KERO TANESCO Mkoa wa Katavi mmepatwa na nini, mbona kila siku mnakata umeme ifikapo saa mbili kasoro usiku?

KERO TANESCO Mkoa wa Katavi mmepatwa na nini, mbona kila siku mnakata umeme ifikapo saa mbili kasoro usiku?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Kero hii ya kukata umeme ifikapo saa mbili kasoro usiku kila siku katika mji ya Mpanda tumechoka kwani wala hatufahamu mnakata umeme kwa masirahi ya nani?.

Jambo ambalo hatupendezwi nalo wala taarifa yoyote ile hamtoi kwa wakazi wa Mpanda na tunaona waziwazi hizi ni hujuma kwetu Wananchi wa Mpanda maana kukata umeme Kila siku inapofika mida ya usiku inaleta hali ya hatari kwetu hususani vibaka na wezi wanatamalaki kufanya uhalifu.

Wenye mamlaka tunaomba chukueni hatua za kuondoa kero hii ambayo haivumiliki.
photo_2025-03-31_20-30-31.jpg

photo_2025-03-31_20-30-43.jpg

Pia soma ~ Mwananchi Katavi ahoji umeme kukatika wakati wameunganishwa Gridi ya Taifa, TANESCO yafafanua
 
Tanesco ovyo nchi nzima ,hadi unajiuliza faida ya umeme wa bwawa la nyerere mbona haionekani? Kila siku umeme unakatika ukiuliza unaambiwa ni miundombinu ya usafilishaji umeme imeleta hitilafu.
 
Back
Top Bottom