TANESCO: Gridi ya Taifa yapata hitilafu. Umeme wakatika nchi nzima - Juni 27, 2026

TANESCO: Gridi ya Taifa yapata hitilafu. Umeme wakatika nchi nzima - Juni 27, 2026

Waungwana je huko kwenu kuna umeme? wapi ulipo?

Maana sisi maeneo ya Ilala, Sinza, Dodoma, Tarime kote ripoti ni hakuna umeme,

Nini itakua sababu?

=====

TANESCO wanasema hivi:

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuwa leo, tarehe 27 Juni 2026, majira ya saa 01:00 usiku, kumetokea hitilafu ya kiufundi katika Mfumo wa Gridi ya umeme ya Taifa, hali iliyosababisha mikoa yote inayopata huduma ya umeme kupitia Gridi ya Taifa kukosa huduma hiyo.

Wataalamu wetu wanandelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme kwa awamu katika maeneo yaliyoathirika.

Soma Pia: TANESCO: Kuna hitilafu kwenye gridi ya taifa iliyosababisha kukosekana kwa umeme

Shirika linawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na linawashukuru kwa uvumilivu wao wakati jitihada za kurejesha huduma zikiendelea.

Dodoma hakuna umeme
 
Back
Top Bottom