Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa
TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu
Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu
Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"
Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.
View attachment 2753272
Huu umropo, ropo ropo yake hii baada ya "kuvimbewa maharage ya wapi" umemnyang'anya tonge mdomoni dadeki!
Aende Ttcl nako akayafanye aliyoyafanya Tanesco waTz tutayapokea tu, kwa kuwa sasa hatuna mtetezi.
Rais Samia kuendelea kukumbatia hawa mumiani badala ya kufukuza inamharibia taswira na haiba yake sana.
Inaonekana dhahiri hayuko na wananchi, bali yuko upande wa genge la hawa wezi na ananufaika nao.
Hatua anazochukua za kuuma na kupuliza kwa mtindo wa panya, asidhani anawafurahisha waTz, aelewe kuwa anawakera na kuwaudhi pakubwa sana waTz!
Wana mizizi gani imara hawa mafisadi kushindwa kung'olewa hata wanaponajisi hadharani taaluma na ajira zao?
Je yeye Rais Samia anakuwa ananufaika na nini katika madhila wanayoyapitia wananchi kwa sasa kutokana na utendaji mbaya wa hawa wahuni hadi aendelee kuwalinda kwa mtindo wa: "wa huku peleka kule na wa kule lete huku"?
Mtindo huu wa uteuzi na utenguzi umemtia doa kubwa sana Rais Samia katika utawala wake huu na kuzirudisha imani za raia zinazoendelea kuporomoka kila uchao itahitaji nguvu za ziada!
Mgao wa umeme na maji kila kona ya nchi ulivyotamalaki, tafsiri yake ni nini kwa mtawala kama huyu kuendelea kukaa kimya huku akicheka na nyani?
Maswali yote haya yasiyokuwa na majibu ina maana yeye Rais hazisikii kero hizi!
Tukisema Ccm imeshindwa kuongoza nchi, hatusemi kwa chuki bali tunasema kwa kufuata mnyororo wa matukio haya mabaya ya kiuongozi na kiutawala yanayoivua Serikali nguo.