Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME CHA KINYEREZI NA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME YA MSONGO WA KILOVOTI 132 KINYEREZI-GONGOLAMBOTO
Ijumaa 15 Novemba, 2024.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuhusu maboresho ya miundombinu yanayoendelea katika Kituo cha Kinyerezi kwa kuongeza transfoma kubwa ya MVA 175 na upanuzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovolti 132 kutoka Kinyerezi hadi Gongo la mboto.
Maboresho haya yataathiri hali ya upatikanaji wa umeme kwa vipindi tofauti kwa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Mkuranga, maeneo ya Mbagala, Chanika, Kisarawe, Gongo la mboto na Kipawa, kuanzia Jumamosi alfajiri ya tarehe 16 Novemba 2024 hadi Jumanne jioni ya Tarehe 19 Novemba 2024.
Kufanyika kwa maboresho haya kutawezesha umeme mwingi na wa kutosha unaozalishwa kwa sasa nchini kuwafikia wateja wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kwa ubora na uhakika.
Shirika linawashukuru kwa uvumilivu wateja wake wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambao wataathirika na utekelezaji wa kazi hii muhimu katika kipindi chote ambacho kazi hii itakua inaendelea.
Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA, TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA
www.tanesco.cotz