TANESCO: Tunawashauri wateja wetu kununua umeme kupitia vituo vya mawakala wetu wa LUKU nchi nzima

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453. DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA CHANGAMOTO YA MANUNUZI YA UMEME

Jumamosi 27 Disemba, 2025

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kumetokea changamoto ya manunuzi ya umeme (LUKU) hali inayosababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia njia za mitandao ya simu, na njia za kibenki.

Tayari Watalaamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa GePG wanashughulikia changamoto iliyojitokeza ili huduma iweze kurejea katika hali ya kawaida.

Tunawashauri wateja wetu kununua umeme kupitia vituo vya mawakala wetu wa LUKU nchi nzima.

Shirika litawafahamisha wateja wake huduma zitakaporejea kikamilifu.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

 
Nanlii hole countries, labda mawakala wameona commission zimeshuka wakaona ifanyike namna. Najaribu kuwaza kimoyomoyo.
 
similar



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…