HATUPELEKI CHAMA KWA MASHOGA - WANACHAMA WA CHADEMA
Katika uchaguzi mkuu wa kumtafuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sauti za wanachama na wajumbe zimetanda mithili ya wingu la mvua, wakiimba kwa nguvu, "Hatupeleki chama kwa mashoga."
Wimbo huo wa aina yake, umevuma kwa kujaza hewa nzito ya msimamo katika ukumbi huo wa uchaguzi.
Wanachama hao, wakiwa na hasira za dhahiri, wamepinga kwa sauti ajenda za kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja, zinazotetewa na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu.
Wamesisitiza kuwa hawako tayari kupeleka chama kwa viongozi wanaotetea vitendo vya ushoga na mapenzi ya jinsia moja kwa ujumla.
Kwa msimamo wa chuma, wameonesha kutokubaliana kabisa na ajenda hizo za kigeni, wakieleza kuwa hazina nafasi katika chama chao.
Wahenga hawakukosea waliposema, "Kila ndege huruka na mbawa zake mwenyewe," kwani tayari wanachama wa CHADEMA wameonesha msimamo wa kuzikataa mbawa za kigeni zilizoletwa na Lissu na genge lake
Kasuku
Januari 21, 2025
kutoka ukumbi wa uchaguzi, Mlimani City - Dar es salaam