Kutokana na kazi kubwa aliyoifanya January Makamba TANESCO lazima wamchukie.
Kabla ya Makamba, mchakato wa kuunganishiwa umeme uligubikwa na urasimu uliowekwa makusudi kurahisisha rushwa.
Wateja wapya walilazimishwa kumkodia gari surveyor wa TANESCO ili aje akague jengo lako.
Mchakato wa kumpata surveyor ulichukua wiki moja mpaka mwezi na zaidi.
Surveyor waliomba rushwa ili wakurahisishie kupata umeme.
Ukikaidi utakutana na vikwazo vya kila aina, ikibidi utaorodheshewa nguzo kadhaa ili kuongezewa gharama na pia kurefusha mchakato wa kupata umeme.
Ukimalizana na surveyor utakutana na kigingi kwenye idara ya ufundi. (Service line).
Hapa utaambiwa waya hatuna, bolt zimeisha, Luku zimeisha.
Wakati wewe unahenyeshwa kwakuwa hutaki kutoa rushwa wenzako watapata huduma ingawa wewe ndiye uliyeanza kuomba.
Na hata hizo Luku zikifika utaambiwa gari bovu, mafundi wameenda kwenye operesheni hii au ile, Subiri wiki mbili.
Kitengo cha dharula nacho hakikuachwa nyuma.
Ukipata Emergency utapiga simu masaa kadhaa, akipokea atakuuliza jengo liko wapi? Ukimwambia niko Mbagala Kisewe utasubiri mwezi mzima.
Upuuzi wote huo umekomeshwa na Makamba.
Hivi sasa nchi nzima tunapiga simu makao makuu Dodoma kwa namba moja tu 0748 550 000 kupata huduma.
Simu inapokelewa kwa wakati na huduma za kuunganishiwa umeme pamoja na ile ya dharula zote zinapatikana kwa wakati.
Kwa utendaji wake huo, amekata ulaji wa mameneja na mainjinia wa vitengo, wasimamizi wa kazi, (supervisor) mafundi pamoja na Vishoka.
Watu hawa hawawezi kumpenda.
Kuhusu kukatika katika umeme, jambo hilo haikwepeki.
Umeme unasafirishwa kama tunavyosafirisha vyombo vya moto.
Hivyo kuna ajali.
Nguzo hugongwa na magari, nguzo au waya hulipuka moto nk.
Lakini hata ukitaka kurekebisha mifumo ya njia za umeme lazima uzime.
Kwahiyo kudai utaongoza wizara ya nishati au Shirika la Umeme bila kukatika umeme ni uongo na Unafiki mtupu.
Mi najua kuwa January Makamba ni mwanasiasa, kwa sababu hiyo ana maadui wengi, lakini NAMPONGEZA kwa mengi mazuri aliyofanya hasa kuisafisha TANESCO.
Namtakia kheri kwenye kazi yake mpya.