Ndondombi Mulin
JF-Expert Member
- Mar 13, 2016
- 820
- 3,618
Kudadadeki.Kuna mtu amesema hapo juu kuwa kuna tariff 6 ambayo ni ya kwenu wafanyakazi wa tanesco ati mnapewa unit 750 kwa mwezi kwa shilingi 8,500/= hii ni ya kweli mkuu.
Habari ndugu mteja,Kama mteja alikuwa T04, mwezi mmoja akanunua umeme zaidi ya unit 75, atapelekwa kwenye T01 papo kwa papo au mpaka afanye hivyo mfululizo miezi kadhaa?
Mtu yupo mjini ila matumizi yake hayazidi units 75 kwanini asipate huduma hiyo?Habari wateja wetu,
Tunawashukuru kwa swali lenu kuhusu bei za uniti za umeme, pamoja na wote waliochangia kutoa maoni na ufafanuzi kuhusu suala hili.
Tungependa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu bei za uniti za umeme. Mfumo wa tozo za umeme umegawanyika katika makundi makuu mawili ya wateja, ambayo ni Tariff 1 na Tariff 4.
MAKUNDI YA WATUMIAJI WA UMEME - TAARIFA KUHUSU TARRIF 1 & 4 (T01 & T04)
Mfumo wa manunuzi ya umeme hupanga mita zote kulingana na matumizi ya mteja, eneo na vigezo vingine. Hakuna huduma ya "service charge", bali mita hupangwa katika makundi mawili ya matumizi, yaani kundi la T01 na T04. Kwa lugha rahisi, huitwa Tariffs (Matumizi).
Aina za Makundi ya Watumiaji wa Umeme Majumbani
NB: Kigezo cha kundi ambalo mita itapangwa na mfumo si matumizi pekee.
- Tariff 04 (T04): Matumizi ya chini ya unit 75 kwa mwezi, matumizi madogo vijijini pekee.
- Tariff 01 (T01): Matumizi ya kati, mjini na vijijini kwa mteja mwenye matumizi zaidi ya unit 75 kwa mwezi. Kundi hili mteja hana kikomo cha manunuzi ya umeme/unit kwa mwezi, pia matumizi ni ya nyumbani na siyo viwandani kama wengi wanavyodhani.
Vigezo vya Kundi la Tariff 04 (T04):
Eneo: Liwe la kijijini na siyo mjini. Matumizi: Yawe chini ya unit 75 kwa mwezi. Hata kama upo kijijini lakini matumizi yako yanazidi unit 75, bado hautakidhi kigezo. Matumizi yasihusishe biashara, uzalishaji mali au nyumba yenye wapangaji. Mteja awe amefanya manunuzi ya umeme kwa zaidi ya miezi sita mfululizo kwa mita mpya, kwaajili ya tathimini ya matumizi yake ya umeme kwa muda huo.Ili kukidhi kuwa katika kundi la T04, ni lazima mteja akidhi vigezo vyote vilivyotajwa na siyo kimoja kati ya hivyo.Bei za Unit kutokana na aina ya Tariff:
Kumbuka
- Unit 1 kwa mteja wa matumizi madogo (Tariff 4) ni Tsh 100/= bila VAT, pamoja na VAT ni Tsh 122/=
- Unit 1 kwa mteja wa matumizi ya kawaida (Tariff 1) ni Tsh 292/= bila VAT, pamoja na VAT ni Tsh 357/=
Mita ikishahamishwa kutoka kundi la T04 kwenda kundi la matumizi ya kati (T1) kutokana na kuzidisha manunuzi ya umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi, haiwezekani kurudishwa tena kwenye kundi la awali la T04, hata kama matumizi yatapungua baadaye au kubadilishiwa mita.
Asante. ^PK
Habari Sozo_Mtu yupo mjini ila matumizi yake hayazidi units 75 kwanini asipate huduma hiyo?
Nimekuelewa, Mimi nipo mjini, ila matumizi yangu hayazidi units 75... kwanini msiniweke kwenye kundi la T04?Habari Sozo_
Kama tulivyoeleza hapo awali, Ili mteja aweze kuwekwa katika kundi la T04, ni lazima mteja akidhi vigezo vyote vilivyotajwa na siyo kimoja kati ya hivyo. ^PK
Habari, ndugu mteja.Nimekuelewa, Mimi nipo mjini, ila matumizi yangu hayazidi units 75... kwanini msiniweke kwenye kundi la T04?
Mwanza imekuwa kawaida umeme kukatwa alfajiri na kurejeshwa kati ya saa 12 na saa 1 usiku.Habari, ndugu mteja.
Tusamehe hatukuelewa ujumbe wako wa awali. Kutokana na tathmini ya sasa, taarif ziliwekwa kutokana na mtazamo mbali mbali juu ya matumizi ya umeme vijijini na mjini.
Ila kwa ujumbe wako, tunaomba tuipokee kama maoni yakufanyia kazi.
Asante. ^PK.
Itakuwa vizuri mkiifanyia kazi, wenye matumizi makubwa wawe T01, na wenye matumizi madogo wabaki T04, bila kujalisha yupo mjini au kijijini, ikiwa wa kijijini wa matumizi makubwa amewekwa T01 basi na wa mjini wa matumizi madogo awekwe T04.Habari, ndugu mteja.
Tusamehe hatukuelewa ujumbe wako wa awali. Kutokana na tathmini ya sasa, taarif ziliwekwa kutokana na mtazamo mbali mbali juu ya matumizi ya umeme vijijini na mjini.
Ila kwa ujumbe wako, tunaomba tuipokee kama maoni yakufanyia kazi.
Asante. ^PK.
Zamu yao mkuu, hata ungekuwa wewe ungeenjoy kimyakimya.Kudadadeki.
Kama ni kweli, basi hawa Washenzi kwenye Keki ya Taifa, wamejimegea upande mzuri sana.
Kwa zama hizi, ukipata umeme kwa bei hii, Maisha yako yatakuwa marahisi sana, issue za Gas, AC, Garden kwako vitakuwa full Automated 24/7.
Tanzania bila rushwa, haiwezekani.
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo, Ndugu mteja, tunapenda kukufahamisha kuna vitu vinavyopelekea umeme kuisha kwa haraka;Kuna Nyumba ina wapangaji 5
(Watanao)
Hakuna Jiko la Umeme.
Hakuna Heater.
Hawatumii sana Pasi zaidi ya Feni na Fridge.
WANALIPA UMEME WA ELFU 50 KWA MWEZI.
Hii haipo sawa kabisa.
Kuna Dhuruma za ajabu sana
Naomba msaada wenu Tanesco katika hili.
Tulijua tatizo ni Wiring au Earth load.
TANESCO WANAANGAZA MAISHA YETU.
TANESCO
Daaaaah jamaa wameseti robot as official TANESCO na wanazengo kadhaa wanaamin wanachart na mtu wa TANESCO
hapana ni TANESCO wenyewe, angalia signature hapo chini baada ya majibu yao zinatofautianaDaaaaah jamaa wameseti robot as official TANESCO na wanazengo kadhaa wanaamin wanachart na mtu wa TANESCO
Mijadala mingi humu jukwaani inadhihirisha watanzania wengi ni weupe vichwani. Swali ni kwanini bei zitofautiane? Mtu anajibu kwa sababu kuna tariff 0 na tarrif 1. Jamani hebu tujifunzeni reasoning kama hatuna uwezo huo basi tuna safari ndefu sana. Anyway; Mleta mada anaka kujua hivi "Kwani wateja wote bila kujali matumizi yao wakiuziwa umeme kwa bei moja kuna tatizo gani?" Mbona mafuta tunauziwa kwa bei hiyo hiyo moja bila kujali unayatumia kwa kiwango gani?kama natumia umeme chini ya Unit 72 kwa mwezi na yule wa zaidi ya Unit hizo wote tukipata bei moja ya Unit kipi kitatokea.?
Namaanisha mfano Vocha za Simu wote tunanunua bei moj kwa wiki, kuna wanaomaliza kwa siku na kunawasiomliza mpaka wiki inaishi kwa nini na Luku isiwe hivyo?