Kangosha
Member
- Sep 18, 2023
- 52
- 135
Nadhani Tanesco wangekuwa wawazi tu kuhusu issue ya mgao ili raia nao wajipange. Mngetangaza ratiba ili mtu ajue kama atakuwa akifanya shughuli zake usiku (e.g welders) ama kama ni wale wa kununua bidhaa za kuoza basi wasitishe kununua ili kuepuka hasara. Sasa hivi mgao wa umeme usio na taarifa imekuwa ni kilio nchi nzima. Kuna mtu alitupa mamia ya mayai aliyokuwa anatumia machine ya umeme kuangulishia vifaranga kutokana na kuoza.
Sioni haja ya kuficha kuhusu mgao wa umeme ilihali kuna watu wanasafiri mkoa hadi mkoa kila siku na wanajionea hali halisi ya mgao ulivyo hasa kwenye mikoa iliyounganishwa na grid ya TAIFA.
Tatizo letu viongozi na watendaji wa Serikalini tumejawa ubinafsi na hatuwajali wengine. Viongozi hili swala la mgao haliwaumi maana wanajua umeme uwepo usiwepo wanapokea mshahara kama kawaida, nyumbani kwao wana majenereta ama strong solar system ambapo umeme wa Tanesco ukikatika wao wanaendelea kuwa na nishati. Wakisafiri kikazi wanafikia kwenye mahoteli makubwa yenye vyanzo mbadala vya umeme ambapo hata umeme ukatike haiwagusi.
Laiti kama viongozi ingekuwa kwamba riziki yenu inatokana na uwepo wa umeme basi mngejitahidi kutatua hii changamoto iliyopo ya umeme wa Tanesco.
Mheshimiwa Rais MAMa yetu Kipenzi, tafadhali ingilia kati hili swala maana wananchi wako waliokosa ajira wakaamua kujiajiri wanateseka na kukosekana kwa umeme. Wanateseka wana CCM,CHADEMA,ACT,NCCR na hata wasio na chama MAMA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. WAJALIE VIONGOZI WOTE NA WALIOPEWA MAMLAKA KUWA NA HURUMA NA RAIA WAKE.