Tetesi: TANESCO 'kwazizima' Makamba kuhamishwa Nishati. Waendelea na 'mfungo'

Basi Januari na Maharage wamewatendea vema kama fikra zao ni paadiem tuu!!!!
 
Wewe mzee wa tupatupa, tunakuamini na mara nyingi habari zako ni za uhakika. Maharage atakuwa amebaki kwenye baridi kali.
 
Yawezekana kweli Makamba na huyo Chande wana Mapungufu yao ila ukiona Wafanyakazi wanakuchukia au Kufurahia Kutemwa au Kuhamishwa Kwako jua ya kwamba uliwazibia Mirija yao ya Upigaji ( Ufisadi ) na kusimamia vyema Uwajibikaji kitu ambacho 85% ya Wafanyakazi wa Serikalini hawakiwezi na hawakipendi ila Kuiba na Kula Bata ndiko Wanakokupenda zaidi.
 
Watungaji wa hekaya za abunuasi kazini. Kuna mwenzako jana alitunga kuwa umeme umeanza kuwaka kila sehemu baada ya makamba kutoka watu wakampiga spana kuwa sehemu nyingi tu hazina umeme.

Naona leo umekuja kivingine na uzushi mpya
 
Unachokiongea na Kitu kizuri sana, Lakini je umewaza hali z a Uchumi wa wananchi ambao ni majority, Hakuna mwekezaji ataunganishia mteja umeme kwa 27k ile hali mteja uyo kwa mwezi ananunua umeme wa 5000 tu mwezi mzima, Hio Biashara kichaa ya ivo anaweza kuifanya serikali tu kwa vile Shirika la umeme sio Business Oriented Kwa nchi nyingi tu, Shirika la Umeme lipo pale Kutoa huduma, Likibinafsiswa basi jua fika Umeme utakuwa anasa hatutaweza ku afford afu inshu za simu na umeme ni tofauti sana kuanzia installation mpaka maintenance
 
Hawatawezana na Dotto mmoja wapo hafiki X-Mas maana Maharage kaletwa na mafisadi
 
Hawatawezana na Dotto mmoja wapo hafiki X-Mas maana Maharage kaletwa na mafisadi
Maharage si ana exposure na Inshu za Nje na amefanya kazi Multi Choice basi Arudi uko, Kiuhalisi Pamoja na Mkurugenzi wa Tanesco kuteuliwa na Rais, Bado Waziri ana influence kubwa na lazima waivane na uyo Mkurugenzi makamba alivyolamba uteuzi alimleta Maharage na Kumfurusha Dr Tito Mwinuka ivo ni zamu ya Mkurugenzi aliepo nae Apishe waziri alete mtu wake
 
Maharage kaletwa na Rostam Makamba alikuwa ni mshenga tu
 
Majungu Kwa Makamba haya.Nyie Hater wake kwani Makamba aliwafanyaga nini?

Kumbe mazembe ndio yanachekelea na pia wamefuta upuuzi mwingi tuu ikiwemo utaratibu wa ku outsource kazi ambapo kabla Tanesco Wakifanya wenyewe na kutumia kama mwanya wa upigaji.
 
Kama sababu ni kufutwa kwa safari basi wenyewe ndio tatizo
Makamba ana udhaifu wake lakini safari za kikazi kufutwa zitakuwa hazikuwa na tija

Shirika lina wafanyakazi wa Tanesco nchi nzima na kila wilaya

Hizo safari za kikazi zilikuwa za nini na walikuwa wakienda kufanya nini ? Na ni akina nani hao ?

Shirika linapata hasara halafu mnataka safari ziendelee hela za safari zinatoka wapi labda wakati shirika linapata hasara

Tueleweshe source ya hizo pesa za Safari zinatoka wapi?
 
Hivi kwa nini watu wanalilia safari kama sio ubadhirifu mtupu?

Je mnataka kusema kuna watu wazima wana hamu ya kupanda gari/ndege/boti/train nk bila malengo?
Kama lengo Lao ni utalii basi watumie mishahara yao.

Serikali ingeuchukua mfumo wa private linapokuja suala la safari hakika nawaambieni hii nchi ingepaa kimaendeleo.

Safari ni ufisadi nyamavu!!! Period…..
 
Sisi watanzania tunatamani Chande apelekwe bandarini akadhibiti wizi wa pale kwa mifumo yake ya tehama
 
Jembe la ufisadi? Biteko ahakikishe huyo Maharage Chande nae anakwenda wizara ya mambo ya nje amfuate boss wake his partner in their crime syndicate!
Wivu tu
 
Kama sababu za hao wafanya kazi kufurahia kuondoka kwa Makamba ni hizo zilizoelezwa, kwa mara ya kwanza nitampongeza Makamba na rafiki yake Maharage.
Kupongeza kwangu ni kwa hili tu jambo, na siyo mengine yanayowahusu hao watu.
 
Rubbish,Basi tutamuweka pengo hapo tanesco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…