TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Mteja akikopa kupitia labda tigo pesa alafu akahamia mtandao mwengine bila kulipa Deni lake la tigo pesa ni sawasawa na mpangaji akope units alafu ahamie nyumba nyingine akiacha Deni la units alipotoka
Hapo mpangaji anakua anamuachia mzigo mwenye nyumba
 
Kwa hiyo leo unapanga nyumba "A" kisha baada ya muda kidogo unahama na kwenda nyumba "B" kisa TANESCO wanakudai 3,000/= ya mkopo wa umeme?
 
Mtu anahama baada ya mkataba wa pango kuisha ila anafukuzwa kabla ya mkataba kuisha. Huo ndio utofauti.
mkuu kila mpangaji anajua mkataba wake unaisha lini,so kama hana mpango wa kuongeza mkataba wake ni rahisi kukopa units kwa ule mda atakao kaa kabla ya kuhama akijua kabisa hizo units zitamfikisha mpaka siku atakayo ondoka
 
Hii itaongeza mzigo kwa TANESCO , mitandao ya Simu tayari ina huduma za kukukopesha fedha kulingana na Mwenendo wako wa Miamala ya Kifedha Kwa mfano Vodacom wana huduma ya Songesha unaweza kutumia huduma hiyo kukopa fedha ya kununua luku na Kiasi cha fedha hii utapatiwa kulingana na Mwenendo wako wa matumizi ya huduma za kifedha, baada ya hapo mtandao husika wa Simu uta 'deal' na wewe moja kwa moja.
 
mitandao ya Simu tayari ina huduma za kukukopesha fedha kulingana na Mwenendo wako wa Miamala ya Kifedha Kwa mfano Vodacom wana huduma ya Songesha
Vp sasa baada ya kukopa akihama kutoka Vodacom kisha akakopa na Tigo pamoja na Airtel, mtawezaje kumdhibiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…