TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Kama kawaislda tenesco haijawahi kufanya manunuzi ya maana yanayojali maslahi ya umma hapo lazima kuna ufisadi tiari
 
Wamalizie Plan ya JK ya kujenga Kinyerezi III na Kinyrerezi IV na sio kutegemea hii mipango ya zima kibatari....

Yaani wanachofanya ni kama wanatarajia baada ya muda mfupi mvua zitaanza kunyesha!
Kweli kabisa. Wawekeze zaidi kwenye gesi tuwe na megawat zaidi ya 2500 zinazotokana na Gesi tu
 
Naona tunarudia yale yale ya Dowans/IPTL na Richmond na kashfa ya malipo yao ya shilingi milioni 54 kwa dakika.

Naona watu wanatafuta hela kwaajili ya Uchaguzi 2025.

Kweli Nchi inaliwa na wenye Nchi 🙆
 
Kweli kabisa. Wawekeze zaidi kwenye gesi tuwe na megawat zaidi ya 2500 zinazotokana na Gesi tu
Na hili likifanyika, kitakachobaki ni hofu ya kukatika umeme tu kutokana na miundombinu lakini sio tena uhaba wa umeme eti kisa kuna ukame!

Sijui tunakwama wapi!
 
Kashfa Juu ya Kashfa!
10% juu ya Ten Percent!

Na watanzania tumenyamaza Tuli!
 
Naona tunarudia yale yale ya Dowans/IPTL na Richmond na kashfa ya malipo yao ya shilingi milioni 54 kwa dakika.

Naona watu wanatafuta hela kwaajili ya Uchaguzi 2025.

Kweli Nchi inaliwa na wenye Nchi 🙆
Hamna cha Dowans wala IPTL... ni ujinga tu wa viongozi...

Nchi tayari imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh 1 TRILLION kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi.

Ambacho "kinatushinda" ni kujenga tu mitambo ya kuzalisha umeme pale Kinyerezi kwa sababu tayari gesi ipo!

Ukiangalia hiyo mipango yao utaona wazi ni ya kutegea mvua... kwamba mvua ikishanyesha, basi tatizo litapungua!
 
Dharura za umeme Tanzania hazitakaa ziishe kwasababu ndiyo kichaka cha utajirisho!
 
Miaka miwili nyuma kulikuwa na umeme wa uhakika na lugha ilikuwa ya majigambo tunaweza miradi ya megawatts 2000+ na mfano juu.

Leo tumerudi na hadithi za megawatts 20.

R.I.P shujaa Magufuli
Umeme wetu wategemea Mvua na Mwaka huu mvua zimekataa kabisa
 
Wamalizie Plan ya JK ya kujenga Kinyerezi III na Kinyrerezi IV na sio kutegemea hii mipango ya zima kibatari....

Yaani wanachofanya ni kama wanatarajia baada ya muda mfupi mvua zitaanza kunyesha!
Tatizo ni nchi yetu haina succession ya miradi, kila mtu anataka akumbukwe kivyake

Kinyerezi ingetosha kabisa kuzalisha umeme wa kutosha nchi nzima
 
Naona tunarudia yale yale ya Dowans/IPTL na Richmond na kashfa ya malipo yao ya shilingi milioni 54 kwa dakika.

Naona watu wanatafuta hela kwaajili ya Uchaguzi 2025.

Kweli Nchi inaliwa na wenye Nchi [emoji134]
We naye umezidi uongo
 
Mambo ya masandarusi kama kazi !! Walisema mitambo ilikuwa haifanyiwi marekebisho kipindi kile !! Sasa ndio inafanyiwa matengenezo!! Na umeme ndiyo imekuwa shidaa !!
kakojoe kwenye mito ili tupate maji ya kusukuma mitambo.
Unaona kabisa ukame hata maji ya matumizi nyumbani mgogoro bado unawaza umeme wa maji!
 
Tatizo ni nchi yetu haina succession ya miradi, kila mtu anataka akumbukwe kivyake

Kinyerezi ingetosha kabisa kuzalisha umeme wa kutosha nchi nzima
Hilo ndo tatizo... nahisi kila mmoja ni kama anataka aandike historia yake...

Ule Mradi wa Kinyerezi kama ungekamilika, hivi sasa ingekuwa tuna umeme mwingi ambao hatuwezi hata "kuumaliza"

Na uzuri zaidi, hata lile Bwawa la Nyerere lingeweza kujengwa bila pressure hii iliyopo sasa!!!
 
Mmiliki wa huo mtambo ni nani? Tuanzie hapa kwanza. Kama ni TANESCO, sina tatizo! Ila kama ni mabepari wa Richmond, basi tujiandae kupigwa tena na kitu kizito kichwani.
 
another richmond in the making
 
Miaka miwili nyuma kulikuwa na umeme wa uhakika na lugha ilikuwa ya majigambo tunaweza miradi ya megawatts 2000+ na mfano juu.

Leo tumerudi na hadithi za megawatts 20.

R.I.P shujaa Magufuli
Huyo shujaa wako angejaza maji kwa mkojo? Kile kitendo cha kuacha mradi wa gas ambayo ilikuwa tayari kwenye stations ni kununulia tu mitambo na kuifunga ilikuwa wazo mfu kwasababu gas haina msimu kama maji.
Yani nchi iliendeshwa kwa kutumia ndoto za Nyerere za 70s kana kwamba dunia iko vile vile
 
Bwawa kuchelewa ndiyo wengine wanapata tender . Mama awe makini sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…