TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Kwanin wakopeshe? Sio kila huduma itolewe kwa mkopo
Wabongo kwenye mikopo sio waaminifu kabisa.

Ibakie hivi hivi kama huna pesa ulale gizani tu ili upate akili vizuri.
 
Kukopesha umeme ni suala gumu ndiyo maana hata ww haujatoa ni njia gani watatumia kukopesha unit ila umeandika wawe wanakopesha.
Mimi nimewapa hints tu, sasa kazi ni kwa wataalam wa uchumi na ICT kukaa na kuona wanaweza vp kutekeleza hilo.

Wanaweza kufanya arrangement ana kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahsusi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote.
 
Kwanin wakopeshe? Sio kila huduma itolewe kwa mkopo
Wabongo kwenye mikopo sio waaminifu kabisa.
Mbona serikali inakopa? Mbona wapo watanzania wanalipa madeni yao ya bank kwa mikopo bila shurti za mahakama?
 
Ni ngumu na italeta migogoro sana. Fikiria umepangishwa nyumba halafu kuna deni la 40,000 halijalipwa. Hiyo hela anatoa nani?
Hakuna umeme wa dharura wa 40,000/= huu ni uongo. Mikopo ya dharura katika simu haizidi 20,000/= na kiwango hupanda kulingana na uaminifu wa mteja husika.
 
Ibakie hivi hivi kama huna pesa ulale gizani tu ili upate akili vizuri.
Maisha hayaenda kama unavyofikiria ndio maana waliojenga mabondeni kama pale Jangwani wakikumbwa na mafuriko serikali inawaokoa ingawa walifanya kosa kutohamia mabwepande walipopewa viwanja.
 
Mkuu mbona ni simpo tu, mathalana tanesco wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.
 
Mkuu mbona ni simpo tu, mathalana tanesco wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.
Mkuu, huyo jamaa ana PhD ya ubishi sijapata kuona
 
Ukopeshe watanzania hawa hawa waliofanya TALA akabeba virago vyake, Africa mambo ya postpaid bado sana sisi hata matundu ya vyoo shida
 
Kuna meneja mmoja wa tanesco nilikua naongea nae akaniambia shirika linaenda kufa...coz cost of production n kubwa kuliko mapato.
Alikupa maelezo na ufafanuzi wa kutosha ukijiridhisha? Au umekurupuka tu baada ya yeye kukwambia hivyo? Maana ulitakiwa umuulize vizuri upate maelezo yanayojitosheleza kabla ya kuweka comment yako humu!
 
Msamehe bure tu huyo mkuu
 
Nunua umeme tu mdogo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…