Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,497
- 3,823
Niko Mbeya but manung'uniko ya kuhusu kukatika kwa umeme nayaonaga mtandaoni tuuu!huwezi kuamini aisee!Angalieni na maeneo mnayonunua viwanja🤣🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna muda huwa unatoka hapo uliponunua kiwanja au unakaa bila kubanduka siku 365 za mwaka?Niko Mbeya but manung'uniko ya kuhusu kukatika kwa umeme nayaonaga mtandaoni tuuu!huwezi kuamini aisee!Angalieni na maeneo mnayonunua viwanja[emoji1787][emoji1787]
Huko ni kwa kina ChoiceVariableVipi Lucas mwashambwa hayuko Mbeya?
Ngoja nimwambie Luhaga Mpina mtetezi wa wanyonge.
Kuna muda huwa unatoka hapo uliponunua kiwanja au unakaa bila kubanduka siku 365 za mwaka?
kwan umeme tunatumia bure kias washindwe kupambana kubuni namna ya kuongeza uzalishajKuna clip moja twitter nilimwona mzee Dewji akisema matumizi ya umeme yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa vifaa vinavyotumia umeme vilivyoingizwa nchini katika miaka mitatu ya mama wa taifa, TV laki sita, friji laki saba, pasi laki tano, majiko ya umeme laki 8, pump za kujazia mafuta elf 60 na blah blah nyingine kibao huku akidai hizi takwimu kazipata TRA.
Kwa hiyo anatafsiri upungufu wa umeme kama maendeleo na kwamba hata bwawa la Nyerere likianza uzalishaji umeme hautatosha maana chini ya mama maendeleo yanaenda kwa kasi watu wengi wananunua vifaa vya umeme.
Sasa nilichojiuliza huo uchambuzi kautoa kama mtaalamu, kalumanzila au kaamua tu kujivika uchawa.
Aaaaaah shinyanga mjini mpaka kerooo. Ratiba n j3 na ijumaa lakin kwa wiki unakatika zaid ya mara 3 halafu ratiba ya muda haijulikaniShirika la umeme TANESCO mkoa wa Mbeya kuna tatizo kubwa, tunaomba viongozi wa makao makuu pamoja na wizara ya Nishati mliangalie hili. Hali ni mbaya sana. Kuna matatizo yafuatayo:
1. Ratiba ya kile kinachoitwa, "upungufu wa umeme" haifuatwi. Pamoja na TANESCO mkoa wa Mbeya kutoa ratiba hiyo kila wiki inayoonyesha muda ambao line husika zitakosa umeme, ratiba hii imekua ni kama kiini macho tu, kwani haifuatwi kwa asilimia 80. Shida ni nini? Tunashindwa kuelewa, ratiba wanaiandaa wenyewe na wanaikiuka wenyewe.
2. Hali ya upungufu wa umeme inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyokwenda mkoani Mbeya, wakati tulikua tunategemea hali izidi kuimarika. Kwa mfano, pamoja na mvua kubwa kuwa zinanyesha kuanzia December 2023 kwa ukanda huu, pamoja na maeneo ya Ruaha ambayo ndio chanzo kikubwa cha maji kwa bwawa la Mtera, hali ya umeme imezidi kuwa mbaya sana kulinganisha hata na kipindi cha ukame. Pia, tuliambiwa kuwa kuanzia Januari hii majaribio ya bwawa jipya la Nyerere yataanza, hivyo hali ya umeme itaboreka zaidi, lakini hakuna maboresho yoyote sana sana hali inazidi kuwa mbaya tu kwa mkoa wa Mbeya.
3. Nimeambatanisha ratiba ya upungufu wa umeme kwa wiki hii kama mfano. Hii ratiba hadi sasa haijafuatwa kwa asilimia 80. Mfano eneo nililopo, siku ya Jumatatu tarehe 15, kwanza tulilala bila umeme usiku wa kuamkia jumatatu (ulikatika jumapili saa 5 usiku na kurudi saa 11 asubuhi), halafu saa 12 ukakatika tena, ukarudi saa tatu za usiku, wakati ratiba ilikuwa inaonyesha ungerudi saa 12 jioni. Pia, siku ya leo, Jumanne tarehe 16 ratiba yetu ilikua inaonyesha utakatika saa 12 jioni hadi saa 5 usiku, lakini tayari umekatika tangu saa tatu asubuhi.
TANESCO MKOA WA MBEYA INA SHIDA GANI?
Aione kwenye jalada beny jr
Uchawa pro maxKuna clip moja twitter nilimwona mzee Dewji akisema matumizi ya umeme yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa vifaa vinavyotumia umeme vilivyoingizwa nchini katika miaka mitatu ya mama wa taifa, TV laki sita, friji laki saba, pasi laki tano, majiko ya umeme laki 8, pump za kujazia mafuta elf 60 na blah blah nyingine kibao huku akidai hizi takwimu kazipata TRA.
Kwa hiyo anatafsiri upungufu wa umeme kama maendeleo na kwamba hata bwawa la Nyerere likianza uzalishaji umeme hautatosha maana chini ya mama maendeleo yanaenda kwa kasi watu wengi wananunua vifaa vya umeme.
Sasa nilichojiuliza huo uchambuzi kautoa kama mtaalamu, kalumanzila au kaamua tu kujivika uchawa.
Kuna jamaa wana kiwanda cha maji, yaani uzalishaji ni kama umesimama kabisa!Daa mbeya tunateseka sana sisi wa viwanda hatufanyi kazi yani kero kero sana kazi haziendi lakini nao TRA nao wako moto hawa oni tatizo hili la umeme mda mwingine umeme unaweza ukawepo ila wanakuwa wametowa nguvu kwenye mitambo mikubwa