TANESCO: Kuna tatizo katika mfumo wa kununua Umeme, Wataalam wanaendelea kurekebisha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-04-05 at 08.00.57_1a140e23.jpg

Muda mfupi baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamika kuwa kuna changamoto ya umeme kupitia andiko lake ~ Kwa zaidi ya 10 hrs sasa tangu jana mitandao na benki zote zinagoma ku-access malipo ya LUKU, hii shida ni kwangu tu? Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi na kukiri kweli kuna changamoto.

TAARIFA KWA UMMA
CHANGAMOTO YA MANUNUZI YA UMEME KWENYE MFUMO WA LUKU
APRILI 5, 2025.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna changamoto kwenye manunuzi ya umeme (LUKU) inayosababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia mitandao ya simu na njia za kibenki kuanzia leo majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi.

Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurekebisha changamoto iliyojitokeza ili kuwezesha manunuzi ya umeme kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

Kwa sasa tunawashauri wateja kufanya manunuzi ya tokeni za umeme kupitia njia mbadala za mawakala waliopo nchi nzima wakati hatua za utatuzi zikiendelea.

Tutawataarifu huduma itakaporejea Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

IMETOLEWA NA;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA, TANESCO-MAKAO MAKUU, DODOMA.
 
Yaani hii nchi kuna wakati unajiuliza tumepatwa na nini na hupati jibu.
Hivi sasa ni zaidi ya masaa 10 mifumo ya kununulia umeme kupitia mitandao haipo hewani na Wahusika yaani Tanesco wako kimya tuu.
Nilidhani ukale huu uko kwenye siasa tu ambako bado wanawatumia watu kama STEVEN WASSIRA katika kipindi ambacho hawaendani nacho kumbe hata kwenye mashirika yanayotegemewa na nchi au idara za serikali bado wapo ambao ni Business as usual kwa kila kitu.
Tanesco tuelezeni kulikoni? Na tufanyeje sasa?
 
Wanazingua sana na wanakata saa 3 asubuhi kurudi mpaka saa 5 usiku luku toka jana zinaleta usumbufu na Kodi zao za kumkandamiza mtanzania wiki hii ndio wanaendelea kuiba zile unit 5
 
Muda mfupi baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamika kuwa kuna changamoto ya umeme kupitia andiko lake ~ Kwa zaidi ya 10 hrs sasa tangu jana mitandao na benki zote zinagoma ku-access malipo ya LUKU, hii shida ni kwangu tu? Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi na kukiri kweli kuna changamoto.

TAARIFA KWA UMMA
CHANGAMOTO YA MANUNUZI YA UMEME KWENYE MFUMO WA LUKU
APRILI 5, 2025.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna changamoto kwenye manunuzi ya umeme (LUKU) inayosababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia mitandao ya simu na njia za kibenki kuanzia leo majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi.

Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurekebisha changamoto iliyojitokeza ili kuwezesha manunuzi ya umeme kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

Kwa sasa tunawashauri wateja kufanya manunuzi ya tokeni za umeme kupitia njia mbadala za mawakala waliopo nchi nzima wakati hatua za utatuzi zikiendelea.

Tutawataarifu huduma itakaporejea Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

IMETOLEWA NA;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA, TANESCO-MAKAO MAKUU, DODOMA.
Watakuambia ndio maana tunamtaka mhindi aje kuwekeza.
Kwani haujasikia lile jinamizi limefufuka na Tanesco wanadaiwa ?
 
Yaani hii nchi kuna wakati unajiuliza tumepatwa na nini na hupati jibu.
Hivi sasa ni zaidi ya masaa 10 mifumo ya kununulia umeme kupitia mitandao haipo hewani na Wahusika yaani Tanesco wako kimya tuu.
Nilidhani ukale huu uko kwenye siasa tu ambako bado wanawatumia watu kama STEVEN WASSIRA katika kipindi ambacho hawaendani nacho kumbe hata kwenye mashirika yanayotegemewa na nchi au idara za serikali bado wapo ambao ni Business as usual kwa kila kitu.
Tanesco tuelezeni kulikoni? Na tufanyeje sasa?
Comment yako imenichekesha sana
 
Mimi nazani Tanzania ndo nchi inayoongoza kwa watu kutokuwa na furaha yani pesa zetu zinatutesa pia umeme unakatika almost masaa 16 kwa siku haupo kabisa.
 
Ndiyo tatizo la wanasiasa kuleta ujinga kwenye maswala ya kitaalam.

Tanesco kumonopoly soko ndiyo shida ,wabadili sheria watu binafsi wasambaze umeme ,kuwe na kampuni nyingine kama tanesco kuwe na ushindani....Tanesco kuwa peke yao akili zimelala wanajua hatuna cha kuwafanya.

Wafanye kama kampuni za simu ,ukiona mtandao huu unazingua unatoa line unatumia mtandao mwingine ,the same ukiona tanesco wanazingua chap unaomba connection ya umeme kampuni nyingine.
 
Back
Top Bottom