Responded HOJA TANESCO, naomba kujua utofauti wa bei za unit za umeme inasababishwa na nini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Habari ndugu johnmashilatu, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tunapenda kukufahamisha kuwa katizo la huduma ya umeme katika Mkoa wa Mwanza lilitangazwa rasmi na lilihusu baadhi ya maeneo kwa siku zilizoainishwa kwenye tangazo la TANESCO.

Katizo hilo lilipangwa kwa muda ili kupisha utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma. Mradi huu unalenga kuimarisha miundombinu ya umeme pamoja na kuongeza uhakika na ubora wa huduma ya umeme kwa wateja.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunakushukuru kwa uvumilivu wako. Asante.^FL
 
S
Asante.
Sio wateja/ wabanchi wote waliona/ kusikia tangazo hilo. Ingekuwa vyema kama ungeyarejea yaliyomo hasa hiyo " baadhi" ya maeneo.

Pia, swali langu lilitaka kufahamu ni lini tatizo hilo litamalizika?
 
S

Asante.
Sio wateja/ wabanchi wote waliona/ kusikia tangazo hilo. Ingekuwa vyema kama ungeyarejea yaliyomo hasa hiyo " baadhi" ya maeneo.

Pia, swali langu lilitaka kufahamu ni lini tatizo hilo litamalizika?
Ndugu johnmashilatu,
Tunapenda kukufahamisha kuwa, kwa mujibu wa tangazo rasmi la TANESCO, ratiba ya katizo la huduma ya umeme kwa Mkoa wa Mwanza ilihitimishwa jana.

Pia pale tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo au maboresho yaliyopangwa, TANESCO hutoa taarifa mapema zikieleza sababu za katizo pamoja na muda unaotarajiwa wa utekelezaji. Taarifa hizi hutolewa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwemo ujumbe mfupi (SMS), mitandao ya kijamii na makundi ya WhatsApp yaliyopangwa kulingana na maeneo.

Iwapo hukupata taarifa hizo, tunaomba radhi. Tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp pamoja na jina la eneo lako kupitia ujumbe binafsi (inbox) ili tuweze kukuunganisha kwenye kundi husika na uendelee kupokea taarifa muhimu kuhusu huduma ya umeme katika eneo lako.

Asante kwa uelewa na ushirikiano wako.^FL
 
Habari ndugu Holoholo, asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tuandikie namba yako ya mita kwa maelekezo zaidi.^FL
 
Wewe ndio fala huelewi nini watu au tanesco wamejibu, bei zinatofautiana kutokana na aina ya kiwango cha matumizi kwa mwezi ndio maana kuna tartifs mbalimbali, wanaotumia umeme kidogo hasa vijijini maana yake ni kundi la maskini wao wamewekewa unit moja kwa sh 100, wenye matumizi ya kati wamewekewa sh 300. Sasa wewe unachohoji nini kama sio ujuaji halafu mbaya zaidi ni new member unafoka.
 
kwanini wote wasiwe na bei moja
 
Habari ndugu Holoholo, asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tuandikie namba yako ya mita kwa maelekezo zaidi.^FL
nahtaji tu ufafanuzi sitataja namba ya mita yangu kwa sababu kiusalama na binafsi.
 
wewe ndiye haujamuelewa jamaa. Jamaa anauliza, kwa nini kuwe na madaraja wakati umeme ni uleule? Kwa nini umeme usiwe wa bei moja kwa wote maskini na tajiri? Kama mtu ana matumizi makubwa kwa mwezi maana yake si itamuhtaji kununua umeme kulingana na mahtaji yake? Kwa nini wanamuongezea bei ya unity? Kwa niaba yako nawaita TANESCO kwa ufafanuzi.
 
Habari ndugu Tulibhalegha, asante kwa kuwasiliana nasi.

1. Suala la umeme ni taaluma, katika utaalam huo kuna mahitaji (demand) mahitaji ndiyo yanatoa taswira ya aina ya miundombinu inayohitajika kukidhi mahitaji ya mteja.

2. Hata katika mazingira ya kawaida umeme wa majumbani unatofautiana na umeme wa viwandani. Msongo (voltage) unazopokea ni tofauti na viwandani. Lakini kwenye viwanda utasikia lugha nyingi Kama kVA,Power factors nk. Vitu Kama hivyo vinaleta utofauti sana kwenye mahitaji,namna ya malipo, hata miundombinu.

3. Mtumiaji mkubwa wa umeme (viwanda) vinasababisha mzigo mkubwa kwenye transfoma na nyaya za usambazaji, jambo linalohitaji miundombinu ghali Zaidi ukilinganisha na majubani.Katika hali ya kawaida utofauti lazima uwepo.

KUHUSU BEI MOJA
Ni ukweli kuwa, Kama watumiaji wote wangeuziwa umeme kwa bei moja kuna uwezekano mkubwa kuwa ingekuwa moja ya nishati ya gharama kubwa Zaidi hivyo ingewafanya wananchi wengi washindwe kabisa kumudu umeme.
Ndiyo maana Serikali inachukulia umeme kama huduma ya msingi ya kijamii, na kuweka ruzuku mfano;miradi ya REA kulinda wananchi wa hali ya chini ili wamudu mwanga na mahitaji madogo ya nyumbani.

Asante.^FL
 
Sasa kwann upande wa mteja kutoka tarrif 1 kwenda tarrif zero n mpka uandke barua? Kwann wasibadilishe wenyewe (tannesco) hawababilishi automatically?
Nchi hii ina mambo mengi ya ovyo kweli kweli. Kutoka Tarrif 01 kwenda Tarrif 0 ni mpaka uandike barua, lakini kutoka Tarrif 0 kwenda Tarrif 01 ni automatic. Kwa nini isiwe automatic hata kutoka Tarrif 01 kwenda Tarrif 0?
Lakini pia usidhani kwamba utaandika barua leo ya kuomba kubadilishiwa Tarrif ukafanikiwa leo au, hakuna kitu cha namna hiyo. Utasumbuka sana tena sana.
Wakati wa utawala wa JPM ilikuwa rahisi angalau, lakini baada tu ya kutoweka kwake, ni ngumu mno.
 
Asante TANESCO
 
Asante kwa maelekezo mazuri,
Naomba kufahamishwa, kama Mimi ni mteja wa tarrif 04. Kwa mwezi nikiwa nanunua unit 20 TU, inaruhusiwa? Ama mpaka niwe nanunua unit 75 kwa mwezi? TANESCO
 
Asante kwa maelekezo mazuri,
Naomba kufahamishwa, kama Mimi ni mteja wa tarrif 04. Kwa mwezi nikiwa nanunua unit 20 TU, inaruhusiwa? Ama mpaka niwe nanunua unit 75 kwa mwezi? TANESCO
Habari, ndugu mteja.

Ndio, inaruhusiwa. Chakuzingatia ni kuhakikisha matumizi yako yasizidi unit 75 kwa mwezi.

Asante. ^PK
 
Sasa kwann upande wa mteja kutoka tarrif 1 kwenda tarrif zero n mpka uandke barua? Kwann wasibadilishe wenyewe (tannesco) hawababilishi automatically?
Habari, ndugu mteja.

Kwa kawaida, mteja anapohamishwa kutoka Tariff 4 kwenda Tariff 1 na akahitaji kurejea kwenye Tariff 4, mteja anapaswa kununua umeme usiozidi uniti 75 kwa mwezi kwa kipindi cha takribani miezi mitatu hadi sita, na akakidhi vigezo vilivyowekwa, mfumo utamrejesha moja kwa moja kwenye Tariff 4.

Aidha, kuandika barua ya maombi ni mojawapo ya taratibu zinazotumika. Kupitia barua hiyo, mteja huomba kufanyiwa tathmini ya matumizi yake ya umeme ili kubaini kama anastahili kubadilishiwa tariff kulingana na vigezo vinavyotumika. ^HN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…