TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

ina tofauti gani na wanachofanya kampuni za simu tayari kama Vodacom wana songesha ambapo wanaweza kukukopesha ukanunua salio? Wangefanya hii idea miaka kumi iliyopita ingekuwa sawa, kwa sasa washachelewa labda waweke viwango vya riba vya chini sana
 
ina tofauti gani na wanachofanya kampuni za simu tayari kama Vodacom wana songesha ambapo wanaweza kukukopesha ukanunua salio?
Salio la songesha unaweza ukalifanyia miamala mingi tofauti na Songesha - LUKU ambayo utanunua LUKU pekee na huwezi kufanya muamala mwingine.

Songesha ya Vodacom mtu anaweza kuacha kutumia Voda akahamia Tigo na kukopa tena kwa Tigo pesa lakini ukikopa LUKU hauwezi kubadili number ya LUKU. Ukinunua kwa mtandao mwingine wowote lazima wakukamate...
 
Mkuu serikali yenyewe hailipi madeni ya Tanesco sembuse Raia,wewe unataka hili shirika lishindwe kujiendesha. Tena nawashauri na watu wa mamlaka za maji waje la mita za luku kabisa ili kuboresha makusanyo
 
Mkuu serikali yenyewe hailipi madeni ya Tanesco sembuse Raia,
Usifananishe serikali na mwananchi wa kawaida mkuu biashara ya kukopesha inaingiza faida kubwa saaaana fanya utafiti kwenye banks kisha utaleta majibu hapa...
 
Infantry hebu jaribu kuliangalia hilo kwa mukitadha wa Wapangaji, Ni kweli Tanesco kwa mantiki hiyo atapata faida, lkn hasara itakuja kwa wenye nyumba, mpangaji nitakopa umeme nitatumia then nahama kambi, vipi apo ?
 
Usiwarudishe nyumba. Walianza na mita za kawaida (unalipa baada ya matumizi), but watu walikuwa hawalipi kwa wakati au hawalipi kabisa.

LUKU ndio mpango mzima. Tena wangeanza kwenye taasisi za serikali kabla ya watu binafsi.
 
Usiwarudishe nyumba. Walianza na mita za kawaida (unalipa baada ya matumizi), but watu walikuwa hawalipi kwa wakati au hawalipi kabisa.
TANESCO waliweka limit ya kiwango cha matumizi na malipo? Unamruhusu mtu atumie umeme mpaka wa 400,000/= unategemea nini?

Kukopa umeme wa 10,000/= haiwezi kuiua TANESCO hata siku moja mkuu...
 
Unawezaje kukwepa deni la 20,000/= la LUKU?
Mimi ni mpangaji,nakaa nyumba Luku yangu kila kitu sishei na mtu

hii system ikikubalika ikaanza si wapangaji kama sisi tunakua tunakopa

umeme wa LAKI naingia nakaa miezi 6 nahama deni linabaki kwenye nyumba ya watu

huoni hapo kuna kushikana mashati? wengine sisi tukihamia nyumba hatuonekani tumehamia saa ngapi

na tukihama hatujulikani tumehama saa ngapi yani tupo kama ma zombie huoni tuta taftia watu majanga yasio ya lazima bwana mjeshi?
 
Naunga mkono hoja kwa 100%
 
hili ndio hata mimi nalitaka litokeee iwe kama tunavyolipia vifurushi vya ving'amuzi tu
 
Ni wapi nimezungumzia mkopo wa laki moja? Vodacom wanatoa mkopo wa laki moja kwa mara moja? Ndio maana nimesema anayeweze kuruhisiwa kukopa ni mtu mmoja tu.
Sio kila nyumba ya kupanga ina watu wengi, kuna nyumba mpangaji anamiliki luku yake peke ake

si kwamba kajiwekea ile luku ila n mwenye nyumba kaiweka,sasa kigezo kikiwa n mtu mmoja tu

nadhani mpangaji kama mimi nina sifa zote za kukopa maana nipo peke angu na baada ya mkopo kodi ikiisha πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Tumepokea ushauri tunashukuru sana mpendwa mteja wetu

TANESCO , Makao Makuu
Mnazingua kinoma hadi nahisi hii Account yenu huku JF pamoja na kuwa Verified nahisi kuna mtu binafsi kakaa geto anatuzingua,sioni kbisa msaada wenu nyie viumbe zaidi yakujibu kama ulivyojibu hapo juu.

Ngojea namimi niji verifaishe halafu naweka Profile pic la Tanesco najibadilishia na jina tukutane kwenye thread yetu pendwa ya Tanesco maswali na majibu,ngojeeeni muone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…