TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Voda wakikopesha 5,000/= baada ya siku nne mtu anakopa tena Tigo 2,000/= atahama huko na kukopa tena Airtel au Halotel.

Sasa ukikopa LUKU directly kwa kuandika number ya mita, ni ngumu kwa mtu kuweza kukopa zaidi ya mara moja.
Saaaaf sana
 
Ukopeshe watanzania hawa hawa waliofanya TALA akabeba virago vyake, Africa mambo ya postpaid bado sana sisi hata matundu ya vyoo shida
Usijishushe kihivyo boss, au Kama Ni kujishusha sio kwa wingi kiasi unachotaka kuaminisha watu.
Mimi binafsi Ni mteja wa branch inayohusika na kukopesha fedha nilianza na elfu 20 na Sasa naweza kukopa Hadi laki 5 na kuresha bila ya shida. Na wapo wateja wengi qa namna yangu huko.
Hao tala waliondoka kwa mambo yao.
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Kwanini TANESCO haikopeshi units za umeme wa LUKU kwa wateja wake? Mimi ninaona kama mchakato huu utawawezesha kupata faida kubwa sana kama riba kwa maana ni ngumu sana kwa mteja kukwepa marejesho.

Tofauti ya mteja wa TANESCO na mteja wa mtandao wa simu za mikononi kama Vodacom na Tigo ni kwamba, mteja wa mitandao hii ana nafasi kubwa sana ya kutokulipa deni kwa maana anaweza kubadili simcard au anaweza kufa kisha deni likawa limepotea tofauti na mteja wa TANESCO ambaye deni linakuwa limebebwa na nyumba kiasi kwamba hata akifa, deni litakatwa wakati wa ku-transfer property ownership.

Mteja wa mitandao ya simu za mikononi anaweza akakopa Vodacom kisha akahama mtandao akaanza kutumia Tigo, lakini mteja wa TANESCO hawezi kubadili number yake ya mita ya LUKU. Kama alikopa umeme wa 20,000/= kwa kutumia M-PESA inakuwa ngumu sana kukopa tena kwa kutumia mtandao mwingine kama vile TIGO PESA kwa maana atatumia number ile ile ya mita hivyo computer system itakataa kufanya muamala wa kumpa units.

TANESCO wanaweza kufanya special arrangement na kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahususi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote. Ukitumia pesa hiyo kwa muamala mwingine inakataa.

Mathalana TANESCO wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.

Wataalam wa masuala ya uchumi pamoja na ICT mnaweza kulifafanua hili zaidi kwa maana hiyo sio taaluma yangu lakini ninapendekeza number itakayoruhusiwa kukopa iwe moja tu (Mmiliki wa nyumba) hususan kwa nyumba zenye wakazi (wapangaji) wengi

NB: Ndugu zangu waislam, Mungu awatangulie na kuwasimamia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Siku zote 30 za mfungo zikawe za kheri na baraka kwenu. Wishing you courage and strength so that you win every challenge of this life.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Good idea
 
Waweke mfumo wa vocha za kununua luku yaani unaingiza direct kwenye simu umeme unajiconnect.
 
Tanasco hawazalishi umeme "produce" anasambaza "supply".
Yeye pia ananunua huo umeme kutoka kwa wazalishaji.
Pili, Tanesco ili akopeshe umeme lazima awekeze hela ya kununua umeme toka kwa mzalishaji kwa minajiri ya mkopo tuu. Yaani kutakuwa na mtaji wa kuendesha mkopo wa umeme. Unaposikia Mpawa au Songesha katika mitandao ya pesa ujue ile ni "separate legal entity" yenye mandate ya kukopesha. Mara nyingi Kampuni za simu huwapa hilo deal mabenki.
Tatu,kwa kufanya hivyo inabidi Tanesco walipe kodi ya mapato yatakayotokana na mikopo ya umeme kwa muda fulani kitu hivyo hicho unachowaza kwamba ni "faida kubwa" haitakuwepo pesa nyingi italipa kodi (VAT na nyinginezo) na gharama za uendeshaji.
Nne,timing ya kumlipa mzalishaji itakuwa disrupted na mikopo ya umeme. Tanesco ili amlipe umeme mzalishaji lazima auuze. Fuatilia uendeshaji wa hili shirika ndio utajua kwanini selikali ime-monopolize huduma ya umeme. Kwanini hakuna soko huria la umeme. Yani kila mti azalishe na asambaze.
 
Tanasco hawazalishi umeme "produce" anasambaza "supply".
Yeye pia ananunua huo umeme kutoka kwa wazalishaji.
Sisi wateja tunawajua TANESCO ndio anatuuzia umeme hao wengine sio kazi yetu sisi kuwajua. Lakini asante kwa taarifa.
 
Pili, Tanesco ili akopeshe umeme lazima awekeze hela ya kununua umeme toka kwa mzalishaji kwa minajiri ya mkopo tuu. Yaani kutakuwa na mtaji wa kuendesha mkopo wa umeme. Unaposikia Mpawa au Songesha katika mitandao ya pesa ujue ile ni "separate legal entity" yenye mandate ya kukopesha. Mara nyingi Kampuni za simu huwapa hilo deal mabenki.
Sioni tatizo lolote juu ya hili kama lina manufaa kwa taifa. Watanzania wanakopa kutoka TANESCO na yeye (TANESCO) anakopa kutoka huko anaponunua.

Kwani hayo makampuni ya mitandao ya simu yanayokopesha watu data wao ni main (ISP) suppliers?
 
Back
Top Bottom