TANESCO yaahirisha zoezi la uzimaji wa mfumo wa mitambo ya LUKU kwa siku 4

Wanaupdate vipi hiyo mysql database kwa siku 4

Mbona utani umekuwa mwingi sana kwa taasisi za serikali za Tz
 
Tangazo lao lilikuwa halieleweki na hivyo kuleta mkanganyiko mkubwa!
Nafikiri walikusudia kuandika; Luku itazimwa saa nne usiku hadi saa moja asubuhi kila siku kwa muda wa siku nne hivyo ndani ya hizo siku nne wananchi wanashauriwa wanunue luku muda wa mchana au kabla ya muda huo ili kuepuka usumbufu.
Ilikuwa ni marekebisho ya kawaida ila kilicholeta mtafaruku ni tangazo lenye makosa ya kisarufi/halieleweki!
 
Hawa tanesco na kipara wao miyeyusho kweli! Huenda wamebadili Nia Yao baada ya kuisoma luku yangu niliyoijaza token saa moja iliyopita ili nikwepe kero za kulala Giza! Wameniharibia bajeti yangu kabisa! Kipara nitakuotesha nywele ipo siku!
 
unarudi pale pale
umesoma tangazo vizuri wamesema ni kuanzia saa 4 usiku mpk saa 1 asubuhi kwa siku 4
sio kwamba HUDUMA haitapatikana kwa SIKU 4 mfululizo
mchana itakuwepo
kwani usiku napo hakuna umuhimu,ni uzembe tu wa wataalamu wetu
 
Je Tanesco kuzima issue ya LUku hizo tarehe 22-25 ambazo ni siku za sensa hawaoni kama ni tatizo kwa nchi.

Sensa itahtaji umeme muda wote kwenye kila KATA
Akili ndogo ya Januari makamba. Na Rais analiona hili lakini hachukui hatua.
 
Unategea wakati wa sensa. Akili ya kichwa au tundu kuu?
 
unarudi pale pale
umesoma tangazo vizuri wamesema ni kuanzia saa 4 usiku mpk saa 1 asubuhi kwa siku 4
sio kwamba HUDUMA haitapatikana kwa SIKU 4 mfululizo
mchana itakuwepo
Sijui mnaelewa maana ya usiku wa manane ? Ilipaswa iwe saa nane mpaka saa kumi usiku mwisho hata zikiwa siku nane sio mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…