TANESCO: Gridi ya Taifa yapata hitilafu. Umeme wakatika nchi nzima - Juni 27, 2026

TANESCO: Gridi ya Taifa yapata hitilafu. Umeme wakatika nchi nzima - Juni 27, 2026

Uvccm hawaonekani hapa... Ndio wapo kwenye ufundi wa umeme🤣🤣... Ccm bana!! Lile jamaa la zimbabwe sio linapakia wanaya kutoka mbuga zetu kweli?.... Hitilafu gani itokee usiku aseeee...
Kuna mission inaendelea? Na leo pillika pillika za humu haikuwa coincidence
 
Nchi ina mikosi hii
Mkuu,nchi hii haina mikosi hata kidogo, ukitaka kuamini maneno yangu sikiliza yowe la shangwe (huoooo...) pale watakapo washa umeme. Ungesema nchi hii imefuga mazuzu labda ningekubaliana na wewe maana hatuijui haki yetu
 
Ingekuwa ulaya mkurugenzi wa TANESCO kuanzia jumatatu angejiuzulu au kutenguliwa, maana huu ni uzembe umeme kukatika nchi nzima namna hii
 
Waungwana je huko kwenu kuna umeme? wapi ulipo?

Maana sisi maeneo ya Ilala, Sinza, Dodoma, Tarime kote ripoti ni hakuna umeme,

Nini itakua sababu?

=====

TANESCO wanasema hivi:

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuwa leo, tarehe 27 Juni 2026, majira ya saa 01:00 usiku, kumetokea hitilafu ya kiufundi katika Mfumo wa Gridi ya umeme ya Taifa, hali iliyosababisha mikoa yote inayopata huduma ya umeme kupitia Gridi ya Taifa kukosa huduma hiyo.

Wataalamu wetu wanandelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme kwa awamu katika maeneo yaliyoathirika.

Soma Pia: TANESCO: Kuna hitilafu kwenye gridi ya taifa iliyosababisha kukosekana kwa umeme

Shirika linawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na linawashukuru kwa uvumilivu wao wakati jitihada za kurejesha huduma zikiendelea.

Hahaha kama kawaida yetu na nchi yetu hapo Hadi wakaitwe watu wengine
 
Vyanzo vya umeme vipo vingi tu. Ajabu wanakomaa na chanzo hichp hicho cha maji miaka yote.

CCM michosho sana.
Ni grid mzee!! Grid huwa inacombine vyanzo vingivingi Jua,HEP,umeme wa zile wind turbine,mbolea na chochote kile kinachozalisha umeme..kwahiyo kilichozingua hapo ni mfumo katika Grid ya taifa na sio chanzo
 
Ni grid mzee!! Grid huwa inacombine vyanzo vingivingi Jua,HEP,umeme wa zile wind turbine,mbolea na chochote kile kinachozalisha umeme..kwahiyo kilichozingua hapo ni mfumo katika Grid ya taifa na sio chanzo
Maana yangu ilikuwa tuwe navyanzo tofauti vya umeme vinavyojitegemea.
 
Back
Top Bottom