepo kwa Mh. Zitto hapa kuliwezesha mijadala mingi kusikia na upande wa system upo vipi na unasimama vipi kwa hoja mbalimbali ambazo Mh. alishiriki.

Nina uhakika Mh. Zitto alifanya hivyo kwa moyo mkunjufu pasipo shaka kwamba baadhi ya watu wataweza kumnukuu vibaya kwa malengo yao binafsi. Kama ulivyosema kuhusu siasa na Tanzania, inaonekana ni wazi kwamba tupo mbali sana na ukweli halisi wa tekinologia.

Leo hii ni rahisi kujua Rais wa Marekani ana tekeleza vipi majukumu yake, na hii ni kupitia FB, na mpaka sasa hayo magazeti makubwa ulimwenguni hayamnukuu vibaya ama kupotosha kile anachoandika.

Ni jukumu la Waandishi wetu kuheshimu mipaka ya kazi zao, ilikuwa ni rahisi kwao kusoma hapa JF msimamo wa Mh.Zitto, na kumuuliza pale waliposhindwa kuelewa alichokuwa akimaanisha badala ya kukimbilia kuchapisha magazeti yao kwa uelewa wao.

Tekinologia hii isiwafanye wawe wavivu wa kufanya kazi zao kwa mujibu wa maadili ya uandishi.
 
Huyu jamaa kisha poteza mwelekeo, kishakula hela za watu hana tena uhuru wa kusema mambo yake. Misimamo yote kwisha.

Jamaa gani huyo unzayemzungumzia? anaitwa RWECHU?
 
Tanzania hata aje CEO wa kutoka Ulaya kama siasa haitajitenga na uendeshaji wa mashirika hatutafika popote ndugu zangu
 
Pole Mh. Zitto, nadhani tuendelee na huo mjadala kwenye hiyo hiyo thread ya Tanesco, No. #94 & #97 ulikuwa hujatujibu, ukipata nafasi basi pitia, ulisema uko kwenye mkutano.

Nakushauri ukiona vinginevyo badilisha jina lako hiyo inasaidia saana, humu kuna members kazi yao ni kuchunguza mienendo ya kila member mmoja mmoja nan nini anachangia.
 
mwandoshi wa makala hii toka gazeti la kulikoni yumo hmu janvini na huwa hachangii mada, kzi yake ni kuandika maoni ya watu kisha kupleka gazetini, na hawa kulikoni huwa hawana jipya habari zao zote 97% huwa zinatoka hku janvini then wanasema ''uchanbuzi wa kina''
 
utumbo mwingine huo!

kwa hiyo na mimi nikisema RWECHU ni fisadi then watu wataniamini?

Mkuu ukiweka vithibitisho havitaisaidia JF tu, ila vitaongeza heshima yako wewe! maana mawazo yako hayana tofauti na ya mtaani , na kwa tabia hii CCM haitatoka madarakani mkuu, kwa nini umejiingiza kwenye kundi la wapumbavu! wewe sio mmoja wapo, story za vijiweni hazitusaidii

Just imagine wewe ndio Zito na mtu kaandika ulivyoandika wewe na pengine ni completely false.Ikiwa kweli ukatuhabarisha tutapona wengi!

Rwechu huyu sio wewe usiige wengine, wameshajichokea

Hivi ndugu yangu waberoya unadhani mtu aliyenunuliwa anakuwaje? Usimuamini mtu kupita kiasi, yeye ni mwanadamu anaweza shawishika. Soma alama za nyakati, tambua zito alikuwaje, yukoje na baada ya muda imagine atakuwaje!
 
mwandoshi wa makala hii toka gazeti la kulikoni yumo hmu janvini na huwa hachangii mada, kzi yake ni kuandika maoni ya watu kisha kupleka gazetini, na hawa kulikoni huwa hawana jipya habari zao zote 97% huwa zinatoka hku janvini then wanasema ''uchanbuzi wa kina''

Unajua hakuna mahali penye uchambuzi wa kina kama humu, kwasababu tupo huru na majina hayajulikani, kwa wenye akili ni nafasi ya kutoa maoni yako huru.

Kwahiyo kulikoni wapo sahihi.
 
Ndg. Kibunango, Je ni meneno gani ambayo gazeti limemnukuu vibaya Zitto? Tuwe makini na sweeping statements, mimi nimefuatilia kwa makini mjadala wa JF kuhusu Dk. Rashidi. Kulikoni imenukuu verbatim (neno kwa neno) michango aliyoitoa Zitto kwenye JF. Naomba upitie habari ya Kulikoni kwa makini utuonyeshe ni maneno gani Zitto amekuwa misquoted. Ni vizuri tukajenga hoja kwa facts kuliko kutoa sweeping statements.
 
Pre-emptive strategy...........!

Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals.

nakubaliana kabisa na Zitto. nilibahatika kufanya nae tanesco kabla sijaondoka kwa kweli unaweza kuona improvement toka alipoingia. kazi aliyoifanya ni kubwa sana. Collection kwa mwezi imepanda sana.
 
Mwandishi ameishiwa. hana maana.

Jamani lazima tukumbuke Zitto ni mtanzania kama wananchi wengine. na vile vile tunatakiwa tujuwe Zitto hayupo juu ya sheria za nchi. Yeye anao uhuru wa kutoa maazo yake kama mtanzania yoyote ili mradi tu asivunje sheria za nchi.

Kwa hakika hata mimi na kwa ninavyomfahamu Dr Idriss siwezi amini kabisa kama aneeza fanya mabaya dhidi ya Tanesco. Hata vyombo vyenu vya habari vya huko vimesema wazi kuwa Dr anapendwa sana na wafanyakazi wa chini na anachukiwa na mameneja. Sababu kuu ni kuwapunguzia posho zao walizojiwekea na kuwalipa wafanyakazi wa kawaida.

nakuunga mkono Zitto kwa kuona wazi juhudi na kazi zote na maamuzi sahihi ya Dr Idrissa.

Tuache siasa kwenye kitu cha kitaalamu.
Mkuu kupendwa na wafanyakazi wa chini siyo jambo baya,but perfomance is what matters,kwa hiyo unataka kuniambia hao wanabodi,wanasiasa,Dr Idrissa na wafanyakazi wa chini wako kambi moja,na hiyo kambi nyingine hatuijui,ama ndiyo hiyo waliyoko hao "mameneja?' Mh Zitto keshasema kuwa "kuna wanasiasa" wako behind some few applicants ambao anadai "wameline up" Sasa kwani Dr Idrissa hana wanasiasa ambao wako nyuma yake?Mh Zitto yeye si mwansiasa?Rostama Aziz,Lowassa ambao wanahusishwa na Richmond/Dowans si wanasiasa?Hao na Dr Idrissa pamoja na Zitto hawataki mitambo inunuliwe?

Kusema unataka siasa iondolewe sasa ni sawa na kutaka issue yote ife kwasababu ufisadi wote huo uliwekwa peupe kupitia wanasiasa....Issue ishughulikiwe step by step,yani ufisadi uliofanyika,then kuhakikisha kuwa wanasiasa hawana maslahi binafsi yanayoweza kuhujumu maamuzi yenye maslahi ya Taifa.

Hata hivyo jambo moja liko wazi,kuna kambi moja yenye kutaka mitambo inunuliwe,certainly kuna isiyokubaliana,mjadala uendelee na huku tukikumbuka kuwa mojawapo ya issue inayovisumbua vichwa vya wananchi walio wengi ni ununuzi wa mitambo hiyo...Na hao wanasiasa wengine ambao wanasemekana wameweka watu wao wanaotaka wapewe nafasi hiyo waje open na watueleze nia yao haswa nini?Hatuwezi tu kusikiliza upande unaosema siasa zisiwepo na wakati siasa tayari zipo,wajitokeze na wao watuambie kwanini hawataki mitambo hiyo inunuliwe na what is the solution,wananchi tayari wanajua hili na kwahivyo sioni kwanini wasishirikishwe....Facts ziwekwe wazi wananchi wajadili tutajuwa whats good for the people and whats good for the interests of our nation.
 
Zitto ametoa mawazo yake kwamba idris ni mchapa kazi...yeye ni sawa na wengine wanaosema idris hafai...embu sasa tu-judge watu kwa data siyo hisia tu...
 
Ndg. Kibunango, Je ni meneno gani ambayo gazeti limemnukuu vibaya Zitto? Tuwe makini na sweeping statements, mimi nimefuatilia kwa makini mjadala wa JF kuhusu Dk. Rashidi. Kulikoni imenukuu verbatim (neno kwa neno) michango aliyoitoa Zitto kwenye JF. Naomba upitie habari ya Kulikoni kwa makini utuonyeshe ni maneno gani Zitto amekuwa misquoted. Ni vizuri tukajenga hoja kwa facts kuliko kutoa sweeping statements.
Jumuisho la yote kwa mwandishi wa habari hiyo ni kwamba Mh. Zitto anampiga debe Dr. Rashid ilhali Mh. ametoa ufahamu wake juu ya utendaji kazi wa Dk. Rashid.

Huu ni upotoshaji wa wazi waliofanya KULIKONI, kumbuka kwamba Mh. Zitto alikuwa akijibu hoja za baadhi ya wajumbe waliokebehi utendaji wa kazi wa Dr. na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom