Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Status
Not open for further replies.

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

========
Moderator:

JamiiForums imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hii ni ya uwongo na hivyo mjadala umefungwa.
 
Daaaah asante sana hawa wanyonyaji......

Magufuli akifanikisha hili nitamuunga mkono kwa Mara ya kwanza......

Sina utani katika vitu ambavyo vilikuwa vinaniuma ni huu mkataba wa kishenzi sana.

Tuungane kupinga hii mikataba ya kulinyonyaji katika taifa letu...

Ushauri tushushe pia bei ya umeme....

Ingia kote kabisa wafulumushe mafisadi hii nchi waliigeuza shamba lao pekee.....
 
Mungu Mkubwa, JAMANI Huyu mdudu IPTL hivi atakwisha lini? Rais JPM naomba uanze Kunyonga watu hasa wale waliosaini mkataba wa kuiongezea muda kampuni hii kinyume cha mkataba.

Hili lidudu IPTL ni la nani? kwa nini linaisumbua nchi hivi?

Tena ikibidi JPM Angusha Kombora kwenye mitambo yao tu kama hujuma, tumechoka, nimechoka, bora nchi iwe na mgao kuliko kuwa na hili lidubuwasha
 
Hapo JPM amecheza vizuri sana, sasa ni kwamba fedha zote ambazo walitakiwa kulipwa hao IPTL zimesitishwa nadhani wanasubiri rufaa iliyokatwa na TANESCO, kama TANESCO wakishindwa kesi basi fedha hizo walipwe Standard charted tu.

huo mtambo wa IPTL utaifishwe tu, nadhani na IPTL wanaweza kuacha kutuuzia UMEME, hapo ndo patamu ili mkataba uvunjwe tu
 
Mkuu taarifa kutoka chombo gani cha habari?
Tafadhali tupe chanzo cha habari.
 
Tunachezewa shele za kisheria. TANESCO watapelekwa mahakamani na kudaiwa hizo pesa pamoja na riba.

Ningeelewa kama tungefanikiwa kuvunja hii mikataba.

Ni matumaini yangu hizi pesa zitafunguliwa akaunti nyingine ya ESCROW
 
hamna. sema watu sasa wameshiba.
 
Nadhani itabidi fedha hizo ziwekwe kwenye ESCROW ACCOUNT
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…