Habari wateja wetu,
Tunawashukuru kwa swali lenu kuhusu bei za uniti za umeme, pamoja na wote waliochangia kutoa maoni na ufafanuzi kuhusu suala hili.
Tungependa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu bei za uniti za umeme. Mfumo wa tozo za umeme umegawanyika katika makundi makuu mawili ya wateja, ambayo ni
Tariff 1 na
Tariff 4.
MAKUNDI YA WATUMIAJI WA UMEME - TAARIFA KUHUSU TARRIF 1 & 4 (T01 & T04)
Mfumo wa manunuzi ya umeme hupanga mita zote kulingana na matumizi ya mteja, eneo na vigezo vingine. Hakuna huduma ya "service charge", bali mita hupangwa katika makundi mawili ya matumizi, yaani kundi la T01 na T04. Kwa lugha rahisi, huitwa Tariffs (Matumizi).
Aina za Makundi ya Watumiaji wa Umeme Majumbani
- Tariff 04 (T04): Matumizi ya chini ya unit 75 kwa mwezi, matumizi madogo vijijini pekee.
- Tariff 01 (T01): Matumizi ya kati, mjini na vijijini kwa mteja mwenye matumizi zaidi ya unit 75 kwa mwezi. Kundi hili mteja hana kikomo cha manunuzi ya umeme/unit kwa mwezi, pia matumizi ni ya nyumbani na siyo viwandani kama wengi wanavyodhani.
NB: Kigezo cha kundi ambalo mita itapangwa na mfumo si matumizi pekee.
Vigezo vya Kundi la Tariff 04 (T04):
Eneo: Liwe la kijijini na siyo mjini.
Matumizi: Yawe chini ya unit 75 kwa mwezi. Hata kama upo kijijini lakini matumizi yako yanazidi unit 75, bado hautakidhi kigezo.
Matumizi yasihusishe biashara, uzalishaji mali au nyumba yenye wapangaji.
Mteja awe amefanya manunuzi ya umeme kwa zaidi ya miezi sita mfululizo kwa mita mpya, kwaajili ya tathimini ya matumizi yake ya umeme kwa muda huo.
Ili kukidhi kuwa katika kundi la T04, ni lazima mteja akidhi vigezo vyote vilivyotajwa na siyo kimoja kati ya hivyo.
Bei za Unit kutokana na aina ya Tariff:
- Unit 1 kwa mteja wa matumizi madogo (Tariff 4) ni Tsh 100/= bila VAT, pamoja na VAT ni Tsh 122/=
- Unit 1 kwa mteja wa matumizi ya kawaida (Tariff 1) ni Tsh 292/= bila VAT, pamoja na VAT ni Tsh 357/=
Kumbuka
Mita ikishahamishwa kutoka kundi la T04 kwenda kundi la matumizi ya kati (T1) kutokana na kuzidisha manunuzi ya umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi, haiwezekani kurudishwa tena kwenye kundi la awali la T04, hata kama matumizi yatapungua baadaye au kubadilishiwa mita.
Asante. ^PK