TANESCO: Tuna upungufu, siyo mgao wa umeme. Wananchi endeleeni kuvumilia

TANESCO: Tuna upungufu, siyo mgao wa umeme. Wananchi endeleeni kuvumilia

Nadhani Tanesco wangekuwa wawazi tu kuhusu issue ya mgao ili raia nao wajipange. Mngetangaza ratiba ili mtu ajue kama atakuwa akifanya shughuli zake usiku (e.g welders) ama kama ni wale wa kununua bidhaa za kuoza basi wasitishe kununua ili kuepuka hasara. Sasa hivi mgao wa umeme usio na taarifa imekuwa ni kilio nchi nzima. Kuna mtu alitupa mamia ya mayai aliyokuwa anatumia machine ya umeme kuangulishia vifaranga kutokana na kuoza.

Sioni haja ya kuficha kuhusu mgao wa umeme ilihali kuna watu wanasafiri mkoa hadi mkoa kila siku na wanajionea hali halisi ya mgao ulivyo hasa kwenye mikoa iliyounganishwa na grid ya TAIFA.

Tatizo letu viongozi na watendaji wa Serikalini tumejawa ubinafsi na hatuwajali wengine. Viongozi hili swala la mgao haliwaumi maana wanajua umeme uwepo usiwepo wanapokea mshahara kama kawaida, nyumbani kwao wana majenereta ama strong solar system ambapo umeme wa Tanesco ukikatika wao wanaendelea kuwa na nishati. Wakisafiri kikazi wanafikia kwenye mahoteli makubwa yenye vyanzo mbadala vya umeme ambapo hata umeme ukatike haiwagusi.

Laiti kama viongozi ingekuwa kwamba riziki yenu inatokana na uwepo wa umeme basi mngejitahidi kutatua hii changamoto iliyopo ya umeme wa Tanesco.

Mheshimiwa Rais MAMa yetu Kipenzi, tafadhali ingilia kati hili swala maana wananchi wako waliokosa ajira wakaamua kujiajiri wanateseka na kukosekana kwa umeme. Wanateseka wana CCM,CHADEMA,ACT,NCCR na hata wasio na chama MAMA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA. WAJALIE VIONGOZI WOTE NA WALIOPEWA MAMLAKA KUWA NA HURUMA NA RAIA WAKE.
 
Yaani utadhani nchi ipo vitani, hawa viongozi mbona wanaelimu kubwa tu, ma Dr. Kibao kwanini kama taifa tusumbuke na tatizo moja kwa zaidi ya miaka 60?.

Au ni kweli asili yetu ni Sokwe?.
 
Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu

Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu

Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"

Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.

View attachment 2753272
Naona visingizio vya maji wamejua tumeshagundua. Tanesco ukweli kuna ufisadi mkubwa sana kuanzia ununuzi wa vifaa, waleta gas, miradi tofauti hivyo matatizo yanazidi kwasababu hiyo

Mawazo ya kuibadilisha TANESCO

Umeme wa Maji Tanzania ni 36.64% tu ya umeme wote
 
Halafu kelele za kuuza nchi utazizuia wewe, serikali ikifanya hivyo watakuja akina mbowe waseme watanzania wenyewe tunaweza kujiendeshea mashirika yetu, then Tec nao wataandika waraka!!
Kama huna chakuchangia bora uache.
 
Jibu jepesi ni kwamba kazi imewashinda, mpo bize kupiga dili tu, bodi ivunjwe
 
Akizungumza leo September 18 katika kipindi cha #Supa Breakfast cha East Africa Radio, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndugu Maharage Chande amedai kuwa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme bali kuna upungufu

Wateja na wananchi watuvumilie katika kipindi hiki najua ni kigumu kuvumilika na kuelekeweka lakini wafanyakazi wanajitahidi, wizara inajitahidi na serikali inajitahidi kuhakikisha tunatatua changamoto, vile vile uchumi unakua sana kwahiyo ni vizuri na mahitaji ya umeme yanaongezeka, tuko katika kushindana kuzalisha na matumizi ambayo ni mashindano mazuri kwa ustawi wa nchi yetu

Katika mitandao ya umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara maeneo mbalimbali huwezi kusema utakuwa na mtandao wa umeme isitokee hitilafu na pale zinapotokea wateja wetu huwa wanafahamishwa lakini pale ambapo tunapata upungufu"

Siyo kwamba nchi nzima hakuna umeme, kuna baadhi ya meeneo yanakosa na pia tunatoa taarifa kwenye hayo maeneo, ni vizuri mwananchi apate taarifa na tumekuwa tukitoa taarifa na tutaendelea kufanya hivyo.

View attachment 2753272
Yaani huyu sijuhi tu, contradictory statements kama zote. Upungufu si unasababisha mgao. What a DG?
 
Hakuna mgao
Ila Kuna upungufu kwa hivyo watu wanapata umeme kwa zamu.
Hivi tukipata umeme kwa zamu, si ndio mgao wenyewe hhuo?
Nhdugu maharage umekula maharage ya wapi?
Sio mkenya ni mswahili huyo, ukipenda utaelewa usipende utaelewa!
 
Upungufu wa umeme na mgao wa umeme tofauti yake ni ipi?
Nitajaribu kukujibu samahani lakini,
Upungufu unatokana na uwezo mdogo wa uzalishaji.
Mgao unatokana na maamuzi tu kwasababu zao wanazozijua wao wenyewe.wapi tuwashe au wapi tuzime.
 
Screenshot_20230918-191130.jpg
 
shida kubwa ni uwelewa watanzania bado wameshindwa kutofautisha magao na hitilafu .
hivi vitu viwili naona vinawachanganya bado
 
shida kubwa ni uwelewa watanzania bado wameshindwa kutofautisha magao na hitilafu .
hivi vitu viwili naona vinawachanganya bado
 
Back
Top Bottom