TANESCO
Official Account
- Jul 12, 2014
- 5,210
- 2,779
Habari, ndugu mteja. Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja.Naomba kufahamu je Kuna kifaa kinachowezesha wateja kutumia meter Moja lakini kila mmoja akanunua umeme kivyake?
Kwa sasa, ikiwa unahitaji huduma ya aina hiyo, unaweza kuitumia kupitia mfumo wa sub mita, ambapo sub mita huunganishwa na mita kuu ya TANESCO ili kukidhi mahitaji binafsi ya watumiaji.
Tafadhali fahamu kuwa sub-meter (mita ndogo za kugawa matumizi kwa kila mpangaji au mtumiaji) hufungwa baada ya mita ya TANESCO na hufungwa na fundi aliyechaguliwa na mteja kulingana na mahitaji yake. Hivyo, matengenezo na usimamizi wa sub-meter hizo ni jukumu la mteja na fundi wake wa umeme.
Kwahiyo, matumizi, ukipata changamoto, tafadhali umshirikishe fundi wako ili afanye ukaguzi na kurekebisha changamoto iliyojitokeza. Endapo itabainika kuwa tatizo linatokana na miundombinu ya TANESCO au mita kuu ya TANESCO, tutachukua hatua stahiki kwa haraka ili kukuhudumia.
Asante kwa kuendelea kutuamini. Tupo tayari kukuhudumia wakati wowote. ^HN