Kero hii ya kukata umeme ifikapo saa mbili kasoro usiku kila siku katika mji ya Mpanda tumechoka kwani wala hatufahamu mnakata umeme kwa masirahi ya nani?.
Jambo ambalo hatupendezwi nalo wala taarifa yoyote ile hamtoi kwa wakazi wa Mpanda na tunaona waziwazi hizi ni hujuma kwetu Wananchi wa Mpanda maana kukata umeme Kila siku inapofika mida ya usiku inaleta hali ya hatari kwetu hususani vibaka na wezi wanatamalaki kufanya uhalifu.
Wenye mamlaka tunaomba chukueni hatua za kuondoa kero hii ambayo haivumiliki.
Tanesco ovyo nchi nzima ,hadi unajiuliza faida ya umeme wa bwawa la nyerere mbona haionekani? Kila siku umeme unakatika ukiuliza unaambiwa ni miundombinu ya usafilishaji umeme imeleta hitilafu.