TANESCO: Tuna upungufu, siyo mgao wa umeme. Wananchi endeleeni kuvumilia

TANESCO: Tuna upungufu, siyo mgao wa umeme. Wananchi endeleeni kuvumilia

Kwani we hukusikia ripoti ya uchunguzi iliyotolewa juzi?

TANESCO wamegundua maeneo ya buza buza kushuka chini huko hakunaga matumizi ya msingi ya umeme

Zaidi ya kuchajia simu afu zikijaa muanze kusumbua mitandaoni na habari za Yanga.
Duh! sio haki kabisa.
 
Hakuna shida ya umeme, huwa unawaka usiku wa manane

View attachment 2755164
Wachapakazi
FB_IMG_1695178180578.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninawasiwasi huu mgao mkali wa umeme ni michezo ya kufungulia maji ya enzi za kikwete, huu mwaka una maji mengi sana ukilinganisha na mwaka 2017 kulikuwa na ukame hadi wanyama pori na wakufugwa walikosa maji na malisho wakafa, lakini hakukuwa na mgao wa umeme. Bwawa la mwl Nyerere limejaa maji kabla ya muda uliopangwa, hadi mda huu mito mingi Bado inatiririsha maji yenye ujazo unaoridhisha.Sababu waliyotoa ya kupungua kina cha maji, mimi binafsi naona sijashawishika.
 
Wana boost biashara ya solar power na magenerator....[emoji2960]
 
Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu

Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu

Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"

Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.


View attachment 2753272
This is a Stupid statement
 
Tanesco imesema Hapatakuwepo tena na Mgao wa Umeme bali patakuwa na Ratiba ya Upatikanaji Umeme

Kwahiyo Umeme utakuwa wa Ratiba

Taarifa ipo kwenye ukurasa Wao wa X
 
Tanesco imesema Hapatakuwepo tena na Mgao wa Umeme bali patakuwa na Ratiba ya Upatikanaji Umeme

Kwahiyo Umeme utakuwa wa Ratiba

Taarifa ipo kwenye ukurasa Wao wa X

Try kupaka kinyesi rangi nyeupe ili kiwe keki. Pathetic
 
Back
Top Bottom