shamimuodd
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,188
- 2,113
Hizi ndizo zilimuondoa Lowasa kwenye uwaziri mkuu. Ila jamani hakika bongo kuna mchwa wasiokuwa na aibu. Hivi kipindi cha Dkt Magufuli mbona hapakuwa kabisa na dalili za kuagizia mitambo?????Hizi jitihada za muda mfupi zimetugharimu sana kama Taifa, hasa kupitia hili shirika la Umeme, nitashangaa kama mwisho wa siku haitakuja kuwa kashfa, ni suala la muda tu.
R.I.P shujaa Magufuli
Kwa sasa wanajikuta wanatumia hela nyingi kujenga vyanzo viwili kwa pamoja....Hilo ndo tatizo... nahisi kila mmoja ni kama anataka aandike historia yake...
Ule Mradi wa Kinyerezi kama ungekamilika, hivi sasa ingekuwa tuna umeme mwingi ambao hatuwezi hata "kuumaliza"
Na uzuri zaidi, hata lile Bwawa la Nyerere lingeweza kujengwa bila pressure hii iliyopo sasa!!!
Ndio akili za watu wanaojinasibu wana-chadema hizo kwenye ili jukwaa wao mzaha kwenye kila kitu.
Tuambie wewe uliye mkweli MkuuWe naye umezidi uongo
Watu wamegawana kuila NchiHamna cha Dowans wala IPTL... ni ujinga tu wa viongozi...
Nchi tayari imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh 1 TRILLION kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi.
Ambacho "kinatushinda" ni kujenga tu mitambo ya kuzalisha umeme pale Kinyerezi kwa sababu tayari gesi ipo!
Ukiangalia hiyo mipango yao utaona wazi ni ya kutegea mvua... kwamba mvua ikishanyesha, basi tatizo litapungua!
Hilo Jambazi sio shujaa wala nini Aangamie kwenye moto wa milele.Ndio akili za watu wanaojinasibu wana-chadema hizo kwenye ili jukwaa wao mzaha kwenye kila kitu.
Sasa ndio nini ulicho post, si usome tu kama huna cha kuchangia.
Ok goodHilo Jambazi sio shujaa wala nini Aangamie kwenye moto wa milele.
I am happy because you are around.Wamalizie Plan ya JK ya kujenga Kinyerezi III na Kinyrerezi IV na sio kutegemea hii mipango ya zima kibatari....
Yaani wanachofanya ni kama wanatarajia baada ya muda mfupi mvua zitaanza kunyesha!
Kwa nini watu wengi mna act kama vile TANESCO hawana kipato. Sijawahi kuona seuemu yoyote taarifa ya mapato ya TANESCO kwa mwezi au mwaka. Kila siku tunasikia manunuzi, matatizo na madeni tu.Ni watu wenye very simple minds, kazi yao kuropoka tu. Hawajui ata madeni iliyokuwa nayo TANESCO kwa suppliers wa gas were in trillions.
Financial Statements zao zipo kwenye website yao be it mara nyingi ni a year behind, mwaka huu awajaweka.Kwa nini watu wengi mna act kama vile TANESCO hawana kipato. Sijawahi kuona seuemu yoyote taarifa ya mapato ya TANESCO kwa mwezi au mwaka. Kila siku tunasikia manunuzi, matatizo na madeni tu.
Sidhani kama kuna shirika lenye mapato makubwa kuzidi TANESCO. Tuanzie hapo.
Dah... long time no see!!I am happy because you are around.
Huu Mpango Wametupata HatuchomoiMjini mipango
Muongo MuongozeNjia ya mtu muongo siku zote huwa ni fupi.
Anyway kuna watu wengi ndani ya JF walishatuonya miezi kadhaa nyuma inatafutwa sababu ya kupigwa deal.
Ngoja sasa tuambiwe gharama ya huo mtambo.
Ajabu zaidi logistic tu ya kununua huo mtambo na kuuleta hadi Tanzania udhani ni kama chini ya miezi mitatu; ina maana walijua mapema nchi itakuwa na giza la muda mrefu kweli kweli kuweza kufanya yao.
Only in Tanzania
Hiyo kesi nyingine. Richmond mpyaIjumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.
Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.
Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.
Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.
Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.
“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.
Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
View attachment 2437844
wanaombeza magufuli wana jehanamu yao spesho...Miaka miwili nyuma kulikuwa na umeme wa uhakika na lugha ilikuwa ya majigambo tunaweza miradi ya megawatts 2000+ na mfano juu.
Leo tumerudi na hadithi za megawatts 20.
R.I.P shujaa Magufuli