Cod-2
JF-Expert Member
- Jun 11, 2017
- 297
- 434
Hpana mkuu ili siyo la kweli. Wateja waliolipia elfu 27 wanaunganishiwa vizuri tu . Tena hapa Bagamoyo, sema kunaucheleweshaji kidogo sababu ya uchache wa vifaa.Wakuu Kuna tetesi nilisikia kuwa Tanesco hawataki kuwaunganishia umeme wateja wale waliolipia elfu ishirini na Saba (27000) , eti kisa haikuwa Bei yenye uhalisia.
Wakati nakumbuka hata Rais wakati yupo maeneo ya pale tegeta akiwa kwenye msafara wa kuelekea kaskazini, alisamama nakueleza kuwa serikali inawajali wananchi, na ndiomaana imewapunguzia Bei ya kuunganishiwa umeme, Sasa wanasemaje Ni Bei ambayo haikuwa kwenye uhalisia,inamaana wakati wanaipitisha walilazimishwa na wananchi au Ni wao wenyewe tu walihamua kwa utashi wao?
Huu Kama nikweli ni uhuni kabisa, na saizi nilikuwa namsikiliza mzungumzaji wa Tanesco alikuwa anahojiwa na Kipindi Cha Asubui Cha ITV, akisema eti zile Bei hazikuwa halisi, Sasa sisi zinatuhusu Nini. Mimi nilijenga nyumba yangu, Nikakamilisha kila kitu, na nikaenda Tanesco kutaka umeme, wakanipa bei yao halisi nikalipia. Bei ambayo walipanga wao sio Mimi mteja, na hata ingekuwa milioni inamaana ningelipia tu Kama mteja, maana nisingekuwa na namna,
Sasa hii mshachukua hela za watu, na mshakaa nazo karibia miezi minne Hadi sita, Wengine na hela zenyewe tushamaliza katika ujenzi, leo unamtuambia habari za Bei haikuwa halisi, hiyo Bei mlifosiwa kwani au.
Mimi Kuna bi mkubwa wetu amelipia umeme tangu mwezi wa kumi ni maajabu haya
Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app