Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu
Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu
Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"
Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.
View attachment 2753272
Unalipwa shilingi ngapi unapotetea ujinga?.shida kubwa ni uwelewa watanzania bado wameshindwa kutofautisha magao na hitilafu .
hivi vitu viwili naona vinawachanganya bado
[emoji1787][emoji1787]Hakuna mgao
Ila Kuna upungufu kwa hivyo watu wanapata umeme kwa zamu.
Hivi tukipata umeme kwa zamu, si ndio mgao wenyewe hhuo?
Nhdugu maharage umekula maharage ya wapi?
Tatizo ni viongozi tuliowaweka madarakani, kwa kura zetu, kuteua washikaji kuendesha mashirika nyeti. Serikali ndio inapaswa kubinafsishwa iendeshwe na DP World ili waweze kusimamia uendeshwaji wa mashirika ya Umma: TRC, TANAPA, TPA, TIRDO, na baadhi ya Wizara km TAMISEMIHalafu kelele za kuuza nchi utazizuia wewe, serikali ikifanya hivyo watakuja akina mbowe waseme watanzania wenyewe tunaweza kujiendeshea mashirika yetu, then Tec nao wataandika waraka!!
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]Kwani we hukusikia ripoti ya uchunguzi iliyotolewa juzi?
TANESCO wamegundua maeneo ya buza buza kushuka chini huko hakunaga matumizi ya msingi ya umeme
Zaidi ya kuchajia simu afu zikijaa muanze kusumbua mitandaoni na habari za Yanga.
Huo mtaa wako hauna jina?Moja kwa moja..
Ndani ya wiki moja siku kama Nne pamoja na leo umeme umekatika kuanzia asubuhi unarudi saa 1 kasoro au mishale ya Saa 1 usiku.
Hali hii imepelekea shughuli nyingi kukwama, ukosefu wa maji, watu kulalamika nk nipo Dar lakini kama naishi kijijini Chimba unye.
Je, mtaaani kuna hali kama ya mtaa wangu au ipo mtaa wangu pekee ?
#UziTayari
Tanzania wananchi tunapata shida sana. Mchana inzi usiku mbu.Ndio utaratibu kipindi hiki cha jua kali...mgao
Wananchi wa hali ya chini...makapuku...kajamba nani...walala hoi...wanyongwe...ndio tunapata shidaTanzania wananchi tunapata shida sana. Mchana inzi usiku mbu.
Sasa ukiangalia ishu ya umeme inaponyesha tu mvua tegemea umeme kukatika au kipindi kama hiki cha jua umeme unakatika pia.